Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta asisitiza kuwa hatarajii kusalia kwenye Ligi ya Ubelgiji msimu ujao -

eden kimario

JF-Expert Member
Jun 13, 2015
10,227
16,178
Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta amesisitiza kuwa hatarajii kusalia kwenye klabu yake ya Genk msimu ujao na badala yake kuchezea Ligi ya Primia ya England.

Samatta ambaye ni kinara wa ufungaji wa klabu ya Genk ambao ni mabingwa wa Ligi ya Ubelgiji, anawaniwa na klabu kadhaa za England.

Akizungumza na runinga ya Azam TV, mshambuliaji huyo amesema yupo tayari kuchukua nafasi ya Romelu Lukaku wa Man United endapo atapata nafasi.

Lukaku amekuwa na wakati mgumu Old Trafford msimu uliopita na amekuwa akihusishwa na mipango ya kutaka kuhamia klabu ya Inter Milan.

Alipoulizwa na Azam TV endapo anaweza kuvaa viatu vya Lukaku Samatta alijibu: "Kwanini nishindwe? Naweza kuvaa. Mafanikio yanaweza yasiwe kama niliyopata Genk, lakini naweza kucheza, sababu mpira ni uleule. Tayari nipo Ulaya na najua nini natakiwa kufanya kwenye ligi za Ulaya. Itakuwa ni klabu kubwa na presha itaongezeka mara dufu, yaweza kuwa vigumu kuzoea mwanzoni lakini mwisho nitazowea."

Samatta ameendelea kuficha ni klabu gani za England ambazo uongozi wake unafanya majadiliano nazo kwa sasa.

Hivi karibuni alidokeza kuwa kuna klabu sita za Primia zinamuwania.

"Kwa sasa hivi siwezi kusema sana, ni kitu ambacho kipo kwenye mchakato nasubiria kitakapokuwa tayari na wakati utakapofika nitaweza kukizungumza. Lakini sijioni tena Genk, namuomba Mwenyezi Mungu litimie, lakini ikishindikana bado nina mkataba na Genk."

Katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari mwaka huu, klabu ya Cardiff ilituma ofa ya Pauni milioni 13 kumng'oa Genk, lakini uhamisho huo ukakwama.

Hata hivyo Cardiff imeshuka daraja.

Mwezi uliopita Samatta aliliambia gazeti la Mwanchi kuwa: "Ndiyo, nitaondoka mwishoni mwa msimu huu...(klabu ya England) moja inanifukuzia sana na imekuwa ikipiga simu kwa wakala wangu kila siku."

Samatta amefunga zaidi ya magoli 30 msimu huu akiwa na klabu ya Genk.

Streka huyo mwenye miaka 26, ameifungia Genk magoli 23 na kumaliza kama mshambuliaji bora wa ligi. Pia ameifunga magoli 9 kwenye michuano ya ligi ya Europa.

Jina la Samatta limekuwa likiimbwa na mashabiki wa Genk, na wamekuwa wakimuomba mshambuliaji huyo kusalia klabuni hapo kucheza ligi ya Mabingwa Ulaya.

"Hawa jamaa (Genk) hawajacheza Ligi ya Mabingwa tangu mwaka 2011 enzi za akina (Kevin) De Bruyne, najua wanataka nicheze msimu ujao lakini Ligi Kuu ya England ina heshima yake...ni ligi ambayo tayari imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na Ligi Kuu ya Ubelgiji. Ni ligi ambayo inapendwa na watu wengi duniani, Ligi inayoonekana sehemu kubwa duniani. Yaani kwa vitu vingi iko mbali," amesema Samtta.

Samatta alijiunga na Genk akitokea TP Mazembe Januari 2016 ambapo alitia saini mkataba wa kumuweka katika klabu hiyo hadi msimu wa 2019/20.

Kabla ya kujiunga na Mazembe alikuwa akiichezea klabu ya Simba ya Tanzania.
hqdefault.jpg
 
Ajifananishe kwanza na welbeck na chicharito au Luis saha

In united there is no second chance otherwise your a Britain lad
 
Mbwana Alli Samatta mimi kama mtanzania nakushauri baki Genk kidogo! Ligi ya England tamu ila ngumu kupata nafasi ya kuwika kirahisi! Kina Sanchez, Morata......wamechemka pale!
 
Samata anaweza,,kucheza EPL,,kikubwa akomae zaidi manake ile ligi ni ngumu mtu kwa mtu mguu kwa mguu pasi jiwe,
Ajiandae kukutana na mabeki visiki,,
 
Mimi namshauri abaki huko huko Genk walau kwa msimu ujao ili awe mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya mabingwa ulaya. Baada ya hapo aende sasa kupuyanga anakotaka. Historia ina raha yake.
Binafsi siamini kama kuna klabu ya England inayoshiriki klabu bingwa msimu ujao kumhitaji Samatta. Nb: mwamuzi wa mwisho ni yeye mwenyewe, wakala wake na hiyo timu yake ya Genk.
 
Mimi namshauri abaki huko huko Genk walau kwa msimu ujao ili awe mtanzania wa kwanza kucheza ligi ya mabingwa ulaya. Baada ya hapo aende sasa kupuyanga anakotaka. Historia ina raha yake.
Binafsi siamini kama kuna klabu ya England inayoshiriki klabu bingwa msimu ujao kumhitaji Samatta. Nb: mwamuzi wa mwisho ni yeye mwenyewe, wakala wake na hiyo timu yake ya Genk.
Baba yake Haji Manara alisha cheza Champions League kama sikosei. Japo zamani jina lilikuwa tofauti.
 
Back
Top Bottom