Naipenda Jumamosi yangu - Stori bomba ya uhusiano

FB_IMG_1560786341206.jpg

SEHEMU YA THELATHINI NA MOJA
Nilikuwa njiani natembea kuelekea kupata chakula cha usiku, chochote kwa maana ya mishiki ama chips mayai, ama kitu kingine chochote ambacho kingekuwa rahisi mimi kukipata kwa ajili yam lo wangu wa usiku kwa siku hiyo.
Akili yangu kidogo ilikuwa imeanza kutulia, na picha ambazo zilikuwa kichwani kwangu nilikuwa naziona zinatimia kwa maana yakwamba ndoto zangu zimetimia.Niwe na nyumbani kwangu ambapo siwezi kusumbuliwa na mtu, niwe na biashara yangu na tayari nina gari ya kutembelea, naenda nayo wapi sijui lakini ninagari tayari ni hatua.
Fadhili ananipenda, Fadhili ananijali, Fadhili ana upendo wa dhati, kumnunulia mwanamke gari sio kitu kidogo, lakini kumpangishia nyumba na kumpa vitu vya kuanzia maisha ni upendo wa hali ya juu huuu.
Kweli Fadhili hapendi mwanamke anyanyasike kabisa.
Mungu mbariki sana Fadhili, mbariki tu .
Nilifika na kuagiza chips kuku.
Walikuwa watu wengi kwenye hiko kimgahawa ambacho nilikuwa nakula hapo.
Kulikuwa na mpira hivyo kelele zilikuwa nyingi sana, na watu walikuwa wakitembea kufuata vinywajina kurudi na kelele za hapa ana pale.
Nilimaliza kula na nilisimama ili kuelekea nje kutafuta usafiri wa piki piki ili nirudi nyumbani kwangu, nilipaita nyumbani kwangu.
Kakaaa, nilimuita kaka wa piki piki, Dereva Toyo kama tunavyowaita.,
Oya sistaaa,,, Aliitika kihuni.. wapi?
Nilimuelekeza ninapoenda, kisha nikapanda kwenye toyo haoo tukaondoka.
Dakika chache tayari tulikuwa tumefika na nilimuomba namba zake ili iwe rahisi kumtumia nikiwa namhitaji.
Nilimpatia pesa zake akaondoka na akaniachia namba zake.
Niliingia ndani nakupanda kitandani, lakini sikuwa na usingizini hata lepe.
Nilikuwa nawaza vitu vingi sana,
Ni kweli nimepata mwanaume wa kunipatia kila kitu, lakini nitakaaje bila kufanya kazi? Ni lazima niwe na kitu cha kufanya kazi, lakini Fadhili kasema atanihudumia na atatumia pesa zake nyingi sana kwa ajili yangu, na kaniomba nimzalie,
Kwa nini nisimzalie? Kwa nini nisikubali kumzaliwa wakati huu mapenzi yakiwa moto moto,, ni bora nimzalie alafu niweze kumuomba kila kituninachotaka,
Najua atanisaidia, najua.
Nyumba ilikuwa kimya na upweke sana,
Niliendelea kuwa mpweke mpaka niliposikia majogoo yakiwika mida ya saa tisa alfajiri,, ndipo na mimi kausingizi kidogo kakanipitia.
Ni siku ambayo natakiwa kwenda kazini, Sina nguo za kuvaa kufaa kwenda kazini.
