Naiona CCM ikishinda tena 2015

Naiona CCM ikishinda tena 2015

Mwiba

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
7,607
Reaction score
1,760
Kila nikiangalia na kuangaza huku na kule bado CCM inatokea kuwa mshindi katika Uchaguzi Mukuu ujao ,na hana
m'badala. Vishindo vya CCM ambavyo kama wewe ni mfuatiliaji wa mambo ya kisiasa kwa kuanzia sasa ni vikubwa
na vyenye kuwashawishi wananchi kwa kasi ya ajabu , inaonekana wameanza mikakati ya kubomoa bomoa fikra
za wananchama wa vyama vingine na kujijenga kiaina ndani ya mioyo ya wapiga kura.

Ujanja ambao CCM inaondoka nao ni mkubwa na unahatarisha uhai na ushindi wa vyama vingine hata katika
ngazi za ubunge.CCM wameanza harakati za uchaguzi mkoa kwa mkoa na hufika hata vijijini ,ukiangalia katika mikutano yao hawataji wala hawagusii neno UCHAGUZI kwani ni agenda ya siri ambayo imo ndani ya mikakati ya mikutano yao

CCM ndani ya mikutano hiyo wamejikita zaidi katika kuelezea mikakati ya miundo mbinu ambayo wameimaliza na pia
kuwekeza katika ile mipango ambayo imeshatolewa fedha na ndani ya miezi michache itaanza kutekelezwa na kuhitimishwa, wananchi wataona CCM inafanya kweli. Na utekelezaji huu utazidi kila uchaguzi unapokaribia na itakamilika ili kuondoa masuali ufikapo uchaguzi mkuu.

Wakati vyama vingine vipo bize na kushughulikia mambo ya KATIBA kwa nguvu zao zote ,CCM huisikii kutoa majibu
kwa njia ya mikutano na badala yake ,hutoa mtu mmoja tu akijibu au kujibishana kwa njia za redio au TV na kuzidi
kuwakoroga wengine ambao huingia katika mtego huo wa kuwekwa bize na mambo ya KATIBA.

Nikiangalia yale madai ya kuwepo na tume huru ya UCHAGUZI mkuu itakayohusisha wadau wa vyama vyote ,vyama vyetu hivi vya upinzani huvisikii kuweka mbele madai hayo ,na angalau kusema Tume hii iwepo kabla ya uchaguzi kuanzia muda flani iwe imeshajulikana ,wanasahau kuwa tume iliyokuwepo ni ile ile iliyotumika kuiba na kubadilisha matokeo ,hivi ikiwa madai haya hayajakuwepo leo na kuanza kutajwa sasa ,yatadaiwa LINI ? Bado mwaka kufikia uchaguzi au baada ya kutangazwa tarehe za uchaguzi ? jawabu kutoka kwa watawala watasema muda hautoshi
na hapo ndio mdomo utakuwa umefungwa ,CCM hao wanaanza kuona raha.

Nadhani vyama hivi vilivyojiunga kuhusiana na mambo ya KATIBA wangeangalia na hili la TUME YA UCHAGUZI kwani ndio mhimili na mategemo ya ushindi ,hata yule mpiga kura aliekatishwa tamaa na tume za uchaguzi zilizopita atapata
ari mpya na matumaini mepya pale atakaposikia kuwa TUME MPYA YA UCHAGUZI imepatikana na imeshirikisha wadau wote wa vyama vya siasa na hata kutoka kwenye asasi zingine za vyombo vya sheria.

Kwa maoni yangu kwa VYAMA vya Siasa huu ni muda muwafaka wa kuwaandaa wananchi kimaandamano na kimikutano kudai TUME MPYA ya Uchaguzi , msicheze mbali na madai hayo kwani Uchaguzi upo kwenye HORIZON na wenzenu CCM wameshaanza kupiga ngoma ndogondogo. KATIBA ni muhimu ila Tume ya Uchaguzi ni muhimu zaidi ukizingatia muda tulio nao.
 
CDM wapo ICU wanapumulia machine sasa, watasambaratishwa kama ilivyokuwa NCCR mageuzi kipindi kile mda si mrefu, ni jambo la kusubiri na kuona ahahha (ni utani lakini una ukweli ndani yake)
 
Magamba hawawez kushinda bila kuiba kura. Nakubaliana na wewe kama tume hii ya uchaguzi ikiendelea kuwepo tutegemee vioja.
 
ha ha ha ndugu unafahamu kuwa tuna mchakato wa kupata katiba mpya? Na kwenye mchakato wa katiba mpya ndiko kutakapo patikana tume huru ya uchaguzi pekee na hata kama hayo mengine ayatapita ila jua hili la tume huru ya uchaguzi litapita na tutakuwa na tume huru safi
 
magamba mnajipa tu moyo bila kuiba kura hamuwezi shinda hata mtaa,chadema yatosha. teh! teh! teh! teh!
 
Ndg Mwiba, Labda kama kuna mbinu nyingine zaidi za Kuiba kura ndo utaweza kutabiri hivyo; Inajulikana kwa kuforge matokea, CCM walipata kushinda, lakini kama mbinu ni hizo hizo za Zamani basi ungesema Unaiona nchi ikielekea Machafuko kwani, mbinu zao tayari zinajulikana na walioshindwa safari hile hawatakubali kirahisi; Kama zipo zingine mpya za kikora basi unayosababu ya kuona ushindi huo ndani ya CCM. Yawezekana umeona juhudi zao na tapatapa yao ktk kuuteka mchakato wa kupata katika huru Zinaenda vizuri. Lakini Ukweli usiofichika CCM bila mbinu chafu hakika haiwezi kutoka kwa CHADEMA. Tusubirie tuone mchakato wa katiba, kama itapatikana katiba tunayohiitaji ( Wananchi) basi CCM kwishenea..Lakini kama itapatikana Katiba wanayoitaka CCM basi Utabiri wako utakuwa wa kweli maana watafanya ukora wa aina yoyote wanaoutaka. Tatizo linalowaumiza Vichwa CCM ni Mchakato wa katiba na Niseme tu Wanajilaumu sana kwa Mzee Warioba kupewa Kuongoza Mchakato.
 
Vyama vya upinzani vinatapa tapa tu sasa.

Kuna mambo mengine muhimu yanayotakiwa kufanyika
kabla ya kufikia uchaguzi mkuu lakini wako bize
na siasa za chuki.

Wasidanganyike na wingi wa watu kwenye majukwaa,
hata lyatonga mrema alikuwa anabebwa juu kwa juu
lakini siku ya uchaguzi akapata kura yake na ya mama
watoto wake tu.
 
CCM haijawahi kushinda, wakati wote wanaiba kura. Muulize Prof. Lipumba aliyekubali kumpatia kura kikwete ili amasaidie mwislamu mwenzake. Kungekua na uchaguzi huru na haki tanzania, CCM ingekua ya mwisho. Wakati kina mwigulu wanapiga domo kwenye mikutano, usalama wa Taifa wanatafuta namna ya kucheza na kura. Inawezekana hata wasimamizi wa kura wengi ni trained usalama wa taifa. Demokrasia tanzania ni kiini macho tuu. kwani ile software ya tume ya uchaguzi ametengeneza nani? Ungejua!
 
ha ha ha ndugu unafahamu kuwa tuna mchakato wa kupata katiba mpya? Na kwenye mchakato wa katiba mpya ndiko kutakapo patikana tume huru ya uchaguzi pekee na hata kama hayo mengine ayatapita ila jua hili la tume huru ya uchaguzi litapita na tutakuwa na tume huru safi

Sasa huo ndio mtego ambao upo kazini ,unajua ngarambengarambe za Katiba mpya ,umeziona au unazisikia ? Uwepo wa Katiba mpya ndani ya miaka miwili au tuseme kabla ya Uchaguzi Mkuu ni wa bahati nasibu na mchezeshaji wa bahati nasibu hiyo ni CCM kupitia serikali yake ,Unalijua hilo ? Usiweke kabiisa matumaini ndani ya KATIBA mpya ,Ndio nikasema Tume Huru ni muhimu kuliko hiyo KATIBA Mpya kwa maana Katiba mpya imekaa kimtegomtego ,ingawa Kikwete alisikika akisema mategemeo yake Katiba mpya itakuwa tayari kabla ya Uchaguzi mkuu ujao. Niliposikia hivyo tu moyo ulienda mbio kutafuta jawabu ukarudi na kusema kuwa hilo ni dongo au changa la macho linatupiwa vyama vya siasa !

Sasa kama vyama vitaweka matumaini katika KATIBA mpya ndio ujue KATIBA mpya itapigwa danadana na ndio kama unavyoona sasa kuna malumbano au tuseme mchezo mchafu unaendelea,na Lini KATIBA itakuwa tayari hakuna anaejua kwani haikuwekewa TIME LIMIT ni kuburuzana tu ,si ajabu ukasikia Tume itaarudia kukusanya maoni ya KATIBA.
 
Yap! Mwiba una wazo lenye point ila hata hayo yote yako na tunayaona na hakika mikakati yake yote inaendelea......................... Tumaini Makene & Mohamedi Mtoi hebu zungukieni kipande hii please!
 
