Niliagiza gari kupitia agent wa hapa Dar es Salaam tangu mwezi wa tatu, ameniambia kuwa meli imefika tangu tarehe 21 mwezi wa tano lkn haijapeleka manifesto TRA ili iweze kulipiwa kodi jmaani kuna ukweli ndani yake?
Ananiweka roho juu kweli au ndo nimeibiwa, km kuna mtu anaweza nisaidia ani Pm nitampa donge nono
ndugu kama agent amekuahakikishia gari iko kenye meli uwe na amani...kaa pata maji ya bariiidiii usubirie kitu yako. Unanikumbusha mwaka 2007 nimeagiza gari yangu ya kwanza, nimeenda kwa agent samora akaniambia imefika mombasa, nkarudi siKu mbili Badae akaniambia meli imefika ila haijaanza kupakua mizigo, dah nkajua nimeliwa ,sana sana niliona nabaki na makaratasi mkononi ila gari ndo ishakwenda, nlipanda ghorofa la ppf towers japo niione meli uku roho inauma , siku ya tatu, ya nne , ya saba , ya nane, aaah nkajisemea hapana, naenda kufa na agent, nlipofika akaniambia imeshushwa ila bado iko yard mpaka ikagul;iwe tena ndo ipate gate pass, dah nkaoona sasa uyu jamaa sijui nimfanyeje...ikabidi nimtafte mshikaji wa bandari aniingize nicomfirm kama kweli gari ipo...nkaigia kijanja mpaka kwenye yard, dah nkakuta machine iko na makaratasi, kuifungua inanukiiiiiiiiiiaaaaaaa, dah yani nkaenda kulala kwa amani.
....furaha yangu ilipunguzwa na ushuru kuwa uplifted. Ila nlifurahi sana,by the way, meli zamani zilikuwa zinatumia muda mrefu iko apo bandari salama hata siku 20 bila kushusha mzigo, ila juzi bungeni mh mwakyembe amesema meli sasa zinasubiri hardly siku 9 mpaka 10 ndo zinashusha mizigo. So mwanaJf mwenzangu uwe na amani, agent ambaye yuko registerd hawezi kukuingiza mkenge kiivo,be patient iyo kitu unapata. ALL THE BEST.