Lakini kazini naenda kufanya nini? Nikafanye nini? Kazini siendi,
Nitafanya biashara, Nitafanya Biashara.
Niliamka na kunawa uso, kisha nikajiandaa ili niende kuchukua vitu vyangu nyumbani.
Nilipomaliza kujiandaa,
Nilimuandikia Msg Geof kwamba nahitaji vitu vyangu.
Hivyo wamuambie Baba Davis kwamba nahitaji vitu vyangu.
Geof hakunijibu huo ujumbe.
Nilipoona anachelewa kupokea simu, nilimpigia baba Davis ambaye nina zaidi ya siku tatu kama sio nne hatuongei.
Simu hakupokea, nikamwambia tu kwamba nahitajikuchukua nguo zangu.
Na vitu vyangu.
Hakunijibu pia ujumbe huo.
Nilipoona hajajibu, nilimuandikia tukwamba, NINAENDA NYUMBANI KUCHUKUA VITU VYANGU.
Hakunijibu pia.
Niliondoka na kuelekea nyumbani kwangu.
Nilifika na kukuta kweli kumefungwa na funguo tunapoweka zikuziona, tulizoea kuacha funguo za geti kwa jirani kama itatokea hakuna mtu nyumbani.
Niliingia kwa jirani na kumkuta na akaniambia funguo hazipo na baba Davis ana siku kama tatu hajaonekana hapo.
Nilijaribu kufungua kufuli sikufaninikwa,
Mwisho nikaamua kumfuata baba Davis ofisini kwake.
Nilifika na kweli alikuwa ofisini.
Nilimsalimia na akaitika vizuri kabisa, tena kwa kunichangamkia,
Bila shaka hakutaka kuonyesha wafanyakazi wenzake kama kuna kitu kinaendelea.
Nilimuuliza kama jumbe zangu kapata?
Ndio nimepata,, ngoja nije tuongeee..
Alisimama na tukatoka nje.
Hivi mama Davis una kichaa ama?
Aliniambiaa..
Sio swala la ukichaa,,, ninaomba funguo nikachukue vitu vyangu, ninaomba.
Alikuwa akiongea sauti ya chini sana, kama asiyetaka kitu kijulikane.
Nilipoona anaogopa na hataki kutoa funguo niliamua kuongea kwa sauti ya juu kidogo
Nipe funguo ,nipe, hukujawahi kuniona wa thamani siku zote, nasema nipe funguo,, nililongea kwa sauti ya juu kiasi amambacho watu wangeweza kusikia.
Aliangalia kushoto na kulia kisha akageuka nyuma,
Na akaniambia huwezi kuchukua vitu bila mim kuwepo
.Sawa nakusubiri,, ninachotaka na vitu vyangu,, tena usinicheleweshe.
Mfanyakazi mwenzake alikuwa akipita na alipunguza mwendo kwani ni kama alisikia malumbano yetu,, na mimi nilipoona amepunguza mwendo nilipaza sauti,
Nimesema sikutaki inatosha, nipe funguo nikachukue vilivyo vyangu basi,, nipe funguo nasema… niliongea kwanguvu.
Yule mwanaume alisimama na kugeuka na kuuliza,,,
Boss kuna usalama?? Akiwa amegeuka anauliza,, niliendelea kuongea,,
Nipe funguo nikachuke nguo zangu uendelee kuishi na huyo Malaya wako, ,, nasema nimechoka..

