Naibu mkuu wa polisi amefungwa jela miaka 15

thesym

JF-Expert Member
Aug 15, 2012
3,825
4,754
Naibu mkuu wa polisi wa zamani nchini Uchina amefungwa jela miaka 15 kwa makosa ya ufisadi, vyombo vya habari nchini humo vimeripoti.

Li Dongsheng alikuwa na uhusiano na Zhou Yongkang, aliyefungwa jela maisha mwezi Juni mwaka jana kwa makosa ya ufisadi.

Habari za kuhukumiwa kwake zimeripotiwa katika mitandao ya kijamii ya runinga ya taifa nchini humo CCTV.

Afisa huyo anadaiwa kupokea hongo ya takriban yuan 22m ($3.3m; £2.3m).

Alituhumiwa pia kutumia vibaya mamlaka akiwa serikalini kati ya 1996 na 2013, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari wakati huo.

Li alifutwa kazi rasmi Februari mwaka jana baada ya uchunguzi dhidi yake kuanzishwa, pamoja na washirika wengine wa zamani wa Zhou Yongkang.

Zhou alihudumu kama mkuu wa usalama wa Uchina kabla ya kustaafu 2012.
source: BBC SWAHILI
 
Mkuu ungeaza kwa kuandika kichwa cha habari chako hivi
"Naibu mkuu wa polisi wa zamani nchini Uchina amefungwa jela miaka 15" nafikiri ingekuwa nzuri zaidi
 
Back
Top Bottom