Naibu Waziri Aweso Jumaa, taratibu na Makandarasi, utachemka!

Nafikiri humjui Awesso vizuri mkuu ila nikuhakikishie tu mkuu kwamba jamaa amejaaliwa karama ya juu sana ya kutekeleza mambo
Ana uelewa mdogo sana.
Kwa nyie watu wake mshaurini ajifunze kazi kwanza kuliko ku seek popularity ya kumfurahisha mkubwa.
Na kwa taarifa tu, ni kwa sababu anawachezea makandarasi wadogo wazalendo, afanye hivyo kwa wakubwa na wa nje, kama hawambwagia miradi na serikali kudaiwa fidia zinazoweza kuleta hasara kubwa.
 
Naibu waziri ni kijana,atulize kichwa afanye mambo kwa busara.

Mara nyingi nimemuona akipayukapayuka hivi.

Unaweza kuongea kwa sauti ya kistaarabu tu na ukaeleweka(si una mamlaka bwana)

Na hii mambo ya kufanya kazi na makamera kwa wingi ndio inaharibu sana utulivu wa viongozi.

Kajamaa kana kiherehere balaaa
 
Acha kumtisha na kumkebehi naibu waziri
Hiyo miradi,ina mikataba yake,kama kandarasi amepewa 80%,na mradi upo kwenye 10% ya ujenzi maana yake huyo kandarasi ni mwizi.
hayo mambo unayotetea ndio yametufikisha hapa
Huyu nae atakuwa mkandarasi na lazima ana elements za ubabaishaji niliwahi kuwa mkaguzi wa mahesabu kwenye miradi inayofadhiliwa na wafadhili katika halmashauri zetu ni majanga wakati huo
 
Viongozi wengi wanatumia nguvu ya dolabbadalabya akili,uzoefu na taratibu za kiuongozi.
Kwa upande wa mh. Aweso haelewi kuwa kazi za ujenzi zinaongozwa na mikataba(civil contracts) na kuingia mkataba na serikali haiendi kuwa a criminal procedure.
Ni vema tukelezwa basi, hao makandarasi waliopigwa Tanganyika Jeki na polisi, wamefunguliwa jalada gani ambslo ni criminal.

Mtu ambaye hajui uendeshaji wa miradi ya serikali , basi ni kwamba hajui kuwa hajui.
Inaonekana wewe ni mmoja wa wale wakandarasi fake au unafaidika kwa njia moja ama nyingine na hao wakandarasi fake. Hahitaji nguvu nyingi kujua wakandarasi fake wanavyopiga pesa za serikali wakishirikiana na watumishi wa serikali wa siyo waaminifu kupiga pesa za serikali bila kufanyakazi stahiki. Sasa waziri anawashughulikia unakuja na mapovu ya OMO hapa? Naibu Waziri pinga kazi hawa watetea wa mafisadi wapo tu mpaka mwisho wa dunia hii usijali sana na kelele za chura hazitakuzuia kunywa maji Mh. Naibu Waziri.
 
Huyu nae atakuwa mkandarasi na lazima ana elements za ubabaishaji niliwahi kuwa mkaguzi wa mahesabu kwenye miradi inayofadhiliwa na wafadhili katika halmashauri zetu ni majanga wakati huo
Mkuu unaongelea Halmashauri tena?
Kitovu cha upigaji wa fedha za Serikali!
Kama wewe ni mtu makini, jiulize na ujijibu kwa nini miradi yote ya barabara imeondolewa Halmashauri zote, na kuanzishwa Mamlaka yenye weledi wa utekelezaji miradi, TARURA.
Mnakagua lakini hamuoni kitu.
 