Shemeji,, ngoja, shemeji, ngoja,, ofisini hapa… Yule mwanaume alinivuta mkono na kunivutia kwenye kikordo .. na Baba Davis akanifuata nyuma..
Kuna nini Boss? Aaa, yani aaa,, hakuongea kitu alikuwa akisema tu hivyo huku akikuna kichwa chake, mara ashike saa mara akune kichwa,, lakini hakutoa jibu.

Samahani, kaka,, nimechosha na tabia zake, nimeamua simtaki, nimetaka ufunguo hataki. Ndio ninataka anipe nikachukue vyangu…
Wakati tunaendele kuongea, alitoke tena mwanamke mwingine akachungulia kisha akaondoka, ni kama aliona jambo na anataka kwenda kuwaeleza wenzake…
Boss naomba tusogee hapan naomba tusogeee,,,
Yule mwanaume alimshika mkono baba Davis na wakawa wanatembea kuelekea nje, nami nikawa nawafuata.
Samahani Boss, unaonaje ukaenda kuzungumza naye sehemu tulivu… hapa itakuvunjia heshima…
Shemeji,, kwa nini msiyamalize pole pole? Yule mwanaume alisema.
Kisha Baba Davis alitoka na kwenda kwenye gari yake na kutoa funguo na kunipatia.
Nilizipokea kwa hasira na kusonya,, na kuondoka.
Nilimuacha pale na Yule mwanaume.
Niliondoka moja kwa moja mpaka nyumbani.
Nilifika nyumbani, na nikiwa nyumbani nilianza kukusanya nguo zangu
Nilikusanya nguo zangu zoote, nikamaliza, na vitu vyangu vya muhimu.
Kisha akili ikaniambia kusanya na nguo za watoto.
Nilikusanya na nguo za watoto nikamaliza.
Baada ya kumaliza, niliita dereva wa taksi, na kuchukua mizigo yangu na kuondoka.
Nilifikisha mizigo yangu kwenye nyumba yangu mpya, na kurushia tu.
Baba Davis hakunitafuta tena japo funguo za getini nilikuwa nazo. Aliingiaje sijui. Na sikufuatilia.
Nilianza kuishi maisha ya kula kwenye mgahawa, na kutoka out Fadhili,
Fadhili aliniahidi atanipatia milioni 4 za kufungua biashara, na hivyo nimvumilie kidogo.Na nilipomuambia nimeacha kazi aliniambia ni sawa tu kutokana na maamuzi yangu kwani kama naona kazi hainilipi ni bora nifanye biashara.
Asubuhi nilikuwa natoka nyumbani kwangu naenda Dukani kwa Mama Karisa, tunakaa tunaongea, na alikuwa akinisaidia kutafuta sehemu ya biashara.
Kila siku tulitafuta eneo la biashara mpaka tukapata.
Nilimueleza Fadhili kwamba nimepata eneo la Biashara na aliridhia, na akaniambia nisubiri kidogo mambo yake aweke sawa kisha anipatie hizo pesa alizoniahidi.
Chumba cha biashara ambacho tulikitapa mwenye chumba alikuwa na haraka nacho sana, na hivyo ilibidi nitafute pesa kwa haraka, na Mama Karisa aliniambia atanikopesha laki tano ni lipe hicho chumba laki nne na nusu kodi ya miezi mitatu, japo mwenye nyumba alitaka miezi sita.
Lakini nikakishikilia kwa miezi mitatu kwanza
Lengo langu ilikuwa ni kufungua duka la vipodozi na urembo wa mwanamke, niweke na huduma za mpesa.
Mtaji wa milioni moja pia ungetosha kuanzia kabisa,
Niliongea na Fadhili kwamba kama hatajali anipatie hata milioni moja ili niendelee na biashara kwani nimeshalipia chumba
Aliendelea kuniomba kwamba kuna pesa anasubiri mahali ningoje azipokee ili anipe kwa mara moja.
Kwa sababu ni mwanaume ambaye amekuwa akinijali sikujali na nikawa naendelea kusubiri siku zisonge ili niweze kupata hizo pesa.
Siku ziliendelea kusonga, Nililetewa barua ya kusimamishwa kazi na kuelekezwa namna ya kupata haki ya pesa zangu, niliipokea barua yangu wala sikuwa na mashaka kabisa akili yangu ilishahama kuajiriwa na ilihamia kwenye kujiajiri.
Hivyo sikuwa na mashaka, namfahamu mama Karisa muda mrefu, duka lake limekuwa likiongezeka siku hadi siku na amekuwa mwanamke wa kuwa na pesa na kumudu maisha yake. Hivyo nilijua na mimi Mungu atanisaidia nikianza biashara zangu nitafanikiwa tu.
Thea alikuwa akiniambia nina bahati sana kupata mwanaume ambaye yuko tayari kunihudumia kiasi hicho.
Kwa vile niliridhika na maisha nilipendeza sana. Vaa yangu ilibadilika, nilikuwa mwanamke wa kujiremba na kujipenda sana, na kuvalia vizuri sana.
Na nilikuwa naridhika tu na maisha ninapoona ile gari , nyumba nzuri, na ahadi za mtaji wa biashara, na tayari ninacho chumba cha biashara.
Muda umepita, sijaona watoto, lakini najua wako sehemu salama, watoto wako kwa mama mkwe wangu.
Mama Karisa kwa sababu ndiye alikuwa anajua kuendesha gari, kuna wakati alikuwa anakuja anachukua gari tunaitumia,
Muda mwingi nilikuwa nashinda dukani kwa mama Karisa na maisha niliona ni sawa tu.
Fadhili hakuwa mwanaume wa kunibana wala kunipangia chochote, japo alikuwa akinipa pesa za hapa na pale lakini hakuwa ananiuliza ninazifanyia nini, wala hakuwa ananiuliza ninaenda wapi ama niko wapi.
Alichokuwa anataka ni akikuhitaji tu upatikane, na mimi sikuwa mtu wa ratiba nyingi, ni nyumbani kwangu, dukani kwa mama Karisa basi, nikitoka sana ni Salon.
Nilianza kuwa napenda kwenda salon kutengeneza kucha na kuosha migu, nitabia ambayo siku za nyuma sikuwa nayo, kwanza kwa sababu ya gharama, lakini sasa naweza kwa sababu nina pesa, nina muda wa kufanya hayo.

