Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Naibu Spika Anna Makinda ni Dikteta!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Feb 5, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa vikao vya Bunge kupitia TBC na Star TV, kuna jambo nilelinote, nikaona sio vibaya nikiwashirikisha wanabodi.

  Spika Sita ni mbabe katika uendeshaji wa vikao vya Bunge, lakini wakati anapoikataa hoja au swali, angalau hutoa sababu.

  Siku anapoendesha vikao Naibu Spika, sio mara moja wala mara mbili, nimemshuhudia akikataa hoja kwa ubabe tuu au tuseme udikteta bila kutoa sababu.

  Mfano hai, ni leo asubuhi katika kipindi cha maswali na majibu, Mbunge wa Viti maalum Chadema, Bi. Halima Mdee, alimuuliza Waziri wa Elimu kuhusu maswali mawili, la kwanza kwanini Prof. Beregu amekataliwa kuongezwa mkataba kwa sababu tuu yeye ni kiongozi Chadema, huku kuna viongozi wengi tuu wa CCM kwenye utumishi wa umma?. La pili, kama Chadema, itampa ushahidi wa majina ya vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma, jee serikali itakuwa tayari kusitisha mikataba yao?.

  Waziri wa Elimu, Prof. Magembe kwanza alikwepa swali la kwanza, kwa kutokuzungumzia kabisa sababu za Prof. Beregu kunyimwa mkataba, bali alisema, Prof. Beregu, alishastaafu toka 1999, hivyo mwajiri anao uhuru wa kumuongezea mkataba au hapana. Kwa sasa, mwajiri ameshapata watu wenye uwezo kama wa Beregu, hivyo hahitajiki tena, ndio maana hakupewa mkataba mpya.

  Waziri akakaa, Naibu Spika akasema swali linalofuata (Swali jipya), Mdee akasisimama kumwambia Naibu Spika, swali la pili halijajibiwa. Naibu Spika akalazimisha limejibiwa wewe ndio hutaki kukubali. Akamshum dowm Halima Mdee na kuitisha swali linalofuata.

  Alichokifanya Naibu Spika, sio tuu ni ubabe, kwa waziri ameulizwa hoja hii, yeye kajibu hoja nyingine, na swali la pili hakulijibu kabisa, bali pale kumlazimishas mbunge kuwa swali limejibiwa na huku halikujibiwa, huu ni zaidi ya ubabe, ni udikteta ndani ya jengo letu la bunge.

  Angalizo: Naomba hoja usiwe Anna Makinda as a person, hatu-discuss watu, hoja ni uendeshaji wa taasisi ya Bunge kidikteta, kuzuia freedom of expression na kui-suppress.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Feb 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Pasco hii tabia ya Anna Makinda hata mimi nimeinotice muda mrefu sasa; mara nyingi wapinzani wanapouliza maswali hasa wale wenye kisomo zaidi yake kama vile Halima Mdee na Zitto, Makinda huwa anapandisha munkali na anajaribu kuwashut down kitu ambacho si busara.

  Sitta kweli ni mbabe lakini huwa anakuwa rational anapoongoza shuhuri za bunge hasa wakati wa maswali na majibu.

  Tatizo la Makinda ni inferiority complex, kisomo cha diploma ya uhasibu hakitoshelezi mahitaji ya dunia ya ulimwengu wa Internet!
   
 3. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #3
  Feb 5, 2010
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,302
  Likes Received: 1,137
  Trophy Points: 280
  Jamani tuache ushabiki, jee si ukweli kuwa profesa alikwisha staafu kitambo na ajira yake imekuwa ni ya mkataba kuanzia alipo staafu.

  Sasa suala la mkataba baada ya kustaafu ni hiyari ya pande hizo 2 kati ya profesa na taasisi husika. Kama profesa hataki kuendelea na mkataba hakuna wa kumlazimisha na vilevile kama taasisi haimhitaji hakuna wa kulazimisha.

  Kwa fikra zangu kwa waziri kusema kuwa profesa alikwisha staafu ilikuwa ni sawa kabisa. Nadhani muuliza swali hakulifremu vizuri swali lake hivyo kwa naibu spika kutamka kuwa swali limejibiwa ni sawa kabisa.
   
