Naibu Spika achelewesha safari ya ndege ATCL kwenda Mbeya! Abiria wakalishwa uwanja wa ndege zaidi ya saa moja

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Kwa ufupi jana shirika la ndege la ATCL lilikuwa na safari ya kuelekea Mbeya kutokea Dar es Salaam iliyokuwa ianze saa saba na dakika kumi (7:10).

Abiria wakajipanga vyema na wakawa kwenye ndege tayari kuondoka. Ilipofika 7:20 likasikika tangazo kutoka kwa "Pilot" akitangaza kuwa uwanja umefungwa gafla kwa kuwa kuna ndege za kijeshi zinatua na kupaa kwa wakati huo hivyo basi abiria wakaombwa kutoka nje ya ndege na kurudi kwenye eneo la kusubiria wasafiri mpaka ilipofika saa nane na robo walipotangaziwa kupanda ndege tena.

Jambo la kusikitisha ni kwamba:

1. Mara baada ya kushushwa kwenye ndege haikuonekana ndege yoyote iwe ya Jeshi au mtu binafsi ikitua au kupaa mpaka wanatangaziwa kurudi kwenye ndege kwa mara ya pili tayari kwa safari

2. Waliporudi kwenye ndege kabla mlango kufungwa aliingia abiria mpya (Naibu spika) ambaye hakuwepo mara ya kwanza wakati wanatangaziwa kufungwa kwa uwanja

Hapa kazi tu!
 
Walichokosea hapo ni kubord abiria,wakati kuna NOTAM ya ndege za jeshi kufanya mazoezi muda huo,zoezi kama hilo lazima kiwanja kifungwe kwa muda...Poleni sana.
 
Hii kitu ATCL kumbe hawajajirekebisha tu!? Mi naona kama pana uhitaji wa kusubiri mtu iwe kwa Rais na Makamu Wa Rais tu..Mambo ya kusubiri sijui waziri au naibu spika nikupoteza credibility tu kwa wateja si wana magari na wananchi tunawajazia mafuta mi naona kiongozi akichelewa flight basi apatr gari au angalia schedule ya flight ingine
 
Huenda huyo Naibu Spika alikuwa na taarifa za kuchelewa kuondoka ndege kabla ya muda wa checkin haujaisha akaona bora akae sehemu hadi muda utakapo karibia.

Au alikuwa chumba cha VIP tofauti na abiria wengine hadi muda wa kuondoka ulipowadia.

Tusihukumu kwa taarifa za kusikia bila uchunguzi.
Tumshukuru mtu alieleta taarifa hizi itasaidia wakubwa wachunguze ukweli. Kama naibu kasababisha bila shaka wahusika watakutana na rungu la mkuu wa wanunuzi wa hizo ndege.
 
Hii kitu ATCL kumbe hawajajirekebisha tu!? Mi naona kama pana uhitaji wa kusubiri mtu iwe kwa Rais na Makamu Wa Rais tu..Mambo ya kusubiri sijui waziri au naibu spika nikupoteza credibility tu kwa wateja si wana magari na wananchi tunawajazia mafuta mi naona kiongozi akichelewa flight basi apatr gari au angalia schedule ya flight ingine

Yote haya yatapita...Wakati ule Mwanza tulizoeshwa kuwasubiri Mawaziri vijana wa JK, Mmoja alikuwa madini mwingine sasa hivi yupo FastJet wao ilikuwa ni kunywaaa wakitosheka wanakuja ndani ya ndege wako bwiii lakini sasa hivi imekuwa historia
 
Kama habari hii ni kweli basi Thom Mwang'onda atatosha kwa ubunge wa Mbeya mjini baada ya Sugu kustaafu.

Bunge nalo linunue ndege zake bhana!
 
mashirika ya umma na biashara wapi na wapi, tulishajaribu na tulifeli vibaya! a wise man learns from other men's mistakes.
 
Back
Top Bottom