Naibu Katibu Mkuu wizara ya maji apokelewa rasmi, ateta na watendaji

Naibu Katibu Mkuu wizara ya maji apokelewa rasmi, ateta na watendaji

DAWASA

Official Account
Joined
Oct 7, 2010
Posts
158
Reaction score
103
Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso ameongoza mapokezi ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Bi Rose Zakaria Ambrose aliyeteuliwa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hasaan mapokezi yaliyofanyika mapema leo katika ofisi za DAWASA Mkoani Dar es salaam.

Katika mapokezi hayo, Waziri Aweso aliambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Mhandisi Mwajuma Waziri, Menejiment ya Wizara, Wakuu wa Taasisi chini ya Wizara ya Maji na Viongozi waandamizi kutoka Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) na kueleza mipango mikakati ya kuimarisha huduma za Maji Nchini sambamba na miradi inayoendelea.

“Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Maji tunakupongeza kwa nafasi uliyopata na tunaahidi ushirikiano katika kufanikisha shughuli zako za kuwapatia huduma bora na ya uhakika ya Majisafi na Salama kwa Watanzania” alisema Waziri Aweso

“Pia tumempitisha katika mipango ya muda mrefu na mfupi na mwelekeo wetu kama Wizara katika kusimamia maono ya Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua Mama ndoo kichwani sambamba na kusimamia Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”alisisitiza Waziri Aweso

IMG-20260209-WA0032.jpg
IMG-20260209-WA0074.jpg
 
Wajinga nyie hatuna maji miezi mingapi?
Juzi mmetunywesha maji ya tope yukaumwa matumbo
Watu wanajichimbia visima na kuuza maji bila hata kipima
Pumbavu
 
Vp hali ya maji huko ???
Upatikanaji

Ova
 
Back
Top Bottom