huko Marekani ulishaona watu wamekaa foleni kusubiri kununua sabuni mbuni, mafuata ya taa, dawa ya mbu, mkate wa Siha, n.k?
Ni ya miaka ya 70 mwishoni wakati wa vita na baada ya vita, hujaelewa nimeandika nini?
Vita ilikuwa ni mwaka 78 baada ya hapo Nyerere akatangaza miezi 18 ya kufunga mikanda. Wazungu wakaendelea kumkwamisha kiuchumi kama wanavyomfanyia Mugabe.
Hata kama kulikuwa na umuhimu wa kubadilisha siasa hivi hakukuwa na sababu ya kuvunja misingi ya maadili iliyokuwepo. Ubinasishaji wa mali za uma, wizi na rushwa, udini, ukabila na kuuwa viwanda.
Kwa hiyo umeelewa enheee? Tulianza kupiga foleni mwaka 1978 mpaka 80.
Enzi hizo nilikamatwa na polisi na kunishikiria kwa masaa kadhaa kisa nimenunua vitu vichache kama sabuni za lifeboy na colgate pale Tunduma mpakani na Zambia kwa matumizi yangu ya shule. Hivyo maisha hayakuwa mazuri kivile hasa kwenye kile kipindi cha miezi 18 ya kufunga mikanda baada ya vita na nduli Amini.
Mkuu. Nilishaweka uzi hapa unaoitwa"cable za kibalozi". Umetokea wikileaks na unazungumzia misaada Nyerere anaomba Marekani. Waziri wake Malecela ndio aliyekuwa mpiga debe wake wa kuomba misaada. Hiyo ilikuwa mwaka 1974-76.Kwa hiyo umeelewa enheee? Tulianza kupiga foleni mwaka 1978 mpaka 80.