Naibu Waziri Aweso Jumaa, taratibu na Makandarasi, utachemka!

Acha kumtisha na kumkebehi naibu waziri
Hiyo miradi,ina mikataba yake,kama kandarasi amepewa 80%,na mradi upo kwenye 10% ya ujenzi maana yake huyo kandarasi ni mwizi.
hayo mambo unayotetea ndio yametufikisha hapa
Unaongea usiyoyajua! Mwingine alipewa Adv. payment leo kesho kiongozi akatokea ikaonekana kana kwamba kalipwa kingi kazi hataki kufanya!!
 
Unaongea usiyoyajua! Mwingine alipewa Adv. payment leo kesho kiongozi akatokea ikaonekana kana kwamba kalipwa kingi kazi hataki kufanya!!
Tunawajua makandarasi wababaishaji na na maofisa mnaokula pamoja
Huyo waziri hakuangalia mkataba?,pesa inaanzia wizarani kwake unataka kunibia hakujua amelipwa lini
Buraza awamu hii sio ya janja janja
 
SULUHISHO NA MAPENDEKEZO

Kama nilivyo anza na ada huko nyuma, Waziri wa Maji na hata naibu wake hawana taaluma katika ujenzi, ingawaje Waziri kakaa Wizara ya zujenzibkwa muda.
Naibu Waziri ndo kabisa ,exposure na experience inabidi aijenge.
Tunapowashambulia si suala la kuangushana kisiasa, bali kuongeza ufanisi wa utekelezaji miradi.
Hawezi mwanasiasa kusimamia miradi, maana siyo part of the contract.
Humu nchi kuna wataalam wengi tu wa kusimamia miradi kwa niaba ya serikali,tena kwa mafanikio.

Kwa Waziri na Naibu wake, nashauri na kupendekeza waanzishe mamlaka maalum ya utekelezaji wa miradi ya maji.
Wizara ya Ujenzi baada ya kusua sua miaka mingi kusimamia miradi ya barabara toka wizarani na kushindwa, serikali ikaanzisha TANROADS.
Mafanikio yake tunayaona.

Wizara ya TAMISEMI baada ya kulalamikiwa sana juu ya utekelezaji wa miradi midogo mingi mijini na vijijini, serikali ilianzisha TARURA.
Nayo tunaona mafanikio mazuri so far.

Wizara ya maji nao wajikite kutengeneza mamlaka itakayoweza kusimamia usanifu, usimamizi na utekelezaji wa miradi ya Maji.
Mimi nitawaita Tanzania Water Projects Authority(TAWAPA-MAJI).
Na Wizara ya Maji ni bora ikafanya hilo kama kipaumbele badala ya sasa mtekelezaji wa miradi ya Maji kuwa Halmshauri zetu, zinazojulikana kwa uzembe na utkelezaji/usimamiaji hafifu wa miradi.

Iwe fedheha kwa Waziri kwenda kusimiamia moja kwa moja mradi na kuwatia Tanganyika Jeki wale anaodhani hawatekelezi miradi.

Lazima tuwe na wanasiasa ambao ni strategic thinkers kwa maana ya kutengeneza modalities na strategies za utekelezaji wa shughuli za serikali.
 
Tunawajua makandarasi wababaishaji na na maofisa mnaokula pamoja
Huyo waziri hakuangalia mkataba?,pesa inaanzia wizarani kwake unataka kunibia hakujua amelipwa lini
Buraza awamu hii sio ya janja janja
Ukiwa na watu wajinga wajinga ndio unaishia kuwa na mawazo kama haya.
Kunakuwepo Client mtoa kazi na mlipaji
Yupo Project Manager, toka kwa Client.
Kuna Supervising Consultant na msimamizi au jicho la Client.
Mwisho kuna mkandarasi, anayefanya mradi.
Kuna Contract inayo waunganisha wote hao .

Watu wote hao wasifanye kazi hata kiduchu na bado pesa inapigwa.
Tuelezeni tu, Client, Project Manager na Consultant ni maboya!

Mirado na ukandarasi si kuuza nya nya sokoni.
 
TARIME: Mbunge Zitto Kabwe amesema amefanya mazungumzo na OCD kuhusiana na hatua hiyo ya Jeshi la Polisi lakini hajaona sababu yoyote ya msingi ya zuio

> Mbunge Esther Matiko(CHADEMA) anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu ambazo bado hazijawekwa wazi

#JFLeo
 
Suluhisho ni kuanzisha taasisi ya maji inayojitegemea kwenye sekta ya maji vijijini kama tarura. Maji ni kichaka cha watu waache wakandarasi waisome kidogo. Barabara sasa hivi kidogo wameelewa
 
Anapewaje 80% wakati physical progress ni 10%? Nawewe acha kujidhalilisha.
Hilo ndio swali la msingi! Hii mirani inayosimamiwa na kandarasi zet za ndani ina matatizo. Mkandarasi anapewa kazi na masharti hela nyingi atakayopewa inarudi kwa waliompa tender! Ndio maana wanatanguliza hela nyingi kwa mkandarasi, wanachota chao na mradi unadorora, baadae mkandarasi anapambana na hali yake "Tanganyika jeki"
 
Suluhisho ni kuanzisha taasisi ya maji inayojitegemea kwenye sekta ya maji vijijini kama tarura. Maji ni kichaka cha watu waache wakandarasi waisome kidogo. Barabara sasa hivi kidogo wameelewa
Mkuu si kwamba hawajui.
Hizi theatrics za kuwatia Tanganika Jeki wakandarasi si tu kwamba zinaudhi, lakini wenyewe serikalini wanajua fika kuwa fedha hakuna za kulipia miradi ya maendeleo.
Makandarasi amkeni kuliona hili.
 
Mkuu si kwamba hawajui.
Hizi theatrics za kuwatia Tanganika Jeki wakandarasi si tu kwamba zinaudhi, lakini wenyewe serikalini wanajua fika kuwa fedha hakuna za kulipia miradi ya maendeleo.
Majandarasi amkeni kuliona hili.
Fedha miradi zinatolewa shinda zinabadilishwa matumizi mbona ushahidi upo!
 
Hakuna mkandarasi fake tatizo ni Serikali kutokulipa makandarasi
Ninachosema Nina ushahidi nacho Nina madai ya miradi tangu mwaka 2012/2013- 2013/2014 - 2014/2015 -2015/2016 katika halmashauri zaidi ya million 700 unaposema fake hujui ama haujaguswa na hili.
Hulipwi kwa sababu uli inflate bei wewe au ulijenga katika low standard!
 
n
Hulipwi kwa sababu uli inflate bei wewe au ulijenga katika low standard!
Wewe ndiye boya.
Unaingia mkataba kama zuzu lisilo enda shule.
Wakati huo huo unalipa mtu kwa kazi ambayo haina usimamizi wala ukaguzi.
Watu serikalini mnatumia wakati weenu na makalio kupangusa viti siku hadi siku.
Na ukiwa fake thinker, you dare kutetea ujinga!
Pathetic.
 
Wanasiasa wasio na uelewa wanasahau kuwa kwenye mradi, fedha ni kifaa cha ujenzi.
Kama hakuna fedha, usitoe kazi, mkandarasi hana muujiza wa kukamilisha kazi bila fedha.

Sasa Wizara ya Maji ilipewa only 22% ya fedha zilizo katika bajeti.
Kwa uelewa huo, mkandarasi atakamilishaje miradi kama uliyempa kazi huna hela.
Hii ni kero!
Wanafikiri wakandarasi tuna mijihela ya kukamilisha miradi yao. Hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom