Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,380
- 39,333
Mrema alikuwa ni Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu. Ingawa cheo hicho hakipo Kikatiba lakini Rais anaweza kukiweka kwani ana mamlaka ya kuunda Ofisi kwa Agizo la Kirais (Executive Order).
Kwa vile Waziri Mkuu aliyepita inaonekana alikuwa na matatizo mengi na kuingilia hata mambo madogo madogo, kuna uwezekano wa Rais kuunda cheo hiki tena ili kumpunguzia Waziri Mkuu majukumu kadhaa. Hata hivyo sidhani kama ana uwezo wa kuunda cheo pekee cha "Naibu Waziri Mkuu" bali anaweza kuunganisha nafasi hiyo na cheo cha Waziri Mwingine.
Hivyo sitashangaa akaunganisha (assuming anakiunda) ofisi hiyo na Waziri wa Mambo ya Nje au Waziri mwingine yoyote yule.