Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

Sio porojo hizi

Story ina mengi ya kujifunza

Watu kujadili ni kama kawa.. na umeona sala zimefungua wengi. Amina
Ni kwel kabisaa.Hii inaonyesha weng humu maombi ni kizungu.halaf mbona mitazamo ya weng inaonekana kama ni suala la wanawake tu katika nyumba.Mbona sie wengine wanaume tupo tu tunaopiga prayers mpaka wake zetu wanasubir??
 
Hapo ndio uone wanaume wenzako wengine hawasali kabisaaa..
 
FB_IMG_1563278602911.jpg

SEHEMU YA AROBAINI NA TANO
Daniel anaonekana kunihitaji mimi kwenda Uganda,ni swala la mimi kumkumbusha na kumuelezea kwamba ninauhitaji wa kwenda huko Sina ninachofanya kazi yangu ni nini? Nilikuwa nawaza muda wote,njia pekee ni kuendelea kuwasiliana na Daniel kimahaba,kwa lengo la kumtamanisha mimi kumfuata Uganda. Niliamka na kujiandaa kwa ajili ya kwenda shuleni kuendelea na driving school yangu. Ninatamani kuweza kuendesha gari. Fadhili hapatikani, simuoni kabisa sijui kakamatikia wapi. Lakini Fadhili wa nini? Ni kweli ana mapenzi ya dhati, lakini hapatikani, na tangu aniahidi kuwa na biashara ni muda sasa, na sina biashara ninayoifanya zaidi ya kupiga ukware tu. Je sin i bora niwe na Daniel ambaye ana kazi nzuri, nimeshajua familia yake na maisha yake, nitasaidika, na kaniahidi kuweza kunisaidia kimaisha. Lakin pia mwanaume ambaye hajawahi kuwa nam ahusiano ya mapenzi nje huyu ndiye mtamu, nitammudu na kumkomesha, na ninataka awe wangu a maisha, nikae naye maisha yote, yani huyu hana ujanja, nitamnyosha.
Niliondoka na kuelekea kwenye shughuli zangu, hasa kufuatilia nione kama nitapata kitambulisho cha kusafiria cha muda na pia kwenye shule yangu kisha misele ya hapa na pale. Nikiwa natoka nje nilishangaa mpaka moyo wangu ukashtuka,, paaa.. Sikuamini, nilishtuka sana kumuona baba Davis,, Mh.. nilijiuliza kaja kufuata nini?Sijamuona muda, sijamuona kitambo. Habari Marino? Alinisalimia akiwa amesimama nje ya geti,, salama nilimjibu. namfahamu ni mwanaume wa hasira nyingi sana na mgomvi mgovi tu. Karibu nilimkaribisha. Asante sikaribii maana sina uhakika mwenye nyumba akija atanielewaje. Samahani naomba tuongee hapa nje kidogo. Baba Davis aliniomba tuongee. Dah,, nilishangaa sana kwa upole wake. Nimekuja na karatasi hizi, ninaomba tufike kweye baraza la usuluhishi kwani ninahitaji tu talaka, sitaweza kuendelea kusubiri kwani tayari una utaratibu wako mwingine wa maisha, na nimeshafuatilia mudda mrefu na kugundua kwamba una mwanaume ambaye anakuhudumia na kukuweka mjini. Hivyo ninaomba tu tuachane kisheria. Na hapa nina karatasi ambazo kama hutajali nitaomba uzisome na kisha uniambie lini utakuwa na nafasi basi tufike kwenye ofisi husika kwa ajili ya kumaliza swala hili. Baba Davis alikuwa anaongea kwa upole sana. Nilimtizama huku naye akinitazama kwa kunikagua sana, Nilitabasamu na kumwambia, ninaomba kuwaona watoto , Alitabasamu na kusema utakua ni mwanamke ambaye hana akili kabisa, hapo kidogo nikaona kama ana jazba..
