Nilikuwa mdogo sana lakini naikumbuka kama jana!
Viwanda vya nguo kochokocho Mwatex, Urafiki, nk. Bora, chuma, mbolea, SIDO nk.
Shule ilikuwa na maana. Ukipasi la saba wewe umetimia hakuna kuhongahonga. Ukiwa kilimani (chuo kikuu) unaranda. Unangojea pijo kupanda.
Hakukuwa na TV lakini RTD ilikuwa burudani tosha kina mzee Jongo, Kipara, Mangushi, Pwagu na Pwaguzi. Usisahau wale watangazajj wa mpira kina Jongo hasa mbili kasorobo na ule mwimbo wa kipindi cha michezo.
Taarifa ya habari na ngoma 10 za mzee Morisi ikifuatiwa na mazungumzo baada ya habari. Habari za siku hizi wala hazinichengui.
Simba na Yanga ilikuwa ngoma nzito. Kibadenj na Sunday Manara. Miji ilizizima. Na hakukuwa na huu ujinga eti mchezaji kachukua hela za Simba na Yanga. Kulikuwa na kina Chogo chemba na Kapela, Yanga Yanga kweli Simba Simba kweli.
Reli ya kati hata kama usafiri ulikuwa mgumu lakini ulikuwa ni rahisi na wa uhakika hasa kwa wanafunzi.
Sikukuu Idi na Krismas utajua tu kuwa leo mjini watu wana furaha. Kila mtoto na nguo mpya. Kidongo chekundu kulinoga.
Kwa wala rushwa na wahujumu Nyerere aliwabamba na pesa za moto na wengi waliishia jela. Kwa wafanyakazi na biashara halali maisha waliyamudu vizuri.
Zamani magorofani Ilala pale kila baba alikuwa na gari. Kulikuwa na datsun, volswagen kobe na kombi, ford cortina na escort. Kulikuwa na land cruiser, landrover na range rover, morris na renault. Mikebe ya benzi za zamani. Pijo ndio usiseme. Teksi zote ni 404. Washua walikuwa na 204, 304, 404 na 504 kwa mabishoo wa mji. Halafu 404 na datsun zilikuwa na pick up zake.
Lile gari la Nyerere sijui lilikuwa Rolls Royce lile. Na pale ndani ya Makumbusho (Museum) kulikuwa na Rolls Royce sijui wajanja washaliuza.
Nani anakumbuka yale maziwa ya pakti ya pembe tatu. Kama sikosei yaliitwa KCC.
Kwa wasio na magari. UDA ilinguruma kila dakika tano. Hii nchi ilikuwa sambamba na Ulaya kwenye miaka ya sabini. Mitaa ilikuwa misafi na nyumba za mpangilio. Tizama nyumba za kota Ilala au za CDA Dodoma.
Namlaani sana aliyeuza lile gorofa la Ilala na kulifanya hoteli ya binafsi. Wengine tulikulia pale. Si afadhali wangehamisha ile shule ya Boma pale gorofani wakachukua eneo la Boma kufanya hiyo hoteli yao. Ubinafsi kitu kibaya sana.
LG Life is Good was then!
Sijui tulipotea stepu wapi!