Naiba, nakiri ila sijutii hata kidogo

Revenge!
Unamfanyia nani? X wako, mumewe au wote wawili?
Umejaribu kuwazia outcome zingine zaidi ya wewe kufededwa ambayo umejiandaa nayo?

Can you live with it; huyo mpenzi wako akiuwawa na mumewe au unafikiri ni wewe pekee una hasira?

Sijui unasali wapi, lkn tumeambiwa "kisasi ni kazi yake Mungu"

Dada, nina mtizamo tofauti, "kisasi ni kazi yangu" ni hivi, naweza kuwa malaika na naweza kuwa shetani. Nikupe stori moja nikiwa shule a level, nilifanya uamuzi wa kipuuzi sana nikaacha shule na kutorokea nchi moja ya jirani. Mkuu wa shule japo hatukuwa na uhusiano wowote na nilikuwa mmoja wa wanafuzi watatizo he went out of his way kuhakikisha narudi shule na nikamaliza na kufaulu vizuri. Huyu mzee alikuja kustaafu akawa amechoka mbaya, nilikuwa namfuatilia maisha yake, siku moja nikamtembelea hakuamini, tukapiga stori, nikarudi mara ya pili na ya tatu akafunguka kuwa maisha yanamshinda, pensheni alinunua basi la masafa marefu watoto wakalifisadi. Sina pesa lakini niliuza vipande vya UTT na gari ambalo sikuwa nalihitaji sana na kuna jamaa alikuwa analichumbia siku nyingi. Nikampa mzee pesa kikawa kianzio cha kukopa benki akanunu basi jingine kwa utaratibu wa asset financing. Nimemtafutia kijana mwaminifu analiendesha na vile nina uzoefu kwenye biashara hiyo nimekuwa namfundisha mzee wapi pa kubana. Anaendelea vizuri na Mwezi wa tano anamaliza mkopo benki na wanataka akope jingine! Aliniambia anataka akimaliza benki aanze kunilipa nimemwambia mzee zungusha pesa kwanza mimi utanilipa tu usijali. Huyu ni mimi nikilipa fadhila kwa alionifadhili, kumbuka nilikaa kwa miezi saba sina usafiri. Ukiwa rafiki yangu wa kweli nitakwenda kuzimu kwa ajili yako, ukiamua kunifanyia ushenzi basi tegemea majibu mara kumi wala simwachii MUNGU!
 
Ninafahamu reformer, nina mkakati wangu wa kujilinda, na wa kushambulia na unaweza ukafanya kazi au usifanye kazi lakini elewa hii ni vita na majeruhu ni lazima wawepo. Huwezi kuingia vitani na hutaki kupata majeruhi, hiyo haitakuwa vita. Kinachotakiwa ni mkakati wa kuhakikisha madhara kwa upande wako ni madogo kadiri inavyowezekana, mkakati huo ninao, swali kama utafanya kazi au la litajibiwa na muda.
Matokeo yake yanaweza yakawa mabaya kuliko unavofikiri..inaweza isiishie kuwa majeruhi tu ila ukapoteza uhai au ukatoa uhai wa mtu. Unless you are ready for anything because of that love.
 
Naipenda hii scenario, naona nzuri sana hata kuitolea comment naona utamu balaa!!

Sikia Ilushenisti nataka nikunong'oneze kitu, naona utamu wa muda umekupofua, fungua macho na uone vizuri:
..........mwache mke wa mtu haraka iwezekanavyo huyo sio mke wako ni X demu wako...........dk 90 za kuchezea mwali zilikuishia na refa katoa ubingwa uwe umefanyiwa rafu, limefungwa goli kwa mikono lakn tayari ushindi umekutupa mkono.........kwa kifupi jilaume wewe na sio huyo bwana.............dunia itakuhukumu...........hapa huna jinsi yeyote ya kuhalalisha unachokifanya eti kwa sababu alikufanyia sijui ushenzi..........sasa hv endelea kuona unafurahi, but ipo siku utanielewa

Jibu hili swali:
Wewe kwanini ulishindwa battle ya dk 90 za kumgombania huyo mwali????....halafu sasa hv ndio unalalamika kuwa ulichezewa rafu???? mm sikutishi lakn lazima tukemee tabia km hiyo wengn wasijeona upo kwenye right track

UNAKOSEA.........take this as my last word!!!!!
 
Last edited by a moderator:
..................................................................... Ukiwa rafiki yangu wa kweli nitakwenda kuzimu kwa ajili yako, ukiamua kunifanyia ushenzi basi tegemea majibu mara kumi wala simwachii MUNGU!

Hapo nilipounderline........take care, jaribu kuhimili mihemiko yako!!!!!!!
 
kumbe haya mambo yapo?
mlongo wangu snowhite una la kusema hapa?
mimi nimebaki na maswali kibao kichwani...... tusubiri labda Nicas Mtei anaweza akatutafutia mada inayofafanua haya.....
mwalimu gfsonwin naomba ufafanuzi wako tafadhali......
naona rafiki yangu Kaunga kaishia kutoa ushauri wa Kiroho tu, lol!
Lord have Mercy........

mmmmmhhhhh!!!!! dunia ina mambo.... kwa kweli kwenye hili mimi nipo kimya kabisa
 
Blue G, Kulipa kisasi ni hisia za kwanza zinazoniongoza, mapenzi yapo ila si sababu.
Unaweza kuwa sawa ila mara nyingi mi nimeona revenge sio suluhisho hata kidogo bali ni muendelezo wa chuki baina ya watu wanaolipiziana kisasi,huwezi jua revenge yako italeta madhara mabaya pengine hata kuutoa uhai wa mtu,utajisikiaje?kuna ule usemi kuwa hate has bring many problems but has not succeded to solve even a simngle problem,em utafakari usemi huu na kisha ufikirie possible outcomes za revenge yako.
 
