Naibu Spika Dr Tulia amuagiza Waziri Jeñister Mhagama kutafsiri maagizo ya Rais kuhusu korosho kwa maandishi ili kuondoa mkanganyiko!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,961
141,959
Naibu Spika amesema Rais Magufuli alitoa maagizo kadhaa kuhusu ushuru na makato mbali mbali kwa wakulima wa zao la korosho. Miongoni mwayo ni wakulima kutokatwa directly madeni yoyote wanayodaiwa na pili ushuru kulipwa katika halmashauri moja tu.

Hivyo Dr Tulia amemtaka mnadhimu wa bunge mh Jenister Mhagama kutoa tafsiri sahihi ya maagizo hayo ya Rais kwa maandishi ili wabunge na wananchi wote kwa ujumla wawe na uelewa wa pamoja.

Naibu Spika ametoa maagizo hayo wakati akiahirisha bunge usiku huu.

Source TBC!
 
tapatalk_jpeg_1542131910472.jpeg
 
Jambo zuri sana

Na kwa mengine mengi wafanye hivyo hivyo.. hii haikupaswa hata Spika kuomba atende hilo

Ila duh.. Nilifikiri watendaji wanaweka kumbukumbu kwa kuziandika ipasavyo.. muhimu kwa lolote mbeleni
 
Back
Top Bottom