Naibu Waziri wa Madini aagiza kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Naibu Waziri wa Madini Stanslaus Nyongo ameagiza kukamatwa kwa Wamiliki wa mgodi wa Nyakavangala(Thomas Masuka and Partners) kufuatia kutofautiana kuhusu taarifa waliyoiwasilisha kwa Naibu Waziri kuhusu namna mgodi huo unavyoendeshwa ikiwemo ulipaji wa kodi na mrabaha.

Alisema pamoja na kujionea shughuli za uchimbaji katika migodi ya dhahabu ya Ulata na Nyakavangala, amebaini ukwepaji mkubwa wa kodi pamoja na mrabaha wa serikali.

“Hatutaki ugomvi hapa kwenye migodi. Tunataka mgodi ufanye kazi. Dhahabu ziuzwe mahali panapoonekana. Hapa naona hesabu za viroba tu. Mnunuzi wa dhahabu hapa ni nani”, alihoji Naibu Waziri.

Imeonekana kuwa kuwa mgodi huo unadaiwa zaidi ya Tsh. Milioni 128 za mrabaha ambazo imedaiwa kuwa, wapo baadhi ya wamiliki ambao wamekuwa wakikusanya fedha hizo lakini zimekuwa hazilipwi kwa serikali.
IMG_20190116_153311.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua kuna vitu vingine vinatia uchungu sana..

Hiyo method wanayotumia hao wachimbaji ni 98% risk, Serikali imeshindwa kuwapa elimu na kuwawezesha ili wawe na namna bora ya uchimbaji ambayo sio hatarishi lakini pia ingewasaidia kukusanya dhahabu nyingi na serikali kupata stahiki kubwa pia.

Tutoe elimu kwa watu wetu, tuwawezesha, tuhakikishe watendaji wetu wako bega kwa bega na wahusika ili wawe na namna bora ya uchimbaji ili mwisho wa siku production kubwa ifanyike, watu wengi wapate ajira, serikali ipate mapato makubwa, watu nao watengeneze vipato vikubwa na waweze kukua kibiashara kiasi cha na migodi hata nje ya Tanzania.. hii ndio maana sahihi ya kumkamua ng'ombe uliyemrisha majani ya kutosha.
 
Back
Top Bottom