PreGE2025 Naibu Waziri wa habari (Mwana FA), avitaka vyombo vya habari kuripoti bila kuhamasisha kususia uchaguzi

PreGE2025 Naibu Waziri wa habari (Mwana FA), avitaka vyombo vya habari kuripoti bila kuhamasisha kususia uchaguzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Jukwaa la Wahariri Tanzania, March 04, 2025, Ruvuma. Naibu waziri wa Habari, sanaa na Michezo na utamaduni Hamis Mwinjuma (Mwana FA) amevitaka vyombo vya habari kuripoti kwa usawa kwa vyama vyote kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Aidha amevitaka vyombo vya habari kuacha kuripoti taarifa zinazohamasisha kususia uchaguzi, kwa kuwa wananchi wamemuelewa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Turipoti bila kuhamasisha kususia uchaguzi ama fujo kwenye uchaguzi tusiyaweke rehani maisha ya Watanzania, Watanzia wamemuelewa Rais Samia" - Naibu Waziri wa Habari sanaa, michezo na utamaduni

 
Naibu Waziri au Waziri wa Habari? Mods rekibisheni hicho kichwa
 
Kwani CDM walisema kama hakuna Reforms watasusia uchaguzi au hautafanyika?
Ukisikiliza tone yake na anavyokosa utulivu + confidence unaweza kuona kabisa tatizo lipo wapi
Hivi kwa nini CCM wanapenda sana ganda la ndizi?...ina maana hawawezi kuwa na wagombea compitent wa kupambana na kushinda katika mazingira fair?...
Dezo hudumaza sana!
 
Back
Top Bottom