NEC yataka ushahidi vituo hewa vya wapiga kura kutoka kwa Wanasiasa wanaosambaza taarifa hizo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewataka wanasiasa na wagombea wanaodai kuwepo kwa vituo na wapigakura hewa kupeleka ushahidi na endapo wakishindwa kufanya hivyo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.

Akizungumza leo na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Mkurugenzi wa Tume hiyo, Dk.Wilson Charles amesema tuhuma hizo zinaleta kuzua taharuki kwa jambo ambalo si la kweli.

Aidha, amesema vituo vya kupigia kura ni vingi kuliko vya kujiandikishia kwa sababu kila kituo wameweka idadi ya wapigakura wasiopungua 500 ili kurahisisha zoezi la upigaji kura.

"Vituo vilivyotumika kuandikisha wapiga kura vilikuwa 37,814,na vituo vya kupigia kura ni 80,155, hii inatokana na kwamba kwenye kituo kimoja kilichotumika kujiandikisha kinaweza kutoa vituo vitatu kwa sababu kituo kimoja kinatakiwa kuwa na wapiga kura 450 hadi 500," amesema

Amewataka wagombea wa kiti cha Urais na Makamu wa Rais kuzingatia ratiba toleo la sita ya kampeni iliyotolewa na Tume.

Mkurugenzi huyo, amesema Tume imejiandaa vizuri katika uchaguzi huo na kwamba tayari vifaa vyote muhimu leo vitakuwa vimefika kwenye majimbo ya Tanzania bara na Zanzibar.

"Pia Tume inawataka wasimamizi wa majimbo wafikishe kuanzia leo vifaa kwenye vituo vya kupigia kura ili kusijitokeze dosari zozote kwenye uchaguzi ikiwemo kuchelewa kwa vifaa na kufunguliwa vituo," amesema.


IppMedia
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewataka wanasiasa na wagombea wanaodai kuwepo kwa vituo na wapigakura hewa kupeleka ushahidi na endapo wakishindwa kufanya hivyo hatua stahiki zitachukuliwa dhidi yao.
Hawa Tume hawaaminiki.. Ni kama mwizi wa kuku, hata akikutwa na kuku aliyeiba au mnofu anaruka kimanga.

Ile orodha ya wapiga kura inayojumuisha majina hewa wameiandaa wao na kuisambaza, afu wanadai wapelekewe!!!
 
Bwana Zungu, Naibu Waziri Mazingira, ameonekana kwenye video clip akiwafundisha watoto wa shule chini ya miaka 18 namna ya kumpigia kura za ndio Magufuli. Wamejifungia ndani ya chumba.

Tume ituambie, hawa watoto watapiga kura kituo gani? Kwa nini Zungu mpaka leo hajakamatwa?
 
Huyu Mahera naona anataka kuwafundisha watu kazi, hao wanasiasa anaowasema wana experience na hiyo kazi zaidi yake, asitake kuwatisha watu, na kama wakithibitisha kuna wapiga kura feki na vituo hewa na yeye atuambie ataachia hiyo ofisi aliyopewa kama zawadi.
 
Siasa sio chanzo cha vita Ila wanasiasa ndio chanzo cha Vita

Wanapenda zaidi maslahi Yao kuliko wapigakura wao!!

Wako tayari kuwaona wapigakura wao na wananchi wakipoteza maisha Yao na wengine kuwa walemavu wa maisha ili wao waende Ikuru.

Hakuna hata mmoja atakayepeleka huo ushahidi, Ni uchochezi tu na si vingine.
 
Tume inajidhalilisha kuendelea kuwajibu Hawa Jamaaa zetu wenye Sacco's.
Wawazoee Sasa na ubwatukaji wao

We watu walokuaminisha Lowasa Ni fisadi na kuuaminisha umma Wana ushahidi wa kutosha ,ghafla wanapiga gia angani na kumchukua walomtaja fisadi kua mgombea wao na kuomba ushahidi Tena wa ufisadi wa lowasa Ni wa kuwaamini hao!
 
Bwana Zungu, Naibu Waziri Mazingira, ameonekana kwenye video clip akiwafundisha watoto wa shule chini ya miaka 18 namna ya kumpigia kura za ndio Magufuli. Wamejifungia ndani ya chumba.
Halafu huyu Azzan Zungu wa ccm anayefundisha UDANGANYIFU kwa watoto "underage" naye ni mgombea, na ugombea wake haubatilishwi!
 
Halafu huyu Azzan Zungu wa ccm anayefundisha UDANGANYIFU kwa watoto "underage" naye ni mgombea, na ugombea wake haubatilishwi!
Tunaitaka NEC iifanyie kazi hili JAMBO haraka kabla ya uchaguzi. Mbinu chafu imebuma. Watoto hawawezi kutayarishwa kupiga kura kawa NEC haijawaandalia kituo hewa.
 
Wakipewa ushahidi watafanya nini wakati jaji wa tume hana hata ubavu wa kuwadhibiti wakurugenzi? Wakati.

Tume inayoongozwa na jaji inawarudisha wagombea waliokatwa na wakurugenzi,majina yanapofika kwa wakurugenzi wanayakalia bila kuwapa barua waliorudishwa na hawafanywi chochote.
 
Back
Top Bottom