Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,229
Kufuatia hali ya Sintofahamu inayoendelea baada ya siku 9 za ziara ya mkuu wa majeshi nchini Italia(Kama ilivyotangazwa na Msemaji wa wizara ), na baada ya ziara yake nje ya nchi(Kama ilivyotangazwa na Rhoda na Aden ambao ni ndugu wa Davis Mwamunyange ambaye jina lake ni kama la Mkuu wetu wa Majeshi),na kwa kuwa mimi kama Mtanzania mwenye haki za kikatiba kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya jamhuri ya muungano ya Mwaka 1977 ambayo haijaheshimiwa hadi sasa,yaani haki ya kupewa taarifa; Sasa naandika kutangaza dhamira yangu ya kuipa serikali siku 7 ieleze Mkuu wa Majeshi yuko wapi .La sivyo ;
Mkuu wa Majeshi ajitokeze hadharani Mwenyewe.
Tunalipenda sana Jeshi Letu Chini ya Jenerali Davis Mwamunyange
Jeshi hili ni la wananchi na halijawahi kuwaangusha wananchi.Tunataka Mkuu wa Majeshi ajitokeze hadharani au serikali itoe kauli ili kuthibitisha usalama wa Mkuu wa Majeshi yetu Pendwa ya JWTZ.
Ni kwanini sasa Serikalli inakaa kimya kuhusu alipo Mkuu wa Majeshi baada ya kumaliza Ziara yake ya siku 9 tuliyotangaziwa na Wizara ya Ulinzi nchini Italia? Siku 9 ziliisha tarehe 1 Oktoba 2015.
Jambo Leo na Uhuru, Magazeti ambayo hayajawahi kushinda tuzo za uaminifu siku za karibuni katika habari Muhimu ndio yaliyoongoza kuripoti ujio wa mkuu wa majeshi bila picha.
Kama hatatoka hadharani Mkuu wetu wa Majeshi na kujiridhisha kuwa yupo salama hasa baada ya tetesi, Uzushi na maneno mengine dhidi yake yaliyopelekea mashtaka mahakamani dhidi ya mtuhumiwa fulani, pamoja na kuheshimu Uhuru wa Mahakama, Nitaongoza kampeni ya "Bring Back Our General " ikiwa Serikali haitatoa kauli au yeye binafsi Mkuu wa Majeshi kuonekana hadharani.
Niliwahi kuitaka serikali ieleze alipo Mkuu wa Majeshi HAPA
www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/953075-serikali-itueleze-sasa-alipo-mkuu-wa-majeshi-tuna-haki-kwa-mujibu-wa-ibara-ya-18-ya-katiba-ya-nchi.html
Serikali isiruhusu taifa kuwa "Taifa la Tetesi/Umbea".Limepata nafasi nyingine ya kulinda utamaduni wa Taifa letu.
Mungu Libariki Jeshi Letu JWTZ, Mungu Ibariki Tanzania,Mungu Ibariki Afrika