 4. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #4
  Feb 5, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  To be honest Anna Makinda ni dikteta na hasa yakija mabo yanayoibana CCM ama Serikali..kabaya sana haka kamama.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Abunuwasi, hoja sio uhalali wa Prof. Beregu kuongezewa mkataba au la, hoja ni waziri kaulizwa swali, hakujibu swali, bali kajibu hoja nyingine, na swali la pili hakujibu kabisa, Naibi Spika akalazimisha eti swali limejibiwa.
   
 6. N

  Nanu JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Nadhani jibu limekwishatolewa lilipojibiwa swali la kwanza kwamba alikwisha staafu na mwajiri hakutaka kuongeza mkataba maana tayari ano watu wa kuziba pengo. Swali ambalo alitakiwa Mh.Mdee aulize ni kuonyesha kuwa UDSM hawana wataalam kama Baregu na wanamhitaji na pia alinyimwa mkataba kisiasa na hapa majibu ya Mh. Hawa Ghasia aliyotoa kwa umma mwezi uliyopita kuwa hajapewa mkataba kwa sababu ni kiongozi wa Chadema ingeletwa mbele.

  Nadhani Mh. Mdee anaweza akalifremu swali tena akinukuu maelezo ya Ghasia na kupeleka bungeni kuonyesha kuwa serikali inapendelea watu kwa itikadi zao za kisiasa katika ajira. Hili halijaisha bado na inatakiwa upinzani walivalie njuga.
   
 7. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Sikuijua hii ya elimu ya Mama Makinda, ila hili la inferiority complex kweli linawezekana ndio maana ili kuonyesha kuwa yeye ni mbabe, anaonyesha superiorty.

  Sina problem na Mama Makinda kama naibu spika, ila akibishiwa tuu kwa hoja, adrenalin humpanda haraka na hana control nzuri, hivyo udikteta ndio the only weapon in her hand to be used.
   
 8. leseiyo

  leseiyo Senior Member

  #8
  Feb 5, 2010
  Joined: Oct 25, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Da na mimi nimeona hiyo issue bungeni.Kwa kweli inasikitisha sana I think Anna Makinda anatakiwa awe makini na alichukulie bunge kama taasisi ya umma otherwise bunge litakuwa la mchezo tu.Maswali ya Mdee yalikuwa ya msingi but the way alivyomcrush inauma sana na inatia huruma kwa wabunge wa opposition.To be honest hajamtendea haki kabisa.
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Feb 5, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,292
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  NI MTIZAMO TU!.....
  ni mawazo tu
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Nanu you are very right. Swali la msingi lilikuwa kwa nini mkataba wake haukuongezwa kwa sababu za kisiasa, jibu la swali la msingi, lilitakiwa liwe, 'sii kweli mkataba huo haukuongezwa kwa sababu za kisiasa, ndipo zingefuatia sababu nyingine waziri alizotoa.

  Jibu la swali la pili, lingekuwa, kwa vile sababu sio za kisiasa, hakuna haja ya kuleta huo ushahidi wa hao vigogo wa CCM kwenye utumishi wa umma.

  Waziri swali la msingi kakwepa, na swali la pili hakujibu kabisa.

  Naibu Spika angeweza kumweleza Mbunge, kuwa swali husika kuhusu hizo sababu za kisiasa, linamhusu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais. Mernejimenti ya Utumishi wa Umma, na huko ndiko huo ushahidi wa Chadema, waupeleke.

  Ile manner ya Mama Makinda kulazimisha kuwa limeshajibiwa, ilikuwa ni udikteta.
   
 11. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #11
  Feb 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,478
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Nyie kweli ni kizazi cha kupenda miujiza na mambo mepesi mepesi..lolz

  Sasa ulitegemea Naibu Spika ambaye yupo pale kwa maslaha ya chama chake cha CCM, ataanzia vipi kumtetea Baregu ambaye ni CHADEMA??

  Ukipanda chelewa na kutegemea utachipua mnazi nadhani wewe mpandaji ndiye mwenye matatizo sio chelewa.
   
 12. K

  Kasanga Member

  #12
  Feb 5, 2010
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baregu kaponzwa na kuwa yuko upinzani!

  Chuo kina uhaba wa wahadhiri kuliko maelezo! Wahadhiri wengi wametimkia UDOM na nchi jirani ya Rwanda!

  Mbona aliyekuwa Vice Chanchellor (Prof Luhanga) baada ya kustaafu tena akitokea kwenye wadhifa mkubwa sasa hivi kaajiriwa tena hapo kitivo cha Uhandisi?