Last edited by a moderator:
sijawahi kuona mtanzania anayeipenda ccm toka moyoni. Inawaje nina marafiki, ndugu zangu, na watu wengine ninawajua wavaa green na wana kadi ya ccm, yote geresha tuu, ni wachumia tumbo, wapo tuu kwa maslahi binafsi, either vyeo au biashara zao ziendelee, lakini ikimvuta pembeni anakuambia kabsa, ccm hamna kitu. CCM is an evil network
 
magamba mnajipa tu moyo
bila kuiba kura hamuwezi shinda hata mtaa,chadema yatosha. teh! teh!
teh! teh!

mkuu, kwa ccm ya sasa na upinzani wa sasa, ccm haihitaji na wala haijawahi kuiba kura ili kushinda. kwa maana ccm sasa inakimbiza ile mbaya. kila kitu kinaenda sawa kabisa. wapinzani walie tu
 
Tanzania bila CCM inawezekana!
Tanzania bila CHADEMA inawezekana!
Nimechoka na tambo za vyama hivi.
 
CCM haijawahi kushinda, wakati wote wanaiba kura. Muulize Prof. Lipumba aliyekubali kumpatia kura kikwete ili amasaidie mwislamu mwenzake. Kungekua na uchaguzi huru na haki tanzania, CCM ingekua ya mwisho. Wakati kina mwigulu wanapiga domo kwenye mikutano, usalama wa Taifa wanatafuta namna ya kucheza na kura. Inawezekana hata wasimamizi wa kura wengi ni trained usalama wa taifa. Demokrasia tanzania ni kiini macho tuu. kwani ile software ya tume ya uchaguzi ametengeneza nani? Ungejua!

Unaposema amsaidie Muislamu mwenzake utakuwa unakosea ,kwani nyuma ya Kikwete ni msururu wa wakiristo ,huko siko takako,weka pembeni udini. Hivyo Lipumba alisaidia msururu huo. Ila sina ushahidi kama Lipumba alizipeleka kura kwa Kikwete,ila kama Ikulu inahitajika ni lazima iwepo ngangari au jicho kwa jicho ,si umeoa ZNZ CUFwametia mguu ndani ya IKULU, Na huku Tanganyika usidhani ziara na majilabu yatasaidia kuitoa CCM ikulu ni lazima jicho kwa jicho na wapiga kura kuhamasishwa kulinda kura zao kwa gharama yeyote iwapo hakuna mabadiliko makuu katika tume ya uchaguzi.
 
CCM haijawahi
kushinda, wakati wote wanaiba kura. Muulize Prof. Lipumba aliyekubali
kumpatia kura kikwete ili amasaidie mwislamu mwenzake. Kungekua na
uchaguzi huru na haki tanzania, CCM ingekua ya mwisho. Wakati kina
mwigulu wanapiga domo kwenye mikutano, usalama wa Taifa wanatafuta namna
ya kucheza na kura. Inawezekana hata wasimamizi wa kura wengi ni
trained usalama wa taifa. Demokrasia tanzania ni kiini macho tuu. kwani
ile software ya tume ya uchaguzi ametengeneza nani? Ungejua!

hayo ni maneno ya walioshindwa. na mtahangaika sana mwaka 2015. wananchi wamewakataa na hawataki tena vyama laghai
 
Kama ndo akina BULEMO waliowengi ndani ya Ccm hapo hakuna jipya. mtoa hoja kajipange na mabadiliko yaanze kwako tena toka moyon
 
Kuiondoa ccm madarakani tunaitaji chama kama democratic chini ya raisi mpenda taifa lake kama Obama na sio hawa wanasiasa wanafiki wa upinzani Tanzania.
 
Kuiondoa ccm madarakani tunaitaji chama kama democratic chini ya raisi mpenda taifa lake kama Obama na sio hawa wanasiasa wanafiki wa upinzani Tanzania.

Ni upi unafiki wao ? Naomba maelezo ili nielimike !
 
Tanzania bila CCM inawezekana!
Tanzania bila CHADEMA inawezekana!
Nimechoka na tambo za vyama hivi.

sasa solution ni kuanzisha cha kwako.....kikiwa na sera hai tunakuunga mkono.
 
Tanzania is ruled by a network of evil CCM that is why it is poorest in the world. Ridhiwani leo hii ni bilionea. kamaliza shule juzi. Anafanya kazi gani?. Killing CCM=Killing Poverty in Tanzania. Utajiri wa Tanzania umeshikiliwa na kundi dogo ovu la ccm, kwa njia ya ufisadi. Hakuna mtu yeyote chini ya jua naye mjua na mwogopa Mungu anaweza kuwa ccm
 
Back
Top Bottom