Naidai Serikali milioni 65 tangu 2018

Serikali ikikopa huduma zako. Uwe mpole, utafilisika na makabrasha, kulikuwa na mambo ya pembejeo na mashamba darasa, watu walikopwa huko Magu akaingia madarakani, akajidai kuhakiki madeni. Hawajalipwa, wamefilisika, wamepata stroke, visukari!

Sikopeshi serikali NEVER labda niwe mwenyewe waziri kwenye hiyo Wizara yenye tenda!
 
mzee serikali mali yake haikamatwi sikuiz kisa deni...

huto kamata gari wa chaki au panadol, sheria ipo wazi...

mkurugenzi ata kubali kulipa kwa utaratibu basi...

una shinda ata msaada wa mwanasheria hukupata?
 
pole ndg,jamaa na rafiki.usikate tamaa mana utampa adui nafasi zaidi.endelea kupambana utapata.
 
Ikishinda Kesi Mahakamani ya kuidai Serikali basi hesabu Umedhulumiwa...Mzee wangu ameidai Serikali hadi umauti umemkuta.
 
Umeandika kweli tupu.
 
Serikali inadaiwa Malimbikizo ya mishahara ya Watumishi tangu 2017 na 2018 haijawalipa wahusika halafu kuna wa 2020 na 2021 wamelipwa.

Hii serikali ipo makini kweli? Au kuna rushwa hapo.


Serikali ilisimamie hili haki itendeke.
 
Tenda za serikali sio za kukimbilia hasa kwa hii serikali dhalim ya CCM. Mzee wangu alikua anaidai serikali 460million toka 2017 holla, mzee akingia kwenye madeni sana sababu yeye ndo alikua MD kwenye hii kampuni.

April mzee ndo amelipwa nusu 230m baada ya kiongozi fulani kula teuzi ambaye ni rafiki sana na mzee ndo aliyemsaidia mpaka malipo yameanza fanyika hio ilobaki wameahidi december wata deposit. Mzee hana ham tena na serikali baada ya kumlipa hio nusu wakaja tena waingie mkataba mwingine mzee akaiuza hio tenda kwa kampuni nyingine kwa 3%.

Watu wengi wanaidai serikali ila malipo ndo shida sasa sijui hizo peswa zinaliwa au laaah. Haiwezekan unampa mtu tenda anatumia pesa zake anakamilisha kazi yenu afu malipo tunanza sumbuana. Serikali badilikeni.
 
Lakini kumbuka taasisi na mamlaka za serikali huwa hazipelekwi CMA!
 
Uli supply vitu kwa system ya quatriple above reality prices nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…