Naibu Waziri Khamis Chillo - Wanachama wa SADC ni Vyema kuwa na Sauti ya Pamoja

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,900
944

NAIBU WAZIRI KHAMIS CHILLO AHIMIZA WANACHAMA WA SADC KUWA NA SAUTI YA PAMOJA

Tanzania imezihimiza nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) kuendelea kushirikiana katika utekelezaji wa Mkataba wa Biashara ya Kimataifa wa Wanyama na Mimea iliyo hatarini kutoweka (CITES) ili kulinda na kuhifadhi wanyamapori na mimea hiyo.

Kauli hiyo imetolewa Juni 22, 2023 na Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Khamis Hamza Chillo (Mb) katika mkutano wa Mawaziri wa SADC wanaohusika na Mazingira, Maliasili na Utalii uliofanyika kwa njia ya mtandao jijini Dodoma.

“Wanachama wa SADC ni vyema kuwa na sauti ya pamoja katika masuala ambayo kama ukanda wa Kusini mwa Afrika tunaona ni muhimu katika kuendeleza uhifadhi na maendeleo ya watu wake” Mhe. Chillo amesisitiza.

Aidha, Mhe. Chillo amesema Tanzania imeridhia Itifaki ya Misitu inayosaidia usimamizi wa misitu katika nchi za SADC na kuzishauri nchi ambazo hazijaridhia itifaki hiyo kukamilisha mchakato ili kuweza kuwa na uoanishaji wa nyenzo za usimamizi wa misitu na rasilimali zake.

Katika hatua nyingine, Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia Mazingira, Maliasili na Utalii wamepokea taarifa ya kuundwa kwa vikundi kazi vya utalii vitakavyokuwa na jukumu la kusimamia programu ya Utalii ya SADC ya mwaka 2020-2030.

Mkutano huo pia umejadili kuhusu makubaliano ya kuwepo kwa Mkakati mpya wa kukabiliana na ujangili (SADC LEAP 2022 – 2032) wenye lengo la kupunguza vitendo vya ujangili wa wanyamapori na uhifadhi kwenye nchi za SADC.

Pia, umejadili azimio la kuwepo kwa Itifaki ya SADC kuhusu uhifadhi wa wanyamapori na himasheria ; Mpango Mkakati wa Uchumi wa Wanyamapori; utekelezaji wa Programu ya utalii ya SADC 2020 – 2030 na masuala mengine ya Mazingira, Maliasili na Utalii.

Nchi nyingine zilizoshiriki Mkutano huo ni Angola, Botswana, Comoros, Democratic Republic of Congo, Eswatini, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Mozambique, Namibia, Seychelles, South Africa, Zambia and Zimbabwe.
 

Attachments

  • FzPVND-WAAEf55dQW.jpg
    FzPVND-WAAEf55dQW.jpg
    62.3 KB · Views: 2
  • FzPVND7XgAA5c6iERT.jpg
    FzPVND7XgAA5c6iERT.jpg
    92.3 KB · Views: 2
  • FzPVND8XoAA2uLkWQER.jpg
    FzPVND8XoAA2uLkWQER.jpg
    62.8 KB · Views: 2
  • FzPVND8XsAIoxs-CVFG.jpg
    FzPVND8XsAIoxs-CVFG.jpg
    79.9 KB · Views: 2
Back
Top Bottom