Mwiba
Hakika haya uliyo yaandika hapa ni changamoto kwetu vyama vya upinzani, tume huru itakuwa ndoto kama hatutaidai, ila nakuhaidi .... my brother hilo muda si mrefu tutaanza kulidai,
Mwiba, tutashinikiza vyama vyetu hadi hilo ulilopendekeza lifanyiwe kazi.
Mwiba labda unisaidie kufahamu jambo hili, ni njia(strategies) zipi tuzitumie ili tuweze kuidai hiyo tume huru? najua CUF na Chadema wote ni waathirika wa tume ya uchaguzi,
Njia ni nyingi sana ,kwani cheche huzaa moto ikiwa nyasi ni kavu ,na wananchi tulio wengi tumekauka .shida mpaka chini ya mvungu ,tatizo na maendeleo na kucheleweshwa kunatokana na Tume za Uchaguzi zilizopita ambazo hatukuwa na imani nazo ila ndio lisilo na budi.
Sasa ndio wakati muafaka mbona KENYA waliweza ? Madai ya TUME HURU ni lazima yawe na TIME LIMIT ya kuyadai na si kungojea mpaka jua limekuchwa ,ndio utaona viongozi wa Vyama vyetu hivi huwa kama wanakurupuka kutoka usingizini ,mwisho wake wanatuletea ngonjera ,kuwa tusiwache kupiga kura ,japo TUME hawana imani nayo ,hivi tuwaeleweje wanapotusomea mistari ya aina hiyo ?
Vyama vikubaliane tu kuwa kama hakuna TUME ya UCHAGUZI Inayokubalika basi havotoshiriki uchaguzi na kuwahamasisha wananchi wasishiriki uchaguzi , ila hapa tujiulize ni vyama vingapi vipo tayari tusije tukaachana kwenye mataa ? Jengine ni kutumia mahakama ,kuipinga TUME ya UCHAGUZI iliyopo ambayo CCM wameipa jina kuwa ni ya kudumu ,hili halihitaji vyama vingi ,ni kuhusisha wanasheria waliobobea ,hapa napo ni sehemu ya kipimo kwani mambo ya
kimahakama yanachukua muda mrefu ,ndio nikasema kwa sasa ndio muda muwafaka wa kuanza kuwasha cheche, na sio
kutegemea KATIBA mpya ,ya Katiba yawachwe kama ya KATIBA .ila tuna miaka miwili tu kufikia uchaguzi na kama ni kuanza kampeni basi ianzwe na hili la kudai TUME MPYA YA UCHAGUZI mpaka kieleweke na si vinginevyo ,kama ni uchochezi sawa ,ila TUME hii ni lazima idaiwe na ipatikanike. Vinginevyo Sultan CCM anaondoka tena na nchi.