Naibu Mayor Amlipua Mkurugenzi

Naibu Mayor Amlipua Mkurugenzi

Joined
Dec 8, 2013
Posts
9
Reaction score
3
Leo mchana diwani wa kata ya daraja II na Naibu Mayor wa Jiji la Arusha Ndg Prosper Msoffe amezungumza na vyombo vya habari akimuagiza Mkurugenzi wa idara ya maji kufukua chemba zote za maji taka za mahoteli kumi(10) aliyoyaziba kwa zege kwa madai ya kuwadai wamiliki wa mahoteli hayo,
Hoteli hizo ni pamoja na Naura Spring, Natron Hotel, Mid way hotel etc ...Kilichotokea wamiliki wa mahotel hayo walikuwa hawana taarifa ya madeni hayo zaidi ya kuona police wakiwa na bunduki wakifika kwenye maeneo yao na kuanza kuziba chemba hizo mapema jana asubuhi!..

Naibu Mayor huyo amesema itakapofika kesho jioni mkurugenzi huyo Bi Ruth awe amezibua chemba hizo kinyume cha hapo atamlazimisha kufanya hivyo kwani njia aliyotumia ni kinyume na sheria na taratibu za nchi hii...

Source: Mi mwenyewe nilikuwepo kwenye mkutano
 
CCM wameshafulia..sasa wataanza kuuza wake,waume na watoto wao,ukizingatia chaguzi haziishi sasa hivi.
 
Huyu mkurugenzi alifunga chemba makusudi kwamba anawadai wenye mahoteli bila wenye mahoteli kuwa na taarifa kama wanadaiwa??
 
Back
Top Bottom