Naiona CCM ikishinda tena 2015

Naiona CCM ikishinda tena 2015

Asante kwa uchambuzi wako.
Nina jambo moja tu ambalo naliona kama mtaji wa CCM kwa raia wa Tanzania nalo ni kukosekana kwa elimu ya uraia. Kama una kundi kubwa la wananchi wanaodhani kuwa kujengwa kwa miundo mbinu ya usafiri, shule na zahanati ni asante na ni bei ya uhuru wa kuchagua kiongozi bora basi CCM itaendelea kushinda.
Kwa mtazamo wangu siasa za Africa na za nchi maskini zinajengwa zaidi na vitu vidogo vidogo kwa kuwa pia upeo wa raia wengi wa nchi hizo ni mdogo sana.
Embu fikiria miaka 50 baada ya uhuru je hiki ni kiwango cha maendeleo ambacho tunaweza kuridhika nacho?!
Binafsi nimeona pia namna ambavyo CCM imekuja na namna mpya ya kuwabana watendaji ambao pia ni wanachama wa CCM ili kuleta picha kwa jamii kuwa wanaorudisha nyuma maendeleo ni watendaji na sio CCM kama Chama, ndio maana kwa sasa ni kawaida tu kumsikia Ndugu Kinana akitoa agizo kwa mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Vyama vya upinzani bado vina kazi kubwa ya kufanya kwa kuwa inawezekana matokeo ya uchaguzi 2010 yaliitisha CCM kwa hiyo hawako tayari kufanya kosa kama hilo 2015.
 
Ni upi unafiki wao ? Naomba maelezo ili nielimike !

Mkuu Mwiba siasa zetu za upinzani hata za chama chetu tawala zinaongozwa na chuki na ubinafsi, kupenda vyeo na kujipendelea maslahi yao binafsi huku wakiacha kuangalia watanzania ambao ndio ngao yao katika kupata nafasi hizo wanazotaka. Chukulia mfano wa chama cha demokrasia na maendeleo kinavyoendesha siasa zake za kibaguzi na chuki. Ni kipi Zitto kawakosea viongozi wa chadema mpaka kufikia hatua ya kumuundia magenge ya wahuni kumchafua na hata mara nyingine kutaka kumuua? Ni kipi kinapelekea katibu mkuu na naibu wake hawana mahusiano mazuri ukizingatia wote lao moja kama sio chuki na ubinafsi? Watu wengi sana wameshakata tamaa na upinzani ukizingatia wengi wao wamejiunga na chadema sababu ya misingi yake mizuri na watu wanaosimamia misingi ipasavyo kama mh Zito. Chadema kinaendeshwa kifamilia na kindugu zaidi pamoja na kwamba katiba yake haipo kihivyo. Leo vyama vya upinzania vinaungama eti kupigania katiba ya JMT lakini kule bungeni vinashindwa kwa sababu za kijinga. Upinzani Tanzania wanawatu ila hawana viongozi. Tanzania kuna watu wameichoka ccm ila hawajui ni nani anaweza kuwasaidia ukizingatia upinzani ndio huo uliokaa kifisadi, kichuki, kibinafsi, kindugu n.k
 
Last edited by a moderator:
Nikisikia habari ya CCM kushika tena dola najisikia hovyo kabisa. Mbaya mbaya mbaya.
 
Hilo hata wao wanalifaham, labda kama watalisimamisha li Wasira hapo ndipo takuwa na mashaka.
Hakuna CCM bila Lowassa, jamaa anakubalika, mwanzo nilikuwa namchukulia poa kumbe moto.
 
ha ha ha ndugu unafahamu kuwa tuna mchakato wa kupata katiba mpya? Na kwenye mchakato wa katiba mpya ndiko kutakapo patikana tume huru ya uchaguzi pekee na hata kama hayo mengine ayatapita ila jua hili la tume huru ya uchaguzi litapita na tutakuwa na tume huru safi
Endeleeni kuishi kwa matumaini ipo siku ARV itageuka kuwa chanjo mh.
 
Nikisikia habari ya CCM kushika tena dola najisikia hovyo kabisa. Mbaya mbaya mbaya.