  Kwa mtindo huu Tanzania tutabaki kuwa nyuma daima!

  Hebu angalia wenzetu Rwanda na Angola ambao miaka michache iliyopita walikuwa kwenye vita lakini sasa hivi wameishapiga hatua kubwa sana!

  Tumebakia tu kuimba UTULIVU NA AMANI!
   
 13. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #13
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  Abdulhalim, issue sio Beregu wala upendeleo kwa CCM, issue limeulizwa swali, halikujibiwa kabisa, Naibu Spika analazimisha limejibiwa, ningekuwa mimi ndio Mdee. pale pale baada ya kufungwa mdomo, ningetoka nje, na wabunge wapenda haki, wangemwelewa.

  Hapa hoja sio siasa za vyama, ni issue ya uendeshaji tuu, kuna siku huyu mama alizuia swali la Ole Sendeka hivyo hivyo, na Ole Sendeka ni CCM.
   
 14. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #14
  Feb 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,918
  Likes Received: 1,318
  Trophy Points: 280
  Kweli wadau mmeona,

  Hata mimi sipendezwi huyu Naibu spika. Bora wale wenyeviti kama Jenista Mhagama
   
 15. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #15
  Feb 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,478
  Likes Received: 161
  Trophy Points: 160
  Nyie nyie bana mnanishangaza sana. Ila endeleeni kusubiria miujiza. Mie nanawa mikono na kizazi hiki.
   
 16. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #16
  Feb 5, 2010
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,935
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Pengine tatizo ni kuwa hazijui sheria vizuri ndo maana anashindwa kuzifanyia kazi na inabidi awe mbabe.Mwenzie Six anabukua sana na anakuwa anajua vitu vingi.
   
 17. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #17
  Feb 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280

  Pasco ukitaka kujua C.V. za wabunge nenda kwenye Website yao ingawa kuna wakati fulani ilikuwahaipatikani sijui walikuwa wanawaficha vihiyo wao!!
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Feb 5, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Pasco

  Swali la pili (2) kutoka kwa Ms Mdee lilikuwepo kwa sababu ya kuamini kuwa Prof Baregu amenyimwa kuongezewa mkataba kwa sababu za kisiasa. Ukiondoa hiyo hoja ya kisiasa basi swali la pili haliko valid.

  Ndivyo alivyofanya Waziri kwa kufafanua kuwa Prof hakuongezewa mkataba kwa sababu alishastaafu tangu 1999. Jibu hili la Waziri linaondoa haja ya kujibu swali kwani tayari waziri ameshaonyesha sababu sio itikadi ya Prof Baregu.

  Nakubaliana na Naibu Spika...swali limejibiwa na Waziri.

  YY
   
 19. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #19
  Feb 5, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Bunge letu ni kichekesho na halina chembe ya uzalendo wa ufanisi katika kuliendesha na hata kutekeleza majukumu yake.

  Linaongozwa kwa ushabiki, hisia na ulimbukeni wa kupita kiasi. Mara nyingi hoja za kuibana serikali ni zile tuuu zenye masilahi kwa waongoza bunge au wabunge (wa ccm) ndizoo hupewaa nafasii nzuri.

  Mara nyingi spika na naibu wake wameshindwa kuweka pembeni ukada wao na wabunge wa CCM wanaongozwaa na hisia, ushabiki na ulimbukenii katika kusifiaa hojaaaa..hawana masilahi ya taifa au uzalendooo..

  Miswada na bajeti mbovuu zimekuwaa zikiungwa mkonoo kwa ushabikii tuuu. Mswaada wa SS ni hisia na ushabikii dhidi yake kutoka kwa wabunge na wala sio umakiniii..
   
 20. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #20
  Feb 5, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,618
  Likes Received: 23,708
  Trophy Points: 280
  YY, nimekubali kuwa kwa vile sababu sio za kisiasa, swali la pili linakuwa rendunty outright, lakini muuliza swali has the right kujibiwa 1. Sababu sio za kisiasa, hivyo Prof. Maghembe amesema Mama Hawa Ghasia muongo au mzushi, na jibu la pili, angejibu kwa vile jibu la kwanza siyo kweli, swali la pili limeshajijibu.
  Hivyo kwa walioangalia live, swali la kwanza limekwepwa, lapili halikujibiwa, muulizaji was shunned down.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...