Chief wa kijijini,
Executive orders kama hizi ndizo moja ya sababu zinanifanya binafsi kupendelea kubadilishwa kwa katiba. Kuunda kwa wizara mpya au cheo kipya isiwe kwenye dola ya Rais pekee, inatakiwa ichanganuliwe kisha ipitishwe na Bunge (lenye spika wa heshima na sio Sitta). Kutokuwa na utaratibu huu ndiko kumesababisha kutokuwa na consistancies za size ya cabinet na matokeo yake mambo mengine huzorota (mf. wizara ya michezo na utamaduni...mara iunganishwe na elimu, mara habari, mara iwe independent). Pia nachelea tukimpata Raisi fyatu, atatumia executive orders kuleta wapambe nuksi wake kuwa manaibu waziri mkuu, naibu waziri mkuu mwandamizi, etc na mwishowe taifa litaingia hasara kwa kuwapa marupurupu ya uwaziri mkuu pale isipokuwa na ulazima.
Tungojee tukiamka tuone kama Muungwana ameshabihiana na Pinda katika kushrink hiyo cabinet!