Uchaguzi 2020 Naipongeza NEC kwa utaratibu mzuri wa zoezi la kupiga kura leo

Ndo hivyo sasa, sisi wenyewe tunapambana mpaka tujikomboe
huwez kujikomboa kama haki na uhuru wako unaminywa na Dola... Ni ngumu

kuna mtu alinitolea mfano wa Hitler kwamba huwez maendeleo hayaji bila kuwa dikteta ko meko yupo sahihi nikamjibu Hitler alijali sana maendeleo ya watu na taifa ndo maan kipind chake hakukuwa na ukosefu wa ajira....
 
IMG_5785.png

Je mtatangaza
 
Nilikua wakala wa kituo idadi ya kura ya mgombea udiwani na uraisi ni tofauti wakati kila mpiga kura alipewa karatasi sawa..


Akuna Uhuru msijidanganye!
Mpiga kura anaweza kumpigia kura Rais na akaharibu kura ya Diwani au mbunge na hivyo hesabu isiwe sawa kwa kila ngazi. Hili ni suala la behaviour za mpiga kura. Muhimu ni kuwa kura zilizopigwa kituoni haizidi idadi ya waliojiandikisha kwenye kituo hicho.
 
Tatizo ni kuwa tume ndiyo yenye mamlaka pekee ya kutangaza matokeo. Hata wewe hapa unavunja sheria kwa sababu source ya hiyo habari yako haiaminiki na ukikabwa sawa sawa sijui kama utaweza kuthibitisha kuwa matokeo hayo ndiyo sahihi. Na tume ikishatangaza matokeo yake hayahojiwi wala kupingwa mahakamani.

Wapinzani elekezeni nguvu zote kwenye kupata katiba mpya ili muweze kufuta haya masheria ya hovyo haya. Rais aondolewe kinga zote. Kuwe na taasisi huru (mf. Tume ya uchaguzi, mahakama). Matokeo yapingwe...na mengine mengi kama yalivyoainishwa kwenye tume ya Warioba. Vinginevyo kila mwaka mtakuwa watu wa kulalamika na kulia lia mitandaoni humu...

Kuwa na katiba inayoeleweka na taasisi huru ni muhimu sana. Trump ni dikteta kabisa lakini pamoja na juhudi zake zote anakwama. Akigeuka huku anakuta jaji fulani kapiga chini mojawapo ya matamko yake, huku taasisi fulani imekataa kufuata maelekezo...). Hizi checks and balances zinasaidia sana...

(Dina; nakuheshimu sana. Usiniporomoshee matusi pulizi )
 
Kwa mjibu wa taarifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari zikiwemo ITV, AZAM, CHANNEL 10, TBC na Online TVs karibu kila kona ya Tanzania zoezi la upigaji kura limeenda vizuri na kasoro nyingi zilizozoeleka kufanyika mwaka huu hazikuonekana na upigaji kura ulifanyika kwa amani na utulivu.

Nawapongeza NEC kwa hatua hii, kamilisheni hatua zilizosalia pia kwa uweledi. Nawaomba watanzania tupuuze madai machache yanayodai kupigwa kwa kura feki.

Kwa utaratibu wa kura za mwaka huu kila kura inayopigwa lazima serial number yake irekodiwe mbele ya mawakala wote. Hivyo hakuna namna kura feki inaweza kupigwa na isionekane wakati wa kulinganisha kura zilizopigwa na zile zenye serial numba zilizorekodiwa. Hivyo tuzipuuze.
Naipongeza NEC kwa uwizi wa kihistoria wa kura,mtu anakutwa na kura 5000 yani ni uchafuzi sio uchaguzi
 
Naipongeza NEC kwa uwizi wa kihistoria wa kura,mtu anakutwa na kura 5000 yani ni uchafuzi sio uchaguzi
Mmeombwa na NEC kutoa ushahidi, hakuna yeyeto liyethubutu hata kutoa chemba ya ushahidi. Ni kauli tu za mfa maji
 
Naunga mkono hoja, uchaguzi huu umeendeshwa vizuri sana, ilikuwa ni uchaguzi huru na wa haki. Atakashinda, ameshinda kwa haki na halali na aliyeshindwa, ameshindwa kwa haki. Mshindwa ampongeze mshindi, maisha yaendelee.
P
Kama wanalalamika ni haki yao kuthibitisha malalamiko yao
 
Back
Top Bottom