CCM si wajinga au wakoromaji waliolewa na madaraka ,wanajua nini kinaendelea na zaidi wanafahamu nini wafanye na ndio wameanza ,ila kwa vile wameonekana kushitukiwa na miendelezo yao ya mikutano ,kesho wameahirisha ,wanajipanga upya na kuja na mikakati mipya,

Wao kushika DOLA ni lazima kwa bei yeyote ile ,sasa ikiwa tutategemea KATIBA basi ujue wazi weshatupiga chenga
kwani usitegemee kuwa KATIBA hiyo itakuwa tayari ,fahamu kuwa KATIBA maoni yanarudi tena ,unafikiri yatarudi mara ngapi ??? Mara hii wamepinga upinzani mara ijayo itakuwa zamu yao ,nao itabidi wakubaliwe ,sijui umeiona game inavyotaka kuchezwa hapo ?

Angalizo ni kwa vyama hivi vilivyoungana na huko bungeni kuweka TIME FRAME ya KATIBA ,sio tunajadili bila ya kujiwekea ukomo wa kujadili. Otherwise tutakuwa tanacheza kwata.
 
Kwa maoni yangu kwa VYAMA vya Siasa huu ni muda muwafaka wa kuwaandaa wananchi kimaandamano na kimikutano kudai TUME MPYA ya Uchaguzi , msicheze mbali na madai hayo kwani Uchaguzi upo kwenye HORIZON na wenzenu CCM wameshaanza kupiga ngoma ndogondogo. KATIBA ni muhimu ila Tume ya Uchaguzi ni muhimu zaidi ukizingatia muda tulio nao.


Lakini hii inahitajika sasa tukielekee kwenye kura za katiba mpya, na namini kw akutumia motomoto motoooo, hii kitu lazima ipatikeni, kiukweli huku sijuhi wanangoja nini, maana znz tayari ipo.
 
Wewe acha kuna sehemu nmeeenda tz hii... mbunhe kutoa kilo kadhaaa za mchele. Wanaona ndio maendeleo
 
Unaposema amsaidie Muislamu mwenzake utakuwa unakosea ,kwani nyuma ya Kikwete ni msururu wa wakiristo ,huko siko takako,weka pembeni udini. Hivyo Lipumba alisaidia msururu huo. Ila sina ushahidi kama Lipumba alizipeleka kura kwa Kikwete,ila kama Ikulu inahitajika ni lazima iwepo ngangari au jicho kwa jicho ,si umeoa ZNZ CUFwametia mguu ndani ya IKULU, Na huku Tanganyika usidhani ziara na majilabu yatasaidia kuitoa CCM ikulu ni lazima jicho kwa jicho na wapiga kura kuhamasishwa kulinda kura zao kwa gharama yeyote iwapo hakuna mabadiliko makuu katika tume ya uchaguzi.

Mwiba
Hakika haya uliyo yaandika hapa ni changamoto kwetu vyama vya upinzani, tume huru itakuwa ndoto kama hatutaidai, ila nakuhaidi .... my brother hilo muda si mrefu tutaanza kulidai,

Mwiba, tutashinikiza vyama vyetu hadi hilo ulilopendekeza lifanyiwe kazi.

Mwiba labda unisaidie kufahamu jambo hili, ni njia(strategies) zipi tuzitumie ili tuweze kuidai hiyo tume huru? najua CUF na Chadema wote ni waathirika wa tume ya uchaguzi,
 
...mwakahuu tunao mpaka,kieleweke...
 
Umelishwa nini weye siku hizi!? Mbona umekuwa hivi!? Dah!!!! :A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:...bado nashughulikia suggestion yako.

Vyama vya upinzani vinatapa tapa tu sasa.

Kuna mambo mengine muhimu yanayotakiwa kufanyika
kabla ya kufikia uchaguzi mkuu lakini wako bize
na siasa za chuki.

Wasidanganyike na wingi wa watu kwenye majukwaa,
hata lyatonga mrema alikuwa anabebwa juu kwa juu
lakini siku ya uchaguzi akapata kura yake na ya mama
watoto wake tu.
 
Mwiba
Hakika haya uliyo yaandika hapa ni changamoto kwetu vyama vya upinzani, tume huru itakuwa ndoto kama hatutaidai, ila nakuhaidi .... my brother hilo muda si mrefu tutaanza kulidai,

Mwiba, tutashinikiza vyama vyetu hadi hilo ulilopendekeza lifanyiwe kazi.

Mwiba labda unisaidie kufahamu jambo hili, ni njia(strategies) zipi tuzitumie ili tuweze kuidai hiyo tume huru? najua CUF na Chadema wote ni waathirika wa tume ya uchaguzi,

Njia ni nyingi sana ,kwani cheche huzaa moto ikiwa nyasi ni kavu ,na wananchi tulio wengi tumekauka .shida mpaka chini ya mvungu ,tatizo na maendeleo na kucheleweshwa kunatokana na Tume za Uchaguzi zilizopita ambazo hatukuwa na imani nazo ila ndio lisilo na budi.

