kizaizai
JF-Expert Member
- Mar 31, 2010
- 6,067
- 7,552
Mmmh sijui. Inaonekana yupo njiani kwenda CCM.Kumbe walitaka kumteka kwasababu ya ulevi?
Mmmh sijui. Inaonekana yupo njiani kwenda CCM.Kumbe walitaka kumteka kwasababu ya ulevi?
![]()
Dady Igogo, Diwani wa Gangalonga ambaye pia ni Naibu Meya wa Manispaa wa Iringa
NAIBU Meya wa Manispaa ya Iringa ambaye ni Diwani wa Kata ya Gangalonga (Chadema), mkoani Iringa Dady Igogo, amenusururika kuwa baada ya kuvamiwa na watu wasiojulikana. Anaripoti Faki Sosi … (endelea).
Igogo ameeleza kuwa ametishwa kutokana na mfululizo wa matukio hayo amedai kuwa ni kiashiria kibaya cha amani.
Anasema kuwa amesikitishwa na kitendo hicho kutokana kuwa kinaviashiria vya ubaguzi wa kisiasa ambapo ameeleza kuwa alivamiwa na vijana wenye pikipiki ambapo walimshambulia.
“Wakati narudi nyumbani nilisimamishwa na pikipiki kama nne waliokuwa kama wanataka kuniuliza jambo. Nilifungua kioo! Ghafla walinivamia na kuanza kunipiga na kunitoa kwenye gari. Niliacha gari na kufanikiwa kukimbia kwa miguu.
“Walichukua simu yangu, pamoja na kuchomoa ufunguo wa gari wakaondoka. Wakati wananipiga walikuwa wanasema ‘kahamishe makaburi ya kwenu’,” ameeleza Igogo.
Amesema kuwa amesikitishwa pia baada ya kuuwawa kwa kiongozi wa Chadema Kata ya Hananasif Daniel John. “Inaumiza sana. Sijui Mama yake Ben Saanane yuko katika hali gani?”
Ameeleza kuwa kuendelea kuwa mwanasiasa wa upinzani ni hatari ambapo hata baadhi watendaji wamekuwa vinara wa kufanya ubaguzi wa kisiasa nchi akimtolea mfano Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ametoa tamko la wazi kuwa anawabagua wapinzani.
Habari ambazo hazitathibitishwa zinadai kuwa Igogo amejiuzuru nafasi yake ya Unaibu Meya wa Manispaa ya Iringa, sababu za kujizuru kwake hazijafahamika.
Chanzo: Mwanahalisi
Mwanahalisi hao...waliomchafua mzee wa watu...na baadaye kumsafisha kwa zana zote za usafi!Sasa kumbe anaugomvi wa makaburi!!! Sasa siasa inakujaje?
Halafu mara aseme habari za Daniel hapohapo mama yake Ben Saanane!!!!
Hivi siyo huyu jana niliskia katangaza kujiudhuru unaibu meya!?
Mzalendo2015 umesema kweli, naona kuna tatizo hapa la watanzania wengi tumebweteka na hali ya amani iliyo kuwepo hapo awali, ukweli ni kwamba ile Tanzania ya amani sasa ina pita kwa kasi kubwa sana kiasi kwamba hizi nyufa zinazo jitokeza za kutugawa kama Taifa moja zisipo zibwa mapema gharama ya kuzijenga itakuwa kubwa mno, nchi nyingi duniani zimeingia kwenye migogoro ya kitaifa katika nchi zao kwa sababu ya matukio ya kishenzi mna hii, na kuna uwezekano mkubwa kwa maadui zetu kutumia mianya Kama hii na kutusambaratisha kabisa.Imefika wakati vyombo husika viangalie utaifa wetu zaidi ya maslahi yoyote ambayo ni muda mfupi yanakuja na kupita ila Taifa letu lenyewe litadumu kuwepo siku zote. MUNGU IBARIKI TANZANIA.Hizi akili za kinyesi mnazitoa wapi?
Talk about ISSUES not PERSONAL and EVENTS....!!!Kuna Mitanzania hasa hii iliyokunywa maji ya bendera ya kijani......haijielewi na haijitambui..!!Mtu ameleta hoja ya kutaka kutekwa,jaribio la kumwuua au kupigwa badala ya kutaka kujua nani anahusika na uunyama huo mijitu inaanza kumshambulia mlalamikaji.....!!!!
Non-sense and Pumbaf zenyu!!!
Amechanganya mambo hadi huruma. Huenda hata hakushambuliwa na mtu yeyote.Sasa kumbe anaugomvi wa makaburi!!! Sasa siasa inakujaje?
Halafu mara aseme habari za Daniel hapohapo mama yake Ben Saanane!!!!
Hivi siyo huyu jana niliskia katangaza kujiudhuru unaibu meya!?