Naibu Meya wa zamani wa jiji la Arusha Prosper Msofe (CHADEMA), ashinda Kesi dhidi ya TAKUKURU Mahakamani

Jembe Jembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
749
1,797
MAHAKAMA ya hakimu mkazi Arusha,mapema leo Alhamisi imemwachia huru naibu meya wa zamani wa jiji la Arusha ambaye ni diwani wa sasa wa kata ya daraja mbili ,Prosper Msofe(Chadema) baada ya kushinda kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kusababisha upotevu wa kiasi cha shilingi milioni nane fedha za halmashauri ya jiji la Arusha .

Msofe alifikishwa mahakamani hapo septembe 23 mwaka jana na taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa {TAKUKURU} na mwenzake ambaye ni ofisa mtendaji wa kata ya daraja mbili,Modestus Lupogo na kusomewa makosa matatu likiwemo la kujipatia kiasi hicho cha fedha kwa njia ya udanganyifu kinyume cha sheria.

Akizungumza nje ya mahakama Msofe ambaye alikuwa akitetewa na wakili ,Philp Moshi alieleza kuwa kesi hiyo ilimpa wakati mgumu katika kipindi cha mwaka mmoja na anaamini kuwa ilipandikizwa na maadui zake wa kisiasa kwa lengo la kumzoofisha na harakati zake za kisiasa hasa alipoonyesha nia ya kugombea nafasi ya umeya katika jiji la Arusha.

0b7e4e20bce7e73a241e2fbcdc746add.jpg
 
Back
Top Bottom