Kwa ufupi jana shirika la ndege la ATCL lilikuwa na safari ya kuelekea Mbeya kutokea Dar es Salaam iliyokuwa ianze saa saba na dakika kumi (7:10).
Abiria wakajipanga vyema na wakawa kwenye ndege tayari kuondoka. Ilipofika 7:20 likasikika tangazo kutoka kwa "Pilot" akitangaza kuwa uwanja umefungwa gafla kwa kuwa kuna ndege za kijeshi zinatua na kupaa kwa wakati huo hivyo basi abiria wakaombwa kutoka nje ya ndege na kurudi kwenye eneo la kusubiria wasafiri mpaka ilipofika saa nane na robo walipotangaziwa kupanda ndege tena.
Jambo la kusikitisha ni kwamba:
1. Mara baada ya kushushwa kwenye ndege haikuonekana ndege yoyote iwe ya Jeshi au mtu binafsi ikitua au kupaa mpaka wanatangaziwa kurudi kwenye ndege kwa mara ya pili tayari kwa safari
2. Waliporudi kwenye ndege kabla mlango kufungwa aliingia abiria mpya (Naibu spika) ambaye hakuwepo mara ya kwanza wakati wanatangaziwa kufungwa kwa uwanja
Hapa kazi tu!