Naipenda ACT, nami ni mzalendo...

Naipenda ACT, nami ni mzalendo...

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2012
Posts
1,985
Reaction score
1,286
Natangaza hadharani, nakipenda chama changu,
Siko na haya usoni, tena sitaki mvungu,
ACT iko moyoni, tambueni ndugu zangu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

ACT si chama bure, chama kina falsafa,
Si nyingine unyerere , kuhuisha yalo kufa,
Tuhariri pasi shere, azimio lilokufa
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Mlengo kati kushoto , ndio itikadi yetu,
Twaamini tu watoto, Tanzania baba yetu,
Nchi ipate mapato, ishinde adui zetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna adui ujinga, si ule wa tangu zama,
Zeruzeru kuwagonga, roho zao kuzichoma,
Huu nao ni ujinga, siseme wajua soma,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna adui maradhi, nisemalo sitanii,
Tena hakuna hifadhi, ya kuilinda jamii,
Bima na iwe faradhi, kwa kila mwanajamii,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Adui umaskini, azidi kutamalaki,
Ajira tabu nchini, mazao hayauziki,
Benki hazituthamini, kisa hatukopesheki,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Sasa nije kwa misingi, ilojenga chama chetu,
Si michache iko mingi, ni kumi misingi yetu,
Chama kimelamba kingi, madhubuti chama chetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Nianze na uzalendo , kuipenda nchi yetu,
Twauishi kivitendo, si kwa maneno katu,
Wasoweza wako kando, sasa wapiga upatu,
Ninaaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Usawa msingi wetu, tena twaupigania,
Usawa katika watu, ACT twaulilia,
Usawa kwa kila kitu, kupata na kuchangia,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Wa tatu uadilifu, katika maisha yetu,
Sio silaha dhaifu, kwa wale mafisi watu,
Wala rushwa wana hofu, na huno msingi wetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Upo pia wa uwazi, lakini si wa chumbani,
Tunautaka uwazi, wenye faida nchini,
Tuuchoke ubazazi, wa mafuta na madini,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tano uwajibikaji , kila mtu kwa kaziye,
Nchi inatuhitaji, kila mtu nafasiye,
Kila mja muhitaji, aombea nyumbaye,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna demokrasia, ile ya rasilimali ,
Umma hujipangia, kutumia zao mali,
Takwa la umma njia, unyayo ni serikali,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Saba tuna hifadhi, si nyingine ya jamii ,
ACT yaja kabidhi, kwa wote stahiki hii,
Na sheria ya kukidhi, ya kulinda haki hii,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna msingi wa utu , kuheshimu binadamu,
Panapothamini utu, maendeleo hudumu,
ACT tajali utu, binadamu kuheshimu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Uko msingi adhimu, kukusanya waafrika,
Tuwashinde madhalimu, Ulaya na Amerika,
Umoja kitu muhimu, umajimui Afrika ,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Nkruma ramani yetu, Nyerere kwetu dira,
Talijenga bara letu, tena pasina papara,
Tuumize bongo zetu, tena sifanye harara,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Kumi kujitegemea, bidii katika kazi,
Sije dhani napotea, weledi katika kazi,
Msingi wachochea, ubora wa makazi,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Sijui niweke koma, ama nitie kikomo,
Nachelea kupogoma, kuingia kwa shimo,
Nawshukuru mlo soma, leo mmepata somo,
ACT chama changu, Tanzania nchi yangu.

tukutane MwembeYanga.
04/07/15
Njano5
255784845394
0762845394 whatspp
 
Dotto C. Rangimoto

Matatizo ya kutokupata breakfast kifungua kinywa njaa mbaya sana.

swissme
 
Last edited by a moderator:
Wasaliti mna tapatapa kupita kiasi, kiherehere chote hiki cha nini?
 
Ha ha ha chama cha waha amakwel hiki chama kimevunja record Dunian ati chama cha waha so kabila zote zianzishe VYAMA
 
uzalendo wenu tutaujua vema baada ya kuyataja majina ya Uswiss kama mlivyoahidi.
 
Siasa za unyerere ili turudi kwenye siasa za kishenzi za kumuona mtu mmoja tu ndie mwenye akili kuzidi watu wote.

Kumiliki tv iwe ni kosa la jinai,ukikutwa na fedha za kigeni unaishia segerea,wamiliki wote wa mitandao ya voda,tigo,Airtel,redio zote za binafsi na tv zote za binafsi waishie kupigwa risasi hadharani.

Turudi enzi za RTD gazeti la uhuru,mzalendo,TBC1 nyongelea mbali kwa kuwa itawafumbua macho watanzania wasije wakatupindua kwa kuwa watakuwa wanaangalia mambo yetu live.

Wazee wetu wanaojitafutia maisha yao mashambani kusanya pamoja kama vifaranga vya kuku, bomoa makazi yao, choma moto makazi yao bila kuwalipa,hata fidia moja tupa kule watajijua wenyewe.

Kuwa tajiri ni marufuku,nyang'anya mali zao,fedha zao,funga maduka yao,wote tulundamane kwenye maduka ya ushirika ili mameneja wa maduka wawe wafalme wetu.

zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM,unyerere hoyeee.
 