Sasa ndio wakati muafaka mbona KENYA waliweza ? Madai ya TUME HURU ni lazima yawe na TIME LIMIT ya kuyadai na si kungojea mpaka jua limekuchwa ,ndio utaona viongozi wa Vyama vyetu hivi huwa kama wanakurupuka kutoka usingizini ,mwisho wake wanatuletea ngonjera ,kuwa tusiwache kupiga kura ,japo TUME hawana imani nayo ,hivi tuwaeleweje wanapotusomea mistari ya aina hiyo ?

Vyama vikubaliane tu kuwa kama hakuna TUME ya UCHAGUZI Inayokubalika basi havotoshiriki uchaguzi na kuwahamasisha wananchi wasishiriki uchaguzi , ila hapa tujiulize ni vyama vingapi vipo tayari tusije tukaachana kwenye mataa ? Jengine ni kutumia mahakama ,kuipinga TUME ya UCHAGUZI iliyopo ambayo CCM wameipa jina kuwa ni ya kudumu ,hili halihitaji vyama vingi ,ni kuhusisha wanasheria waliobobea ,hapa napo ni sehemu ya kipimo kwani mambo ya
kimahakama yanachukua muda mrefu ,ndio nikasema kwa sasa ndio muda muwafaka wa kuanza kuwasha cheche, na sio
kutegemea KATIBA mpya ,ya Katiba yawachwe kama ya KATIBA .ila tuna miaka miwili tu kufikia uchaguzi na kama ni kuanza kampeni basi ianzwe na hili la kudai TUME MPYA YA UCHAGUZI mpaka kieleweke na si vinginevyo ,kama ni uchochezi sawa ,ila TUME hii ni lazima idaiwe na ipatikanike. Vinginevyo Sultan CCM anaondoka tena na nchi.
 
Chadema ni chama cha ukoo na kitafia mikononi mwa wanaukoo tukubali au tukatae ukweli utatuhukumu.
 
Mwiba
Hakika haya uliyo yaandika hapa ni changamoto kwetu vyama vya upinzani, tume huru itakuwa ndoto kama hatutaidai, ila nakuhaidi .... my brother hilo muda si mrefu tutaanza kulidai,

Mwiba, tutashinikiza vyama vyetu hadi hilo ulilopendekeza lifanyiwe kazi.

Mwiba labda unisaidie kufahamu jambo hili, ni njia(strategies) zipi tuzitumie ili tuweze kuidai hiyo tume huru? najua CUF na Chadema wote ni waathirika wa tume ya uchaguzi,
Siyo wote wanaosema bwana bwana watamuona bwana chadema acha wapige kelele kitanzi chao kipo tayari watakufa vibaya sana.
 
Chadema ni chama cha ukoo na kitafia mikononi mwa wanaukoo tukubali au tukatae ukweli utatuhukumu.

Vyama vya siasa unaweza kuviona vile utakavyo wewe kuviona ,kama utakiona cha udini ,ukabila au kilua ,stage inazopita CDM zimeshapitwa na vyama vingine hususan CUF ,unasema cha ukoo CUF kiliitwa cha ukoo wa kipemba. Sijui umeona ?
 
...mwakahuu tunao mpaka,kieleweke...

Mbona kishaeleweka ,jamaa weshajipnga washabadilisha mawaziri na sasa wameshabadilisha mapolisi yaani wameweka timu mpya ambayo itateka ushindi na hakuna kukurupuka ,vyama vya udini na ulevi havitopata mwanya ,ccm oyee !
 
kwa upuuzi huu unaoendeleana chadema wa kuminya demokrasia kwa kisingizio cha usaliti - bora mkoloni mweusi aendelee tu 2015, upinzani wa kweli bado sana Tanzania!
baadhi yetu tulikuwa na matumaini makubwa sana chadema ila zengwe dhidi ya zito limeonesha uchu wa madaraka walionao safu ya viongozi wa chama!!
I wonder watanzania tutakimbilia wapi..............
 
CCM Hakuna mbadala wake... Tunasubiri labda atatokea 2025.
 
Ccm itaendelea kushika hatamu lakin waendelee kujiuliza kwa nini wanatumia nguvu kubwa kuupata ushindi pamoja na ukongwe ktk siasa.
 
Back
Top Bottom