Nakubaliana na wewe Kuwa upinzani umeimarika hila lazima pia Pamoja na figisu zinazotoka nje ya UKAWA tuangalie na makosa ya Kiufundi ndani ya UKAWA.Hapa natoa mfano kwa baadhi ya Majimbo ya Kagera.Wenyeviti wa Chama mkoa wa Kagera hasa Karagwe waliingilia Sana mfumo wa kura Za maoni.Huu ungonjwa ulikuwa CCM sasa umevamia CHADEMA.Jimbo la Karagwe ilikuwa wazi upinzani ungeshinda kwa sababu ulikuwa na nguvu lakini makosa yaliyofanyika ni pale badala ya kumsimamisha mgombea aliyepata kura nyingi kura za maoni Yaani Deus Kahangwa ,mwenyekiti wa Karagwe akishirikiana na mama wa viti maalum Konchesta walipiga fitina kwa viongozi wakuu na kumsimamisha mgombea aliyeshika no 2 Yaani Prince Rwazo ambaye alikuwa hakubaliki na wananchi.Hivyo wana Karagwe walikasirika na kupigia CCM.Vile vile huyu mama wa viti maalum akiingilia mchakato wa kura Za maoni Katika jimbo moja la Mleba wakamsimamisha mshindi wa tatu Ngurumo badala ya Najim wa CUF ambaye alikuwa a akakubalika wa wananchi.Hivyo Majimbo mawili yamepotea kwa ajili ya viongozi hawa.Hata upande wa viti maalum amevuruga na kusambaza fitina akishirikiana na huyo mwenyekiti wa Karagwe hadi kusababisha Kagera kupata kiti kimoja cha viti maalum ambacho kapewa yeye mwenyewe na mwaka 2010 Alipewa ingawa hata mchango wake haukuwahi kuonekana.Mbaya zaidi anatamba Kwamba Kama mtu hamtaki hawezi kujpitshwa na chama.Wana Kagera tunajiuliza huyu mama na huyu mwenyekiti wa Karagwe wanavuruga upinzani Kagera kwa maslahi ya Nani?Bila viongozi wakuu kwenda kuwasikiliza wana Chama katika Majimbo hayo 2020 tusitegemee UKAWA kuchukua Majimbo hayo Kagera .