Inaonekana wewe ni mmoja wa wale wakandarasi fake au unafaidika kwa njia moja ama nyingine na hao wakandarasi fake. Hahitaji nguvu nyingi kujua wakandarasi fake wanavyopiga pesa za serikali wakishirikiana na watumishi wa serikali wa siyo waaminifu kupiga pesa za serikali bila kufanyakazi stahiki. Sasa waziri anawashughulikia unakuja na mapovu ya OMO hapa? Naibu Waziri pinga kazi hawa watetea wa mafisadi wapo tu mpaka mwisho wa dunia hii usijali sana na kelele za chura hazitakuzuia kunywa maji Mh. Naibu Waziri.
Nyie ndo wale nilioongelea kuwa ni ma laymen wa kiwango cha kutisha.
Ila tuanzie mahala, tujiulize maswali kama watu tulioenda shule.
Mkandarasi Fake ni yupi?
Ana vigezo vipi?
Ilikuwaje akaingia mkataba na serikali katika mradi wa maji?
Mbaya zaidi mkandarasi Fake akalipwa!
Mkandarasi Fake hafanyi kazi kwenye mradi, bado analipwa.
Analipwa na watu fulani serikalini , au anaenda kujichotea fedha kwenye kasma?

Sasa hapo Feki ni yupi?
Hapo maana yake kuna viazi wengi serikalini.
Kama wewe ni mmojawapo basi pole tu.
 
Namshauri Waziri aache kujitengezea headlines ambazo wajuzi wanajua kuwa hajui pa kukamata ili kutatua matatizo ya ujenzi wizara ya Maji.
Nina imani kabisa waziri anafikia uamuzi huu baada ya kufuatilia mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi husika. Waziri, siyo kichaa anavamia mkandarasi na 'kumpiga Tanganyika Jeki' kabla ya kwanza kumuhoji masuala kadhaa. Inajulikana baadhi ya makandarasi wana viburi kutokana na kupata miradi kwa njia za kidanganyifu. Hawa lazima waziri, awatembeze kwa 'kucha za vidole gumba vya miguu'!
 
Wakandarasi wengi wa kibongo wamezidi upole.wanazalilishwa na wanasiasa wanatulia tu.ifike kipindi waseme inatosha.mtu anasubiri malipo ya certificate ya kazi aliyofanya kwa zaidi ya mwaka.harafu hapohapo wanategemea kazi iendelee kufanyika huku huu ni muujiza unaoweza kufanyika tz pekee .
 
Nyie ndo wale nilioongelea kuwa ni ma laymen wa kiwango cha kutisha.
Ila tuanzie mahala, tujiulize maswali kama watu tulioenda shule.
Mkandarasi Fake ni yupi?
Ana vigezo vipi?
Ilikuwaje akaingia mkataba na serikali katika mradi wa maji?
Mbaya zaidi mkandarasi Fake akalipwa!
Mkandarasi Fake hafanyi kazi kwenye mradi, bado analipwa.
Analipwa na watu fulani serikalini , au anaenda kujichotea fedha kwenye kasma?

Sasa hapo Feki ni yupi?
Hapo maana yake kuna viazi wengi serikalini.
Kama wewe ni mmojawapo basi pole tu.
Uelewa wako ni mdogo sana kwenye maswala ya upigaji. Unajua maana ya syndicate?? Wanashirikiana hao wakandarasi fake na watumishi wasio waaminifu. Kwani wewe hujui siku za nyuma kulikuwa na kampuni za mifukoni?? Au unajifanya hujui?? Fake maana yake si halisi. Hivyo wanajiita wakandarasi na kubeba sifa ya mkandarasi wa ujenzi wakati si kweli lakini kwa kutumia fedha au makubaliano na hao watoa tender wanapewa kazi kwa makubaliano ya upigaji. Sasa Naibu Waziri anawashughulikia wewe unakuja na malalamiko yasiyo na maana! Mkandarasi amepewa kazi na amelipwa kwa mujibu wa mkataba wa mradi lakini bado anasuasua tu!!
 
Nimekuuliza maswali rahisi.
Unashindwa kuyajibu.
 
Wakandarasi wengi wa kibongo wamezidi upole.wanazalilishwa na wanasiasa wanatulia tu.ifike kipindi waseme inatosha.mtu anasubiri malipo ya certificate ya kazi aliyofanya kwa zaidi ya mwaka.harafu hapohapo wanategemea kazi iendelee kufanyika huku huu ni muujiza unaoweza kufanyika tz pekee .
Mkuu wengi wao kwa sasa wanalipwa kwa mujibu wa mkataba lakini bado hawafanyi kazi kama mkataba unavyosema ndiyo maana hawawezi lalamika kwa kuwa wao ndiyo wenye makosa!
 
