Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,504
- 113,616
Abunuwasi, hoja sio uhalali wa Prof. Beregu kuongezewa mkataba au la, hoja ni waziri kaulizwa swali, hakujibu swali, bali kajibu hoja nyingine, na swali la pili hakujibu kabisa, Naibi Spika akalazimisha eti swali limejibiwa.Jamani tuache ushabiki, jee si ukweli kuwa profesa alikwisha staafu kitambo na ajira yake imekuwa ni ya mkataba kuanzia alipo staafu.
Sasa suala la mkataba baada ya kustaafu ni hiyari ya pande hizo 2 kati ya profesa na taasisi husika. Kama profesa hataki kuendelea na mkataba hakuna wa kumlazimisha na vilevile kama taasisi haimhitaji hakuna wa kulazimisha.
Kwa fikra zangu kwa waziri kusema kuwa profesa alikwisha staafu ilikuwa ni sawa kabisa. Nadhani muuliza swali hakulifremu vizuri swali lake hivyo kwa naibu spika kutamka kuwa swali limejibiwa ni sawa kabisa.
Sikuijua hii ya elimu ya Mama Makinda, ila hili la inferiority complex kweli linawezekana ndio maana ili kuonyesha kuwa yeye ni mbabe, anaonyesha superiorty.Pasco hii tabia ya Anna Makinda hata mimi nimeinotice muda mrefu sasa; mara nyingi wapinzani wanapouliza maswali hasa wale wenye kisomo zaidi yake kama vile Halima Mdee na Zitto, Makinda huwa anapandisha munkali na anajaribu kuwashut down kitu ambacho si busara.
Sitta kweli ni mbabe lakini huwa anakuwa rational anapoongoza shuhuri za bunge hasa wakati wa maswali na majibu.
Tatizo la Makinda ni inferiority complex, kisomo cha diploma ya uhasibu hakitoshelezi mahitaji ya dunia ya ulimwengu wa Internet!
Nanu you are very right. Swali la msingi lilikuwa kwa nini mkataba wake haukuongezwa kwa sababu za kisiasa, jibu la swali la msingi, lilitakiwa liwe, 'sii kweli mkataba huo haukuongezwa kwa sababu za kisiasa, ndipo zingefuatia sababu nyingine waziri alizotoa.Nadhani jibu limekwishatolewa lilipojibiwa swali la kwanza kwamba alikwisha staafu na mwajiri hakutaka kuongeza mkataba maana tayari ano watu wa kuziba pengo. Swali ambalo alitakiwa Mh.Mdee aulize ni kuonyesha kuwa UDSM hawana wataalam kama Baregu na wanamhitaji na pia alinyimwa mkataba kisiasa na hapa majibu ya Mh. Hawa Ghasia aliyotoa kwa umma mwezi uliyopita kuwa hajapewa mkataba kwa sababu ni kiongozi wa Chadema ingeletwa mbele.
Nadhani Mh. Mdee anaweza akalifremu swali tena akinukuu maelezo ya Ghasia na kupeleka bungeni kuonyesha kuwa serikali inapendelea watu kwa itikadi zao za kisiasa katika ajira. Hili halijaisha bado na inatakiwa upinzani walivalie njuga.
Baregu kaponzwa na kuwa yuko upinzani!Nyie kweli ni kizazi cha kupenda miujiza na mambo mepesi mepesi..lolz
Sasa ulitegemea Naibu Spika ambaye yupo pale kwa maslaha ya chama chake cha CCM, ataanzia vipi kumtetea Baregu ambaye ni CHADEMA??
Ukipanda chelewa na kutegemea utachipua mnazi nadhani wewe mpandaji ndiye mwenye matatizo sio chelewa.
Abdulhalim, issue sio Beregu wala upendeleo kwa CCM, issue limeulizwa swali, halikujibiwa kabisa, Naibu Spika analazimisha limejibiwa, ningekuwa mimi ndio Mdee. pale pale baada ya kufungwa mdomo, ningetoka nje, na wabunge wapenda haki, wangemwelewa.Nyie kweli ni kizazi cha kupenda miujiza na mambo mepesi mepesi..lolz
Sasa ulitegemea Naibu Spika ambaye yupo pale kwa maslaha ya chama chake cha CCM, ataanzia vipi kumtetea Baregu ambaye ni CHADEMA??
Ukipanda chelewa na kutegemea utachipua mnazi nadhani wewe mpandaji ndiye mwenye matatizo sio chelewa.
.
Sikuijua hii ya elimu ya Mama Makinda, ila hili la inferiority complex kweli linawezekana ndio maana ili kuonyesha kuwa yeye ni mbabe, anaonyesha superiorty.
Sina problem na Mama Makinda kama naibi spika, ila akibishiwa tuu kwa hoja, adrenalin humpanda haraka na hana control nzuri, hivyo udikteta ndio the only weapon in her hand to be used.
Mfano hai, ni leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.
Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.
Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.
Alichokifanya Naibu Spika, sio tuu ni ubabe, kwa waziri ameulizwa hoja hii, yeye kajibu hoja nyingine, na swali la pili hakulijibu kabisa, bali pale kumlazimishas mbunge kuwa swali limejibiwa na huku halikujibiwa, huu ni zaidi ya ubabe, ni udikteta ndani ya jengo letu la bunge.
Angalizo: Naomba hoja usiwe ASnna Makinda as a person, hatudiscuss watu, hoja ni uendeshaji wa taasisi ya Bunge kidikteta, kuzuia freedom of expression na kuisupress.
YY, nimekubali kuwa kwa vile sababu sio za kisiasa, swali la pili linakuwa rendunty outright, lakini muuliza swali has the right kujibiwa 1. Sababu sio za kisiasa, hivyo Prof. Maghembe amesema Mama Hawa Ghasia muongo au mzushi, na jibu la pili, angejibu kwa vile jibu la kwanza siyo kweli, swali la pili limeshajijibu.Pasco
Swali la pili (2) kutoka kwa Ms Mdee lilikuwepo kwa sababu ya kuamini kuwa Prof Baregu amenyimwa kuongezewa mkataba kwa sababu za kisiasa. Ukiondoa hiyo hoja ya kisiasa basi swali la pili haliko valid.
Ndivyo alivyofanya Waziri kwa kufafanua kuwa Prof hakuongezewa mkataba kwa sababu alishastaafu tangu 1999. Jibu hili la Waziri linaondoa haja ya kujibu swali kwani tayari waziri ameshaonyesha sababu sio itikadi ya Prof Baregu.
Nakubaliana na Naibu Spika...swali limejibiwa na Waziri.
YY