Nikiwa salon natengeneza kucha , Thea alinipigia simu na akaniambia natatutwa na baba mdogo wangu. Nilishangaa sana, kwa nini baba mdogo hajanipigia simu?
Kwa nini mama mdogo asinipigie simu na wananifuata kazini?
Thea aliniambia tu ni baba yako mdogo anakutafuta.
Aliniuliza niko sehemu gani ili baba mdogo aje, na nilimwambia niko salon.
Nilimwambia Thea anipe niongee naye.
Niliongea na baba Mdogo na akaniambia amepelekewa mashitaka na baba Davis kwamba siko nyumbani na nimeondoka na lolote likinipata yeye hahusiki.
Hivyo baba mdogo alitaka tuongee ili kama ni kikao cha makabidhiano kikae.
Nilichukia sana, na kumwambia baba mdogo nimeshaongea na baba Davis na tumeshayamaliza na ndiye aliyenipatia vitu vyangu, hivyo anajua kila kitu.
Baba mdogo alionyesha kunihitaji na tukae tuongee hata kama tumeshaongea na baba Davis ila alisema anatamani kuongea na mimi pia.
Nilimkubalia japo kishingo upande.
Na nilimuagiza mahali nilipo na Thea akamkamchukulia piki piki ambayo ilimleta mpaka sehemu niliyokuwa.
Baba, naomba nimalize kutengeneza kucha mara moja… Sawa sawa, baba aliitikia na kusogea pembeni kwenye kiduka na kukaa hapo akiwa na gazeti lake akisoma.
Nilimaliza kutengeneza kucha na kumfuata baba alipokuwa ,,,,
Tunaweza kutafuta sehemu nzuri tuongee mwanangu? Nina mazungumzo marefu..
Baba alisema..
Ndio baba, nilimuitikia na kutafuta sehemu ambayo tulikaa na tukaanza kuongea.
… Baba alionekana mpole sana, Na ambaye hakuwa na hasira wala papara kwenye maongezi yake.
Baba Davis kaniambia umepata mwanaume… baba alisema.
Sikujibu kitu nilinyamaza kwanza,,, enhe. Niliitikia.
Ndio mwanangu, je ni kweli?
Nilimtazama baba ambaye alikuwa mpole sana,,,
Si kweli baba, sio kweli.. nilikataaa.
Sawa kama sio kweli, kama sio kweli unaweza kurudi kwako?
Baba mimi sirudi kwa baba Davis, nilishaapa sirudi sirudi basi, mateso aliyonionyesha yananitosha, sirudi.

Sawa, sasa kama hurudi ni vyema mambo yakawekwa wazi kisheria kutokana na madai ya baba Davis kwamba una mwanaume, anasema anataka kukukabidhisha kwa wazazi wako ili ijulikane kwamba wewe sio mke wake tena… Baba aliongea kwa upole sana.
Sawa,, sawa baba, sawa tu…. Nimeshamchoka,, sawa. Nilijibu.
Baba alinitazama na akaniambia,, Umelogwa ama ? hizi sio akili zako kabisa mwanangu… baba alisema kwa upole sana.
… mh.. nilipata hasira nikaguna kwanza,, baba,, nilimuita,, wakati mimi napigwa na kuteswa na baba Davis mliona ni sawa kabisa, sasa hivi nimeamua maisha yang ndio mnasema nimelogwa,,, hivi wakati ule napigwa mbona hamkuonyesha hizi juhudi? Mbona hamkutaka vikao vya kisheria kutaka kujua suluhu inapatikana? Bwana eeee,, msinikere mimi… kwanza sitaki kikao na mtu, afuate maisha yake,, niliongea kwa hasira sana, mpaka wateja wa pale waliokuwa wanakula wakawa wananishangaa…..
Mwanangu , huna sababu za kulia, juhudi tulionyesha na ndio maana tuliongea naye, hembu fanya moyo wako uwe mwepesi kusamehe. Samehe maisha yaendelee, mwanangu.
Baba alinisihi.
Nilimtazama baba, alinitia huruma sana, sijui alikuwa anawaza nini, lakini nilipokumbuka ukatili wa baba Davis siku za nyuma alivyokuwa akinifanyia, tena ananijibu kabisa kwamba, .. “MIMI SINA HADHI YA KUWA MKE WAKE” Nilimwambia tu baba, wacha iwe inavyokuwa baba, inatosha.