Nina imani kabisa waziri anafikia uamuzi huu baada ya kufuatilia mchakato mzima wa utekelezaji wa mradi husika. Waziri, siyo kichaa anavamia mkandarasi na 'kumpiga Tanganyika Jeki' kabla ya kwanza kumuhoji masuala kadhaa. Inajulikana baadhi ya makandarasi wana viburi kutokana na kupata miradi kwa njia za kidanganyifu. Hawa lazima waziri, awatembeze kwa 'kucha za vidole gumba vya miguu'!
Imani yako na masuala ya Contract Administration ni vitu mbali mbali.
Elewa hilo kwa umakini.
 
Swali gani? Si umetaka kujua maana ya fake na nimejibu na nikakueleza syndicate inavyofanya kazi mkuu!!
Nimekuuliza a set of questions ambayo unayakwepa to your own convenience.
Dont be a novice, face up to the facts.
Jijibu yale maswali ujiridhishe Fake ni yupi, otherwise ukishindwa kufikiri critically, you are a Fake Thinker.
 
Mkuu wengi wao kwa sasa wanalipwa kwa mujibu wa mkataba lakini bado hawafanyi kazi kama mkataba unavyosema ndiyo maana hawawezi lalamika kwa kuwa wao ndiyo wenye makosa!
Sina hakika mkuu kama kweli wanalipwa.ingekua hivyo sidhani kama kampuni nyingi za kikandarasi zingefungwa na wengi wanao funga kilio kikubwa ni kufilisika na madeni wanayodaiwa na mabenki.Sasa hivi wakandarasi wengi wanaogopa kufanya kazi na serikali sababu kubwa ni kuto lipwa kwa wakati hivyo kuwaletea migogoro na mabenki.
 
Kuamini ninayo sema angalia bajeti ya maendeleo imetekelezwa kwa asilimia ngapi? jaribu kuangalia kila wizara utaelewa ninacho kisema
 
Sina hakika mkuu kama kweli wanalipwa.ingekua hivyo sidhani kama kampuni nyingi za kikandarasi zingefungwa na wengi wanao funga kilio kikubwa ni kufilisika na madeni wanayodaiwa na mabenki.Sasa hivi wakandarasi wengi wanaogopa kufanya kazi na serikali sababu kubwa ni kuto lipwa kwa wakati hivyo kuwaletea migogoro na mabenki.
Mkuu viongozi serikalini wanalifumbia macho tatizo hilo.
Mkutano wa CRB (Bodi ya Usajili Makandarasi) Mashauriano huko Dodoma mwezi June/July mwaka huu, makandarasi waliilaumu sana, tena sana Serikali kwa kuwafilisi kwa kutowalipa katika muda.
 
Nimekuuliza a set of questions ambayo unayakwepa to your own convenience.
Dont be a novice, face up to the fact.
Jijibu yale maswali ujiridhishe Fake ni yupi.
Mkuu unataka nijibu kila swali wakati maswali yako yote yanajibiwa na vitu viwili tu yaani maana ya neno fake na yanayofuata yanajibiwa na neno syndicate. Criminals huwa wanapanga na kujipanga kufanya uhalifu wao. Ndiyo maana nikakuambia ni syndicate ya wakandarasi fake wakishirikiana na watumishi wa serikali wasio waaminifu ili kukamilisha uharifu wao ndiyo maana ya syndicate. Sasa unashangaa eti kulipwa wakati kazi hajafanyika! Hapo ndipo syndicate inapofanyakazi yake. Hivyo waziri mwaache awashughulikie kwanza hao wakandarasi fake then hao watumishi wasiyo waaminifu.
 
Huyu nae atakuwa mkandarasi na lazima ana elements za ubabaishaji niliwahi kuwa mkaguzi wa mahesabu kwenye miradi inayofadhiliwa na wafadhili katika halmashauri zetu ni majanga wakati huo
Mkuu umetoa general comment kusema kwamba mleta thread ni mkandarasi mbabaishaji, na kwa vile umesema uliwahi kuwa mkaguzi wa mahesabu nina uhakika una input ya kutosha.

Tupe uzoefu wa hayo majanga mkuu, kuanzia jinsi tenda zinavyopatikana, utaratibu wa kuanza kazi, malipo kwa phase husika, na wapi miradi ilikuwa inakwama.
 
Back
Top Bottom