Bukwabi
JF-Expert Member
- Dec 30, 2013
- 3,352
- 1,154
Kila nikiangalia na kuangaza huku na kule bado CCM inatokea kuwa mshindi katika Uchaguzi Mukuu ujao ,na hana
m'badala. Vishindo vya CCM ambavyo kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa kwa kuanzia sasa ni vikubwa
na vyenye kuwashawishi wananchi kwa kasi ya ajabu , inaonekana wameanza mikakati ya kubomoa bomoa fikra
za wananchama wa vyama vingine na kujijenga kiaina ndani ya mioyo ya wapiga kura.
Ujanja ambao CCM inaondoka nao ni mkubwa na unahatarisha uhai na ushindi wa vyama vingine hata katika
ngazi za ubunge.CCM wameanza harakati za uchaguzi mkoa kwa mkoa na hufika hata vijijini ,ukiangalia katika mikutano yao hawataji wala hawagusii neno UCHAGUZI kwani ni agenda ya siri ambayo imo ndani ya mikakati ya mikutano yao
CCM ndani ya mikutano hiyo wamejikita zaidi katika kuelezea mikakati ya miundo mbinu ambayo wameimaliza na pia
kuwekeza katika ile mipango ambayo imeshatolewa fedha na ndani ya miezi michache itaanza kutekelezwa na kuhitimishwa, wananchi wataona CCM inafanya kweli. Na utekelezaji huu utazidi kila uchaguzi unapokaribia na itakamilika ili kuondoa masuali ufikapo uchaguzi mkuu.
Wakati vyama vingine vipo bize na kushughulikia mambo ya KATIBA kwa nguvu zao zote ,CCM huisikii kutoa majibu
kwa njia ya mikutano na badala yake ,hutoa mtu mmoja tu akijibu au kujibishana kwa njia za redio au TV na kuzidi
kuwakoroga wengine ambao huingia katika mtego huo wa kuwekwa bize na mambo ya KATIBA.
Nikiangalia yale madai ya kuwepo na tume huru ya UCHAGUZI mkuu itakayohusisha wadau wa vyama vyote ,vyama vyetu hivi vya upinzani huvisikii kuweka mbele madai hayo ,na angalau kusema Tume hii iwepo kabla ya uchaguzi kuanzia muda flani iwe imeshajulikana ,wanasahau kuwa tume iliyokuwepo ni ile ile iliyotumika kuiba na kubadilisha matokeo ,hivi ikiwa madai haya hayajakuwepo leo na kuanza kutajwa sasa ,yatadaiwa LINI ? Bado mwaka kufikia uchaguzi au baada ya kutangazwa tarehe za uchaguzi ? jawabu kutoka kwa watawala watasema muda hautoshi
na hapo ndio mdomo utakuwa umefungwa ,CCM hao wanaanza kuona raha.
Nadhani vyama hivi vilivyojiunga kuhusiana na mambo ya KATIBA wangeangalia na hili la TUME YA UCHAGUZI kwani ndio mhimili na mategemo ya ushindi ,hata yule mpiga kura aliekatishwa tamaa na tume za uchaguzi zilizopita atapata
ari mpya na matumaini mepya pale atakaposikia kuwa TUME MPYA YA UCHAGUZI imepatikana na imeshirikisha wadau wote wa vyama vya siasa na hata kutoka kwenye asasi zingine za vyombo vya sheria.
Kwa maoni yangu kwa VYAMA vya Siasa huu ni muda muwafaka wa kuwaandaa wananchi kimaandamano na kimikutano kudai TUME MPYA ya Uchaguzi , msicheze mbali na madai hayo kwani Uchaguzi upo kwenye HORIZON na wenzenu CCM wameshaanza kupiga ngoma ndogondogo. KATIBA ni muhimu ila Tume ya Uchaguzi ni muhimu zaidi ukizingatia muda tulio nao.
kushinda kwao ni kugumu kwa kuwa safu yote ya viongozi ndani ya chama chao hakuna mgombea makini na anayekubalika kwa wananchi wote. vilevile mikakati ya kuivurugaCDM imegundulika mapema, hivyo CDM wana nafasi ya kujipanga na kuchukua nchi 2015.