Then you have a very good heart,utumie huohuo moyo wako mzuri kuepuka kulipa kisasi ambacho hujui matokeo yatakuwa ni nini, wanasema hakuna mwanzo usio na mwisho,utaanzisha kisasi lakini je wajua mwisho wake ni nini?Unajua jamaa kajipangaje?kama aliweza kuplan kuwatenganisha na huyo X wako kwa akili kiasi ambacho hukuweza kutambua,je unajua anaweza kufanya nini ili kulinda penzi lake na huyo mkewe?Think twice mkaka don't give space for regreats in your life. Ilushenisti
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kuwa sawa ila mara nyingi mi nimeona revenge sio suluhisho hata kidogo bali ni muendelezo wa chuki baina ya watu wanaolipiziana kisasi,huwezi jua revenge yako italeta madhara mabaya pengine hata kuutoa uhai wa mtu,utajisikiaje?kuna ule usemi kuwa hate has bring many problems but has not succeded to solve even a simngle problem,em utafakari usemi huu na kisha ufikirie possible outcomes za revenge yako.

Hv nani kamwambia penzi linagombaniwa, eti hadi kulipa kisasi?............penzi hushawishiwa, mapenzi ni hisia tu its something unrealistic!!!!!
 
Yeah that's it na wengi huwa tunajisahau sana kuhusiana na hilo.
Hv nani kamwambia penzi linagombaniwa, eti hadi kulipa kisasi?............penzi hushawishiwa, mapenzi ni hisia tu its something unrealistic!!!!!
 
Ilushenisti em jaribu kutumia ushauri unaopewa na wanajf ni wenye manufaa kwako,na nataka tu kukukumbusha kuwa hakuna mbabe wa dunia hata siku moja,you have plans yes,but inasemekana kuwa ulipoishia kuwaza wewe mwizi wako huwa ndio anaanzia kwenye hiyo point,shortly you are blinded with the sweet love you've been given with your ex girl within those five days,coz mbona hukuwaza kurevenge hapo kabla ukawaze revenge baada ya kumake love tu?Mapenzi yalimponza Samsoni,Adamu na wengine wengi angalia usiongeze listi ya watu hao.
Ninafahamu reformer, nina mkakati wangu wa kujilinda, na wa kushambulia na unaweza ukafanya kazi au usifanye kazi lakini elewa hii ni vita na majeruhu ni lazima wawepo. Huwezi kuingia vitani na hutaki kupata majeruhi, hiyo haitakuwa vita. Kinachotakiwa ni mkakati wa kuhakikisha madhara kwa upande wako ni madogo kadiri inavyowezekana, mkakati huo ninao, swali kama utafanya kazi au la litajibiwa na muda.
 
Last edited by a moderator:
Ngoja nikueleze kitu, mimi nilipatwa ishu kama yako, mimi mupenzi wangu alinipenda sana na tulipendana sana tena sana, ila kulikua na kaka ambae ni kama kaka angu nimekua nae na yeye akitoka chuo lazima anitafute, ki ukweli nilikua simpendi kabisaaaaa..... ila yeye akawa ananipenda sana mimi nikawa sijui, na mama ake alikua ananipenda sana, siku moja tukakutana viwanja nipo na wangu, nikamtambulisha kuwa kutana na mpenzi wangu, kumbe ndo kama nimempa upenyo, akamfuatilia mpaka akajua anapokaa, marafiki zake na kila mwenendo wake na rafiki zake akafanya chini juu wakawa rafiki zake pia na yeye pia, muda ukienda mara ananitumia msg usiku nipo na shemeji, mi uku nimelala uku mi nshawasiliana nae mupenzi wangu ananiambia yupo om, mara akapandikiza chuki, nami nikaanza kumchukia kwa matendo kwa sababu niliamini maneno yake.

nikaamua niachane nae mpenzi wangu, nikakata mawasiliano, ikapita kama miezi kadhaa akaniambia Mimi ninakupenda sana toka zamani ila sipendi nikualibie uhusiano wako, labda bado unampenda shem wangu, au nijaribu kuwapatanisha, nikasema no... kweli kipindi nilijichukia mimi na wanaume, mwishowe nikampenda huyo rafiki yangu na tukaoana na tumezaa mtoto tayari, na nikaja nikakutana na rafiki yake akanipa mkanda mzima ulivyokua unaenda, alimjaza mpenzi wangu maneno nami pia ili tujenge chuki, kweli niliumia sana tena sana, ila mimi ni mkristu nilipiga moyo konge nikasamehe na maisha yanasonga mbele, japo mitihani ktika ndoa ipo, na mume wangu nampenda sana tena sana, na huyo mpenzi wangu alinipata kwa simu tukawa tunawasiliana, tunajuliana khali, ila alijua kila kitu kilichotokea kuwa ni mchezo mchafu sana, mpaka anasema mi ntakuja kumuua mumeo ila namwambia kama kweli wewe ni mkristo samehe, na nashukuru Mungu, kaoa na mke wake sasa anamimba, so we are both happy, kwahiyo kaka yangu jifunze kusamehe, kupenda ni ugonjwa ila mwombe Mungu akusaulishe, kumbuka duniani tu wanapita.....
 
Mwambie tu huyo mmewe what goes around thos days is coming around now...avumilie kama ulivovumiliaga
 
naelewa maumivu ya mapenzi yalivyo! uliumizwa kaka! hata ningekuwa mie ningefanya kama ufanyavyo wewe! who am i to judge? fanya uonayo yafaa
 
Back
Top Bottom