Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 50,466
- 113,550
Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa vikao vya Bunge kupitia TBC na Star TV, kuna jambo nilelinote, nikaona sio vibaya nikiwashirikisha wanabodi.
Spika Sita ni mbabe katika uendeshaji wa vikao vya Bunge, lakini wakati anapoikataa hoja au swali, angalau hutoa sababu.
Siku anapoendesha vikao Naibu Spika, sio mara moja wala mara mbili, nimemshuhudia akikataa hoja kwa ubabe tuu au tuseme udikteta bila kutoa sababu.
Mfano hai, ni leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.
Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.
Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.
Alichokifanya Naibu Spika, sio tuu ni ubabe, kwa waziri ameulizwa hoja hii, yeye kajibu hoja nyingine, na swali la pili hakulijibu kabisa, bali pale kumlazimishas mbunge kuwa swali limejibiwa na huku halikujibiwa, huu ni zaidi ya ubabe, ni udikteta ndani ya jengo letu la bunge.
Angalizo: Naomba hoja usiwe Anna Makinda as a person, hatu-discuss watu, hoja ni uendeshaji wa taasisi ya Bunge kidikteta, kuzuia freedom of expression na kui-suppress.