Naiona hatari hii kutokea siku zijazo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,695
149,921
Kama yaliyoripotiwa kuhusu kikao cha ndani kati ya waheshimiwa wa chama fulani na mwenyekiti wao ni ya kweli na iwapo hali hii itaendelea kwa siku za usoni,basi kuna uwezekano wa watu kufanya maamuzi magumu wakati wowote kabla ya mwaka 2020 au katika mwaka huo 2020.

Mpaka siri zinatoka ni wazi watu hawaridhiki hivyo kuna uwezekano siku zijazo watu wakaja kuishia uvumiliv na kuamua kufanya mazungumzo na kisha kundi moja kubwa la waheshimiwa likaamua kujiengua kutoka chama fulani na kujiunga na umoja wa vyama fulani kwa makubaliona ya kutetea majimbo yao wakiwa ndani ya umoja huo.

Vitisho na mikwara hii imeanza mapema mno na sidhani kama watu wote watavumilia ubabe huu kwa muda wote huu uliobaki hivyo kundi kubwa kubwa linaweza kuamua kujitoa kuliko kuvumilia haya tunayoyasikia maana kwakweli huu ni udhalilishaji na ni dharau mbaya kabisa.

Kitakachowaunganisha ni kutendewa vivyo sivyo na utekelezaji mbovu wa bajeti katika maeneo yao kunakotishia nafasi zao.

Kaanza vibaya bila kujali ni mapema mno kwa watu kumvumilia.
 
Scatter brain! Bs
Mimi nadhani watu mna hofu zisizo na msingi kabisa.

Vilevile naona kuna kampeni inaendelea ya kutia chumvi na kukuza mambo tu.

The sky is not falling y'all. So chill the fcuk out....
 
Tatizo sio kutokuridhika, ila huridhiki kwa kipi, hii ndiyo hoja ya msingi.

Kama watajiengua sababu ya kunyimwa pesa za vikao na warsha, wafanye hima hata sasa.
 
Vita ya kuwatoa wasaliti ndani ya chama, nihatari huwezi jua anayemsema hafai na yule anayeondoka unajiuliza hana mizizi??
 
Back
Top Bottom