Siasa za unyerere ili turudi kwenye siasa za kishenzi za kumuona mtu mmoja tu ndie mwenye akili kuzidi watu wote.

Kumiliki tv iwe ni kosa la jinai,ukikutwa na fedha za kigeni unaishia segerea,wamiliki wote wa mitandao ya voda,tigo,Airtel,redio zote za binafsi na tv zote za binafsi waishie kupigwa risasi hadharani.

Turudi enzi za RTD gazeti la uhuru,mzalendo,TBC1 nyongelea mbali kwa kuwa itawafumbua macho watanzania wasije wakatupindua kwa kuwa watakuwa wanaangalia mambo yetu live.

Wazee wetu wanaojitafutia maisha yao mashambani kusanya pamoja kama vifaranga vya kuku, bomoa makazi yao, choma moto makazi yao bila kuwalipa,hata fidia moja tupa kule watajijua wenyewe.

Kuwa tajiri ni marufuku,nyang'anya mali zao,fedha zao,funga maduka yao,wote tulundamane kwenye maduka ya ushiriki ili mameneja wa maduka wawe wafalme wetu.

zidumu fikra sahihi za mwenyekiti wa CCM,unyerere hoyeee.
Umeeleweka mkuu..........
 
Si vibaya kuuliza kama hujui...
 
Si vibaya kuuliza kama hujui...

Ukisha sema siasa za unyerere hakuna haja ya kuuliza kwa kuwa zinajulikana kwa watu wote walioguswa na siasa hizo na ukiona mtu yeyote ana shabikia siasa za Nyerere huyo hazijui na hajawahi kupitiwa na siasa za Nyerere.
 
Chadema kwanza .mengine baaadaee..... Hakuna uzalendo nje ya chadema ukisaliti tu we ACT.
 
Natangaza hadharani, nakipenda chama changu,
Siko na haya usoni, tena sitaki mvungu,
ACT iko moyoni, tambueni ndugu zangu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

ACT si chama bure, chama kina falsafa,
Si nyingine unyerere , kuhuisha yalo kufa,
Tuhariri pasi shere, azimio lilokufa
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Mlengo kati kushoto , ndio itikadi yetu,
Twaamini tu watoto, Tanzania baba yetu,
Nchi ipate mapato, ishinde adui zetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna adui ujinga, si ule wa tangu zama,
Zeruzeru kuwagonga, roho zao kuzichoma,
Huu nao ni ujinga, siseme wajua soma,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna adui maradhi, nisemalo sitanii,
Tena hakuna hifadhi, ya kuilinda jamii,
Bima na iwe faradhi, kwa kila mwanajamii,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Adui umaskini, azidi kutamalaki,
Ajira tabu nchini, mazao hayauziki,
Benki hazituthamini, kisa hatukopesheki,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Sasa nije kwa misingi, ilojenga chama chetu,
Si michache iko mingi, ni kumi misingi yetu,
Chama kimelamba kingi, madhubuti chama chetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Nianze na uzalendo , kuipenda nchi yetu,
Twauishi kivitendo, si kwa maneno katu,
Wasoweza wako kando, sasa wapiga upatu,
Ninaaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Usawa msingi wetu, tena twaupigania,
Usawa katika watu, ACT twaulilia,
Usawa kwa kila kitu, kupata na kuchangia,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Wa tatu uadilifu, katika maisha yetu,
Sio silaha dhaifu, kwa wale mafisi watu,
Wala rushwa wana hofu, na huno msingi wetu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Upo pia wa uwazi, lakini si wa chumbani,
Tunautaka uwazi, wenye faida nchini,
Tuuchoke ubazazi, wa mafuta na madini,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tano uwajibikaji , kila mtu kwa kaziye,
Nchi inatuhitaji, kila mtu nafasiye,
Kila mja muhitaji, aombea nyumbaye,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna demokrasia, ile ya rasilimali ,
Umma hujipangia, kutumia zao mali,
Takwa la umma njia, unyayo ni serikali,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Saba tuna hifadhi, si nyingine ya jamii ,
ACT yaja kabidhi, kwa wote stahiki hii,
Na sheria ya kukidhi, ya kulinda haki hii,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Tuna msingi wa utu , kuheshimu binadamu,
Panapothamini utu, maendeleo hudumu,
ACT tajali utu, binadamu kuheshimu,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Uko msingi adhimu, kukusanya waafrika,
Tuwashinde madhalimu, Ulaya na Amerika,
Umoja kitu muhimu, umajimui Afrika ,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Nkruma ramani yetu, Nyerere kwetu dira,
Talijenga bara letu, tena pasina papara,
Tuumize bongo zetu, tena sifanye harara,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Kumi kujitegemea, bidii katika kazi,
Sije dhani napotea, weledi katika kazi,
Msingi wachochea, ubora wa makazi,
Ninaipenda ACT, nami pia mzalendo.

Sijui niweke koma, ama nitie kikomo,
Nachelea kupogoma, kuingia kwa shimo,
Nawshukuru mlo soma, leo mmepata somo,
ACT chama changu, Tanzania nchi yangu.

tukutane MwembeYanga.
04/07/15
Njano5
255784845394
0762845394 whatspp
Mkuu pole, naona mnahamia CCM, wewe lini?
 
Back
Top Bottom