Baba, hivi unakumbuka baba Davis alishawahi kuniambia sina Hadhi yake? Unakumbuka baba? Sasa aniache, nimegundua sina hadhi yake aniache.
Nilikuwa nalia machozi, uchungu nilipata moyoni, jinsi nilivyokuwa nampenda baba Davis kwa moyo wangu wote, lakini kanifanya mpaka nimekuwa na roho ngumu namna hiii..
Baba, niacheni , niacheni.
Hapana mama Davis usiseme hivyo mwanangu, usimpe shetani nafasi mwanangu. Shetani alikuwa anakutafuta wewe ndio maana unaona anaelekea kukupata mpaka unashindwa kumsamehe mwenzako. Ameshatubu na kusema anaomba amani , mbona hurudishi moyo wako?
Baba , baba,, sio baba Davis, siooo, kuna mahali anafundishwa, namjua sio baba, sio …
Ninamjua baba Davis, ninamjua, ni mwanaume mjeuri na ambaye hajali baba , sio yeye, sio akilizake, anafundishwa, alijua nitakuwa nakubali kunyanyasika maisha yangu yote, sitaki, nimechoka.
Nilimhakikishia baba sitaki kikao chochote.

Sawa basi wacha mimi nirudi mwanangu,
Basi napandia wapi? Baba aliuliza.
Nilitoa noti mbili za elfu kumi nikampatia baba na kumsindikiza mpaka stand ya bus. Akapanda gari nikaondoka na kurudi kwa mama Karisa dukani.
Nilimuelezea mama Karisa juu ya kikao anachokitaka baba Davis, nilimwambia kila kitu, na akaniambia kwa nini usiamue limoja?
Umeshaondoka unataka kurudi tena ili nini?
Wewe pambania biashara kwanza, usijichanganye, malizana na Fadhili upate biashara, kwanza, ukianza vikao sasa hivi na kazi huna alafu ukirudi unategemea nini? Hembu maliza limoja kwanza.
Mama Karisa alinishauri na nikaona ni ushauri mzuri,
Kweli nahitaji biashara, sasa mambo ya vikao nani tena kasema… niligonga na mama Karisa na tukacheka.
Niliondoka na mama Karisa na tukaenda sehemu kunywa pombe, nilikuwa na mawazo sana, nilikunywa pombe nyingi sana, akili yangu iliingiwa na mawazo ghafla, ni kama nilikuwa naona mambo yanaenda pole pole, na njia rahisi kwangu ya kupunguza mawazo ilikuwa ni kunywa tu pombe.
Nilikunywa pombe na nikamuomba mama Karisa anipeleke nyumbani.
Mama Karisa alinipelekea nyumbani na kuniacha hapo na kupaki gari yangu na yeye akaondoka na taksii kurudi kwake.
Nilijitahidi kufunga milango, na kuingia ndani kulala.
Nilijibwaga kitandani kama mzigo.
Usiku sana katikati ya usiku, nilisikia honi zikipigwa kwa nguvu sana getini,
Honi zilikuwa zikipigwa mfululizo, nilishtuka na kuchungulia dirishani kuona kama ni getini kwangu ama? Niliona kweli kuna gari getini linapiga honi.
Nilijaribu kuchungulia kilevi levi kutaka kuona ni nani lakini sikufanikiwa kujua ni nani.
Nilichukua simu yangu na kuangalia saa, ni saa sita na nusu, niliamua kumpigia Fadhili kwanza, nimuulize ni yeye?
Simu iliita sana akini haikupokelewa,
Wakati huo bado honi zilikuwa zinaendelea kupigwa, kiasi kwamba zinakuwa kero kwa majirani.
Niliingiwa na hofu, ni nani anawezakuja na gari? Ni nani?
Nilimpigia tena Fadhili simu na simu haikupokelewa.
Niliamua kumpigia Dogo, nilimpigia dogo akapokea, na nilimwambia kunamtu getini anapiga honi ninaogopa kufungua geti.
Aliniambia tu kama unaogopa usifungue ni usiku.
Nilikosa usingizi japo nilikuwa nimekunywa lakini nilikosa usingizi kabisa,

INANDELEA SEHEMU YA 32
Post #749
 
View attachment 1130080

ITAENDELEA
Mambo ndio yaanza
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom