Naibu Spika amzuia Waziri Mkuu Majaliwa kujibu swali la barua ya KKKT

byembalilwa

JF-Expert Member
Aug 7, 2012
2,034
918
James Mbatia alitaka kama Serikali inatambua kazi za taasisi za kidini na umihimu wa dini katika nchi,na Jana kuna barua imesambaa mitandaoni ikiwataka KKKT wajibu ndani ya siku kumi na ikidhaniwa kutoka Serikalini ,ni upi msimamo wa Serikali kuhusu barua hiyo?

Naibu spika amesema kwasasa waziri mkuu hajibu maswali yote ya dini hata Said Kubenea hakujibiwa pia,kwa hiyo waziri mkuu hatojibu.
====

Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amemkingia kifua Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kujibu swali kuhusu Serikali kulipa siku 10 Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kufuta waraka wake wa Pasaka uliotolewa Machi 24, 2018, ambao mbali na masuala ya kiroho, ulitaja changamoto tatu za kijamii.

Swali kuhusu KKKT iliyoandikiwa barua ya kutakiwa kufuta waraka huo na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, limeulizwa leo Alhamisi Juni 7, 2018 katika kipindi cha Maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu na mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia.

Katika swali lake, Mbatia ametaka kujua ukweli kuhusu barua hizo lakini baada ya kumaliza kuuliza swali hilo, Dk Tulia amesema haliwezi kujibiwa na kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni.

“Kuna barua wamepewa KKKT na TEC (Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania ) wakitakiwa kufuta nyaraka zao za Kwaresima,” amesema Mbatia na kuitaka Serikali kueleza uamuzi huo una lengo gani.

Mara baada ya swali hilo, naibu spika huyo amesema, “mtakumbuka mheshimiwa Kubenea (Saed-mbunge wa Ubungo-Chadema) alimuuliza waziri Mkuu swali linalohusu dini na mheshimiwa Spika alizuia suali hilo lisijibiwe.”

Baada ya maelezo hayo, Dk Tulia alimuita mbunge mwingine kuuliza swali huku Mbatia ambaye pia ni Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi akiketi na kuzungumza na na wabunge wengine wa vyama vya upinzani chini kwa chini.


Pia soma> Serikali yaamuru KKKT kuufuta waraka. Yatishia kulifuta "Baraza la Maaskofu wa KKKT" na kuwashitaki

 
Naibu spika azuia Waziri Mkuu Majaliwa kujibu swali la Kubenea asubuhi hii kuhusu barua za onyo walizoandikiwa TEC na KKKT.

Je kwanini kuandika barua ni rahisi ila kujibu swali inakuwa ngumu.
 
Leo ni kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu ambapo Mh. Mbatia alimuuliza waziri mkuu kuhusu barua kutoka.serikalini inayotaka madhehebu ya KKKT na RC kufuta waraka wa kitume uliotolewa wakati wa pasaka.

Naibu spika Tulia alilikataa swali hilo kuwa ni swali la kidini akirejea mfano wa Spika Ndugai alipokataa swali la Kubenea kuhusu masuala ya kidini.

Mytake. Hii serikali inakimbia kivuli chake. Barua wanaandika wenyewe kuwalazimisha madhehebu kufuta waraka haafu wanaogopa kutoa ufafanuzi bungeni.
 
Mh.Mbatia alitaka kama serikali inatmbua kazi za taasisi za kidini na umihim wa dini katika nchi,na Jana kuna barua imesambaa mitandaoni ikiwataka KKKT wajibu ndani ya siku kumi na ikidhaniwa kutoka serikalini ,ni upi msimamo wa serikali kuhusu barua hiyo?
Naibu spika amesema kwasasa waziri mkuu hajibu maswali yote ya dini hata Said kubea hakujibiwa pia,kwa hiyo waziri mkuu hatojibu

Kumbe naibu spika ana nguvu za kumzuia waziri mkuu
 
Labda mI ni mgumu kuelewa, kwahiyo waziri mkuu asubiriwe wapi ili aulizwe?
 
Wamkataze na raisi anapoomba aombewe na Taifa liombewe kwani hayo ni mambo ya kidini na wakiteuana pia waache kuapa kwa vitabu vya dini ila watumie katiba za vyama vyao.

Unazizurutisha taasisi za kidini, mkihojiwa hamtaki kujibu eti ni mambo ya kidini!!!

Awamu ya V-WONDERS!!!
 
Back
Top Bottom