Nikamuacha,, nilichukua zile karatasi, kisha nikamwambia, basi ninasafiri kwenda Uganda, nikirudi nitakujulisha kisha tutaonana.
Uganda? Alirudia hiyo sentensi ni kama hakuamini, Ndio , Uganda, nilimjibu. Okay, aliitika na kuniachia zile karatasi. Na nilikuwa na ufunguo wa gari yangu, nilifungua gari na kuweka zile karatasi akiniona na hakusema lolote. Aliondoka na kuniacha, lakini alikuwa akinishangaa sana. Nilikuwa nimependeza sana, uvaaji wangu, kama wasichana wa mjini kabisa, silei, sifanyi kazi, sijichoshi nakula na kulala tu, tena nakla vixzuri na kulalavizuri, na sikosi laki tatu laki tano, kwa nini nisipendeze? Nilkkuwa nimependeza sana. Aliondoka na kuniacha.
Alipotoka tu, niliita namimi taksi kisha nikaondoka kuelekea kwenye mizunguko yangu.Nikiwa ndani ya Taksi, nilishangaa sana, kuona simu yangu ikiita na aliyekuwa anapiga ni Fadhili.. dah , nilishangaa sana.
Hii mamiiiii.. alisema kama kawaida yake.. akiwa anaonekana ana furaha sana. Nilimjibu hiii, nikiwa na sauti ya upole. Mbona umekuwa mpole mamii? Mpenzi wako nimekuwa busy natafuta pesa mama yangu.. vipi? Mbona umepotea? Aliniuliza. Hapana nipo, nimekuwa tu busy sina mbele wala nyuma. Tulia, mpenzi wako nimepata pesa uko wapi nikupe ile pesa uliyokuwa unaitaka ya biashara? Fadhili aliniuliza. Dah,, karoho kalidunda juu juu, pesa ten,, nilimjibu naenda shule, nimeanza driving school ndio naenda huko . Nooo, alniambia nooo nimekumiss san asana sana. Natka kuwa na wewe leo. Aliniomba niwe naye.
Hapana naomba nitoke shule kisha nikimaliza darasa nitakurudia. Lengo ilikuwa ni kupitia pia ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kufuatilia kama nitapata pasi ya kusafiria yamuda, kwani nilikwa nina pete ambayo ni lazima Daniel aivae ili lengo langu litimie. Sawa , ila ukitoka basi shule uniambie, Sawa hakuna shaka, nitakujulisha.
Fadhili alinishangaa sana Marino amekuwaje na ujasiri wa kumkatalia, sio kawaida. Sio kawaida kabisa, haiwezekani , Alizoea akisema lolote lile Marino anafuata muda ule ule, hivyho aliingia wivu, na saa alitamani kuanza kumfuatilia, na kwa vile Marino alimuelekeza shule na sehemu anapojifunzia kuendesha gari alienda mpaka pale, na kweli alimkuta pale. Na alimsalimia tena kwa kumkumbatia, na kama waliokwua pale hawajui historia ya Marino na Fadhili basi wangeamini kabisa ni mtu na mke wake halali kwa namna walivyokumbatiana na kupigana mabusu . Fadhili alimuomba akimaliza waonena ili ampatie zile pesa alizoomba za kufungua biashara yake. Marino alifurahi sana moyoni n a kusema ama kweil babu Palwa ni kiboko, yani wananiitia pesa wenyewe, dah.
Sawa mpenzi, sawa nitakutafuta nimekumiss sana. Usijali.
Fadhili aliondoka na alipondoka tu, Marino alichukua simu yake na kuanza kumpigia mzee Palwa, ili ampe maelekezo Fulani.
Babuu.. sema babuu. Mzee Palwa alimjibu baada ya kugunduani Marino anapiga.
Samahani babuu, kwanza asante sana, nimeitiwa pesa, yani kuna mwanaume ameniitia pesa babuuu. Saa ninaweza kuwa naye na ile pete bado sijamvalisha mhusika? Marino alimuuliza mzee Palwa,
Babuu,,, ndio unaweza ila hiyo pete hakikisha huyo haishiki, umesikia? Ndio , Marino alijibu na kuachia tabasamu kwamba kumbe inawezekana akachukua pesa kwa Fadhili. Aliomba tu apate Milioni tatu afungue biashara sasa anaona anaitiwa na chumba alishalipia kwa ajili ya biashara. Dah, kismati hichi.
Marino aliondoka harka na kwenda ofisi za uhamiaji na kuomba apatiwe pasi ya kusafiria kwa muda kwani aliazimia kusafiri kuelekea Uganda kukutana na Daniel. Alipomaliza kufanya utaratibu aliambiwa arudi baada ya masaa matatu na atakuta tayari pasi yake ya muda ya kusafiria imetoka. Aliondoka na kumtafuta Fadhili ambaye alimwambia ukimaliza mizunguko yako unitafute ili nikupatie pesa ulizoomba. Fadhili alionekana mwema sana kwa Marino. Marino alimpigia simu na kumelekeza wakutane mahali ili wakae na kuongea, na kweli baada ya muda Fadhili alitokea na kumkuta Marino akiwa amekaa lakini kwa mawazo sana.
Hii mamii… mbona umetulia hivyo? Fadhili alimuuliza Marino.
Yani leo ninamawazo sana, nimejikuta tu nina mawazo juu ya maisha yangu. Marino aliamua kuchomekea sentensi hiyo ili Fadhili amhurumie. Usiogope uko na mpenzi wako sasa kila kitu kitakuwa poa. Nimekuja na lile ombi lako, Fadhili alitoa bahasha kwenye mfuko wa koti alilokuwa amevaa, bahasha iliyotuna, ambayo mtuno huo ulionyesha ni mtuno wa pesa kabisa. Marino alimtazama akatabasamu, kisha Fadhili akamwambia haya uliomba milioni 3 ila hizo hapo Milioni 4. Marino ni kama hakuamini, alisimama na kumkumbatia Fadhili kwa kumaanisha hasa, mpaka machozi yakamtoka, Asante Fadhili, asante sana, Marino alimshukuru Fadhili huku machozi yakimdondoka,,, Usilie, nyamaza, usilie, Nilikuambia nitakupa mapenzi na kukujali na kukuonyesha thamani ya mwanamke ambayo naijua, wewe ni mwanamke wa pekee sana ni mwanamke mrembo, unayejua mapenzi na unayejali wacha ni mimi nikujali, Utakula pesa zangu nyingi sana yani kwa hilo tu jiandae. Fadhili alimhakikishia Marino kumpatia matunzo na pesa na mapenzi. Marino nataka tu unielewe na uwe tayari kunielewa , Nimekuambia wewe ni mwanamke ninayekupenda sana, ambaye mapenzi yako kwangu yamekuwa mapenzi ambayo sijawahi kupata kwa mwanamke yeyote Yule, ni mwanamke mrembo sana, hivyo jua nakupenda, na nitaendelea kukupenda, nitakupa mapendo yangu na pesa zangu utazila . Kama ulikuwa na mpango wa kutafuta mpenzi nikuombe funga ukurasa wa mapenzi, na utulie nikuonyeshe mapenzi, nataka tupendane umesikia mamiii? Fadhili alimwambia Hivyo Marino, Kisha Fadhili akarudia tena,, Jua nina wivu juu yako usisahau hilo, Naomba uwe muaminifu, kwani mapenzi hugeuka kuwa kilio na kifo endapo anayekupenda hutamthamini,, umesikia mamii.
Marino baada ya kusikia sentensi hiyo,, “mapenzi hugeuka kifo” Akili yake ilienda moja kwa moja kwa Daniel. Mwanaume ambaye ameanza naye mapenzi mapya. Hivi nitaweza kweli kuwa na wanaume wawili?hivi nitaweza kweli? Lakini nitaweza,, nitaweza. Marino ghafla alihama pale kimawazo, na Fadhili alimshtukia..
Unawaza nini mamii? Marino aligutuka na kumwambia noo, yani Baba Davis leo ameniletea barua za kuanza utaratibu wa talaka ndizo naziwaza. Ilibidi Marino aongee hivyo ili kumuonyesha Fadhili anawaza jambo la maana lakini ukweli alikuwa anawaza zile pete mkononi , kwamba ni lazima Akamvalishe Daniel haraka sana nan i lazima asafiri kwenda Uganda. Ni lazima.
Usijali usiogope talaka wewe hutakuwa wa kwanza kuachana, mwanamke mrembo sana wewe, tena hiyo talaka idai haraka sana, kisha mimi nakuhakikishia kuwa na wewe milele, na nilikuambia ukitaka hata kuzaa utanizalia mpenzi wangu, si ndio eee.. Fadhili alimhakikishia Marino uhakika wa maisha na akitaka kuzaa azae. Marino alihema kwanguvu kisha akakumbuka muda wa kwenda kufuata pasi yake umefika, Alipokuwa katika kufikiri simu yake ikaita, Ni iphone,, Fadhili alimucha na kisimu cha tochi. Fadhili aliposikia mlio wa Iphone ni kama alishtuka Fulani, kisha akamtazama, Marino alitabasamu na kupokea ile simu. Alionge na ile simu kwa wasi wasi sana kwani ilikuwa nisimu ya kufuata pasi yake.. Tayari anti, uje uchukue pasi yako. Sawa nakuja hapo mnafunga saa ngapi? Tunafunga saa kumi jioni, wahi, bado kidogo tufunge, Afisa alikuwa akimuelekeza Marino kuipata pasi yake.
Sawa nitakuja hapo muda si mrefu. Marino alimaliza kuongea na Fadhili akiwa kwenye kushangaa simu lakini kushangaa pia pasi ya kusafiria.. Mh. Aliguna kindani ndani. Marino aliwaza haraka kwamba akiulizwa atasema ni kwa ajili ya kufuata mzigo kwani ndilo lengo lake la biashara na mtaji ameshampatia. Aliwaza moyoni, yani NITAUA NDEGE WAWILI KWA JIWE MOJA, Naenda Uganda kibiashara na kumfuata Daniel. Aliwaza kisha akamtazama Fadhili na kumuambia, Ninataka kufanya biashara za nguo, ninaomba unisogeze ofisi za uhamiaji nikapate pasi yangu ya kusafiria. Sawa, Fadhili alimkubalia, kisha akampatia Lifti na kumpeleka mpaka ofisi za uhamiaji na Marino akachukua ile karatasi.
Baada ya hapo Fadhili alimuaga na kumuambia kwamba ajiandae ili usiku wa siku inayofuata wawe wote, alimuachia ile bahasha yenye pesa na akaondoka. Marino alikuwa na raha ya namna yake. Alifika nyumbani ni kama alikuwa haamini, Alishachukua fremu ya biashara na hakuwa na biashara yoyote, sasa nitafungua biashara, nianza na huduma ya pesa kwa njia ya simu, nitaomba ma bank niwe wakala, nitafuata nguo Uganda, yani dah, Asante Mola Marino alishukuru nakuanza kujiona akiwini maisha. Nitajenga nyumba yangu nitachukua watoto wangu, na Daniel sitamuacha. Waoooo.. Alijirusha kitandani kwa raha akijiona ni mshindi wa maisha. Akiwa kitandani alimkukumbuka Daniel, Aliamua kumpigia simu, na kumwambia kwamba ameshfanikiwa kupata pasi ya kusafiria hivyo ataanza safari aiza siku inayofuata ama baada ya siku mbili. Daniel alifurahi sana na kumwambia ni sawa tu, yuko tayari.
Asante sana Marino, unanipenda na kunijali sana, na huku itakuwa rahisi kwani hakuna anayenifahamu huku hivyo tutakuwa huru, nikuombe mpenzi wangu nikukatie tiketi ya ndege kisha uje keshokutwa kwani kesho nitakuwa nina mambo mengi sana , alafu tutaturi wote, Sawa mpenzi? Daniel alimuomba Marino asafiri siku inayofuata.
Sawa hakuna shaka, sawa. Marino alikubaliana naye. Waoo, tiketi na mimi napanda Ndege, yani babu Palwa hatavaa tena vile vikanzu vyake na vibaraka shia, nitampiga bonge la suti matata, waooo. Babu kiboko huyu mpaka tiketi ya ndege nakatiwa, waoooo. Marino ni kama hakuamini alichokisikia, Waoooo.
Fadhili atachora chini, yani niache kwenda Uganda na ndege nibaki na Fadhili aaa thubutu atanisubiria tu kwa kweli atangoja sana, atasubiri sana. Sanaaa. Ngoja nijiandae, na hivi nina pesa waoooo, Dah, mara ya kwanza kupanda ndege,, jamani ama kweli kismati kimeniwakia, Asante Mungu jamani waooo. Marino ni kama alikuwa kipofu aliyeona mwezi kwa mara ya kwanza katika maisha yake baaada ya kusikia sententi ya kukatiwa tiketi ya ndege.
*****************************
Asbh ya siku iliyofuata , Mama Naomi anaamka ana nguvu na furaha , japo sio sana lakini ana amani . Ni afadhali, Amejikuta anaweza kukabiliana na hiyo hali na anaendelea kuomba Mungu amsaidie kuweze kusamehe. Ndilo jambo analomuomba Nalo Mungu, Eee Mungu nisaidie niweze kumsamehe huyu mwanaume, hivi anawezaje kunifanyia ubaya mkubwa namna hii? Hivi ingekuwa ni mimi ingekuwaje? Yesu nisaidie nisaidie tu, ni ngumu lakini nisaidie, Mama Naomi machozi yanamtoka peke yake, poda aliyopaka inafutika kwa machozi. Linda moyo wako kuliko vyote ulindavyo. Mama Naomi, tunaolewa na wanaume ambao sio malaika, ni wanadamu, yani kukosea nimuda wowote ule, na ndio maana Yesu alikufa kwa ajili ya watu kama hao Yani hujaolewa na Malaika, kama ulifikiri umeolewa na Malaika aisee futa kwenye akili yako, umeolew ana mwanadamu ambaye anatabia za kibinadamu ambaye maamuzi ya kuishi maisha ya nuruni ama gizani ni yake, hivyo jua hilo kwamba umeolewa na Mwanadamu na usio Malaika. Mama Naomi anakumbuka maneno ya mama Saimonii wakati akimwambia kuhusu changamoto yake. Mama Naomi anachukua simu yake na kuamua kuangalia Profile ya Marino kaweka nini. Mara Zote amekuwa akipekua sana profile ya Marino na kusoma jumbe ambazo walikuwa wakirushiana maneno. Mungu wangu, ni kama hamini anachokiona, Kaona pete ya mume wake kwenyekidole cha Marino, What? Anasema kwanguvu, ni nini hichi? Anarudia tena kuangalia na kuona pete ya mume wake kwenye vidole vya Marino. Tena picha ya Marino imepigwa kwa style ya kuweka mkono kwenye paji la uso na kuachia vidole viwili kidogo na cha pete kuonekena zaidi kwa kuvining’iniza. Mama Naomi haamini.
Anapata hasira na anajihoji, aanze na mume ama na Marino, nianzane na nani? Anaona njia rahisi ni kumuanza Marino. Anachukua simu yake na kumpigia Marino. Marino wala hapokei, anaitazama simu ya mama Naomi ikiita na kutabasamu, kwani tayari anajua kuna kitu kimemkera. Anatabasamu na kuiacha iite. Kisha inaita zaidi ya mara tano na haipokelewi. Mama Naomi anaona sasa simu haipokelewi anaamua kuandika meseji. Anaanza kuandika meseji za kushutumu Marino. Wewe ni Malaya , muizi wa waume za watu, hivi utaendelea na umalaya mpaka lini wewe mwanamke? Rudisha pete ya mume wangu Malaya mkubwa wewe, Rudisha pete ya mume wangu Malaya mkubwa wewe,utaishia kuiba wa ume za watu mpaka lini? Malaya wewe. Una nini kwanza wewe Malaya?Mama Naomi anamaliza kuandika ujumbe na kuutuma. Mudi yake imeharibika tayari.
Akiwa katika kuwaza, anasikia ujumbe unaingia kwenye simu yake.
Malaya nitakuwa mimi ama wewe, Nilicho nacho hupaswi kukiona wewe, mumeo ndio anakijua umesikia, Acha ngebe.. Usishangae mimi kuwa na pete, jiandae kushangaa mtoto.. ha ha ha.
Marino akaandika ujumbe huo na kuutuma kwa mama Naomi. Akiwa anajua kabisa kwamba mama Naomi akiusoma atakerekwa. Mama Naomi anasoma ujumbe nan i kama haamini, Anaanza kulia tena , hata kuondoka kuelekea kazini anashindwa, anaamua tu kubaki nyumbani akilia sana.
“Ni bora nife, ni bora nife, mimi siwezi, siwezi hii siwezi” Mama Naomi anasema kwanguvu mpaka mjakazi anasikia, mama yake akiwa sebuleni akilia na kusema yale maneno. Mjakazi anaogopa kwani anaifahamu hiyo familia ilivyokuwa na upendo na maelewano na mapenzi, leo ameshajua kinachoendelea anamhurumia sana mama mwenye nyumba wake, kinamuuma, Amesimama kwenye sehemu ya kuoshea vyombo jikoni huku akiangalia kwa nje nyumba ya mama Saimonii, na akili inamuambia kwamba Muandikie mama Saimoni ujumbe aje kuongea na mama Naomi. Mama Naomi analia tu sebuleni, hawezi kufanya lolote, analia tu, kaishiwa na nguvu kabisa, analia kwa uchungu sana.
Mjakazi anasogea mama yake alipo, Anashtuka kukuta chini kuna damu, tena damu nyingi tu sana, na mama yake akiendelea kulia pale chini akionekana kuishiwa na nguvu, mama mamaaa.. msichana anaachia sahani aliyokuwa ameishikilia na kukimbia kutoka nje, Anakimbia mpaka kwa mama Saimoni, anamkuta baba Mdogo tu na mama Saimoni hayuko, Anamuelezea baba mdogo , shemeji wa mama Saimoni kuhusu Damu aliyoina chini alipokuwa ameketi mama Naomi. . Sio mimba imetoka kwelli? Mama hakuwa na mimba kweli? Baba Mdogo anamuuliza Mjakazi na wanaondoka wote kuelekea kwa mama Naomi, na wanamkuta mama Naomi anaugulia maumivu pale chini.. Haraka Baba Mdogo anampigia mama Saimoni simu kumueleza kilichotokea, na mama Saimoni anampa maelezo dada kwamba wamsaidie mama kumuweka vizuri kisha baba Mdogo amkimbize hospitali, na wakati huo mama Saimonii anampigia simu mama Naomi.
Mama Naomi anapokea simu kwa shida, huku akiugulia maumivu sana, Mama Saimoni anawaambia yeye yuko mbali hivyo apelekwe hospital na watakutana huko.

Inaendelea sehemu ya 46
Post # 1451
 
View attachment 1155002

Itaendelea.....
Duh mama Naomi sijui atakuwa kajidungua kisu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom