NEC yatangaza nafasi ya kazi kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kwa Jimbo la Konde

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
499
1,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza nafasi ya kazi kwa Wasimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi kwa Jimbo la Konde.

Utaratibu huu ni tofauti na utaratibu wa awali ambapo Wasimamizi wa Uchaguzi wa Majimbo kwa Zanzibar walikuwa wakiteuliwa moja kwa moja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi na wengi wao wakiwa Makada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) au wafanyakazi katika vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa kuzingatia kuwa Chama chetu kiliiandikia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuhakikisha kuwa waliohujumu Uchaguzi wa marudio wa Jimbo la Konde hawarejeshwi kusimamia uchaguzi ujao, tunaunga mkono hatua hii.

Hata hivyo, hatua hii itakuwa na maana iwapo NEC itahakikisha kuwa wanaoteuliwa siyo Makada wa CCM, Watumishi wa Vyombo vya ulinzi na usalama au watumishi ambao rekodi zao za upendeleo wa kisiasa zinafahamika. Chama chetu kinafuatilia kwa karibu mchakato huo kuhakikisha haki inatendeka.

Hatua hii ilipaswa pia kuwagusa Wasimamizi wa Vituo vya Kupigia Kura ambao ndio wamekuwa ni waharibifu wakubwa wa uchaguzi.

Pia, Chama chetu kinatoa rai kwa NEC kutangaza nafasi kwa Msimamizi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Ushetu na kuachana na Wakurugenzi wa Halmashauri ambao wengi wao ni Makada wa Chama Cha Mapinduzi.

Katika kuhitimisha, tunaendeleza wito wetu kuwa Katiba na Sheria za Uchaguzi ziandikwe upya ili Tume ya Taifa ya Uchaguzi ifanye shughuli zake kwa uhuru. Tunatoa rai kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa mchakato huo uanze sasa.

Ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi iwe na watumishi wake wanaowajibika kwa Tume tena wasiwe makada wa Chama chochote cha siasa ili uchaguzi uwe huru, haki na wa kuaminika.

Imetolewa na

Salim A. Bimani,
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
ACT Wazalendo.
01 Septemba, 2021.
Screenshot_20210901-170248_1.jpg
 

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
43,916
2,000
NEC ni ile ile maana wataopita ni lazima NEC ndio iwapitishe,Je utajua viapo vyake mpaka wapewe kazi?
 
  • Love
Reactions: BAK

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,997
2,000
Nyie ni WASALITI wa Watanzania mnakubali kutumika na maccm kwa yale yanayowanufaisha nyinyi tu huko Zenj badala ya kupigania mabadiliko makubwa kwa Tanzania nzima. Ayatollah Zitto ni msaliti tu!!
 

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
30,373
2,000
Nyie ni WASALITI wa Watanzania mnakubali kutumika na maccm kwa yale yanayowanufaisha nyinyi tu huko Zenj badala ya kupigania mabadiliko makubwa kwa Tanzania nzima. Ayatollah Zitto ni msaliti tu!!
Zito akili zake anazijua mwenyewe. Konde inamsaidia nini katika mustakabali wa Tanzania yenye demokrasia? Huyu mtu huwa ni opportunistic, sijui huwa anawaza nini?

Achana na Konde, pigania mambo ambayo yatakuweka katika mizania sawa na CCM katika ushindani na hapo utamshinda maana wameshamchok wapiga kura. Bila Katiba mpya unajisumbua maana Samia hatakubali kunyanganywa urais....
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
25,999
2,000
Si wamtangaze wa CCM kashinda tu yaishe kusumbua wananchi na kutupa hela bure si vzr
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom