Nahodha atangaza uamuzi mgumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nahodha atangaza uamuzi mgumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 30, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Na Dennis Luambano
  WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, ametangaza uamuzi mgumu wa kutengua nafasi za Kamanda wa Polisi wa Mkoa (RPC) na Mkuu wa Usalama wa
  Barabarani (RTO) ambaye mkoa wake utakuwa kinara wa matukio ya ajal
  Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana wakati akizindua Kampeni ya Kunywa Pombe Kistaarabu inayoratibiwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL), na aliwaagiza makamanda na wakuu hao kuyakagua magari yote ya mizigo na mabasi ya abiria yanayoingia katika mikoa yao ili kuwabaini madereva wanaoendesha magari mabovu na wengine wanaokuwa wamelewa.

  "Serikali inaendelea kukisimamia kikosi cha usalama barabarani ili kiweze kutekeleza sheria za usalama barabarani ipasavyo. Kuanzia sasa nawaagiza makamanda wa polisi katika mikoa na wakuu wa usalama wa barabarani kuyakagua magari hayo kila mkoa yanapopita hadi mwisho wa safari.

  "Nitafuatilia taarifa za magari katika mikoa yote na nikiona ajali nyingi zinatokea katika mikoa fulani basi makamanda na wakuu wa usalama barabarani watakuwa wameshindwa kazi katika mikoa yao, kwa hiyo ni bora waziachie hizo nafasi na watapangiwa kazi nyingine za kufanya," alisema Nahodha.


  Alimtaka Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga, kulifikisha agizo hilo kwa makamanda na wakuu wa usalama barabarani.


  Alisema hatua ya kukagua magari ya mizigo na mabasi ya abiria kila yatakapopita katika mkoa mmoja na kwenda mwingine itasaidia kupunguza ajali kwa kiasi kikubwa.


  "Hakuna kinachoshindikana, hata kama kuna uhaba wa vifaa vya kukagulia magari na madereva, lakini tujue kwamba hakuna sayansi inayomshinda binadamu kwa sababu basi linaloenda mwendo kasi linaonekana kwa machom tu ya mwanadamu bila kutumia kifaa chochote," alisema Nahodha.


  Alisema matarajio yao ni kuhakikisha kuwa ifikapo Desemba mwaka huu wanafanikiwa kupunguza ajali kwa asilimia 50.


  Alikiagiza Kikosi cha Usalama Barabarani kuwafungia madereva wanaosababisha ajali kutokana na makosa ya uzembe kwa kuwanyanganya leseni za udereva.

  "Katika kipindi cha mwaka 2008 hadi Agosti 2011 kumetokea ajali 944 ambazo zimesababishwa na madereva waliotumia pombe na kati ya Januari hadi Agosti 2011 tayari kumetokea ajali 111 za namna hii. Takwimu hizi zinatuonyesha kuwa tatizo la utumiaji pombe ni kubwa kwa madereva.

  "Kuanzia sasa hatutasubiri ushahidi wa mahakamani ndipo tuwafungie madereva, kuwafungia miezi sita peke yake haitoshi, bali tuna uwezo wa kuwafungia hadi miaka 10, najua kuna wanasiasa watasema watu hao watakosa ajira, lakini mimi nasema bora wakose ajira kuliko kuendelea kuua watu kwa uzembe," alisema Nahodha.


  Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Richard Wells, alisema kampeni hiyo itakayogharimu Shilingi milioni 350 ni maalumu kwa ajili ya kuwafundisha na kuwakumbusha wanywaji wa pombe kunywa kistaarabu na hatimaye waweze kubadilisha mienendo yao.


  "Kampeni hii itaendeshwa katika vyombo mbalimbali vya habari na itasaidia kuwakumbusha wateja wetu unywaji wa kistaarabu ambao hautamfanya kujuta kwa yale aliyoyafanya akiwa amekunywa," alisema Wells.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Labda itasaidia ajali!!!
   
 3. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Tumeshazizoea kauli za nguvu ya soda zinazotolewa na viongozi kutoka hiki chama kilichozeeka!
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hiyo ni hadithi hata siku mmoja hawezi dhubutu kutengua
  Huko Rwanda Kagame alifanya hii kitu na imeleta sana mafanikio
  (ikitokea ajali kagame alikuwa anatoa siku kadhaa ili RPC awawajibishe kwanza walio chini yake na kisha Kagame mwenyewe anamwajibisha RPC.
   
 5. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  That can not materialize in a corrupt state like Tanzania where people are appointed due to their closeness to higher authority. Nahodha decision might be genuine in itself but it is likely to be hampered by bosses senior to him.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nilimwona akilonga kwenye kile kipindi cha ITV sikijui jina ila ata SITTA alilonga uko.
  KAMA kweli atayasimamia anayosema tutashukuru maana nasikia ajari hushika nafasi ya 3 baada ya ukimwi na malaria kwa kuua watu Tz
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  Mambo haya tumeyaongelea mara nyingi tu lakini tunachoshuhudia ni kwa viongozi wa kitaifa kupigia kampeni ya kuhamasisha ulevi wao wenyewe wakishiriki hadharani kama hawana akili timamu vile.

  Shamsha awanyoshee kidole hawa viongozi waandamizi serikalini wanaokunywa na kumahasisha ulevi ndipo kauli yake itasikika vizuri kwa wananchi wa kawaida.
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  NATO- no action talking only
   
 9. N

  NewOrder JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 489
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 45
  Toka ninaanza kujitambua, nimesikia habari za wafanyakazi wa umma kuhamishwa kutoka sehemu moja kwenda nyingine. Hata kama wameharibu!! "Kupangiwa kazi nyingine" nadhani ni kuhamisha tatizo kutoka sehemu moja kwenda nyingine!! Kama hatujafikia "kufukuza" au "kumshitaki" mtumishi wa umma, lolote nitakalosikia ni bure!!

  Mwenyewe anayesema hakuwafaa watu 4,000 wa Jimbo lake la uchaguzi kule Zenji. Leo eti ana manufaa kwa zaidi ya 40,000,000!!!
   
 10. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Tatizo la mfumo wa uongozi wa Serikali yetu, sehemu yenye maandishi mengukundu badala ya kuwajibishwa hao waliozembea eti atawapangia au kuwahamishia sehemu nyingi wakaendelee kuharibu. Bora asingelonga vinginevyo ni kutupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.
   
 11. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,445
  Likes Received: 22,362
  Trophy Points: 280
  Porojo tu za kisiasa. Akitaka aone kwamba akisemacho ni kigumu kiasi gani, basi siku moja asubuhi aamkie Ubunge na kile kimashine cha kupima pombe.
  Siku hiyo abiria wachache sana watakao safiri
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Labda waagize kile kipima ulevi kinachofungwa ndani ya gari DUI (Driving Under Ifluence), ambacho kinaakisi kiwango cha alcohol alichonacho driver, na kama kiwango kimepita wastani kitapiga kelele na abiria watasikia kulazimisha dereva asitishe kuendesha gari kwa ajili ya usalama. Nchi zilizoendelea kama Marekani, dereva ye yote akishapatikana na kosa la DUI onyo la kwanza ni kufungia kifaa hicho, na ikitokea tena kuendesha akiwa under influence basi atafungiwa kabisa. Hii sheria iko kwenye baadhi ya state na karibu nchi nzima itafuata mfumo huo.
   
 13. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160

  Na hao wanaopinga ulevi nao waache kutumia vitu vyote vitokanavyo na kodi za sisi walevi zikiwemo barabara, shule na Hospitali
   
 14. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  hahah...naona Pinda kama kanyooshwa pasi ...kawa kijanaaa. Ulabu si machezo.
  Wazo la Nahodha ni zuri ila utekelezaji wake ....!?
   
 15. thereitis

  thereitis JF-Expert Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 297
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Magamba ni wazuri wa maneno kuliko vitendo.... wameshindwa kuvuana magamba atawezaje kuwashughulikia hawa POLISI-CCM?
   
 16. Al Zagawi

  Al Zagawi JF-Expert Member

  #16
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,723
  Likes Received: 246
  Trophy Points: 160
  Mkuu badilisha heading ya thread yako....hakuna uamuzi hapo ni kusudio ikiwa hayo yatatokea. huwezi kuita kusudio kuwa ni uamuzi:biggrin:
   
 17. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #17
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Duh!! Hii ni ya Kutengenezwa? au Live? Kama ni live Basi ni Ngumu Kumeza~!!!
   
 18. AirTanzania

  AirTanzania JF-Expert Member

  #18
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 678
  Trophy Points: 280
  Huyu Sio Mtoto wa mkulima bali ni mtoto wa Mafisadi akiwa [​IMG]
   
 19. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #19
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Twende Kwenye Hoja!! Hili suala siku zote Nilikuwa Naombea Litokee kama sio Jana basi Leo!! Huweze Kupunguza Ajali Bila KuControl Madereva Walevi na Magari Mabovu na elimu kwa raia wawapo ndani ya Magari Yenyewe!! Napendekeza wa Kwanza wa Kufukuzwa Kazi Awe Afande Mpinga kwani Jitihada Zake zote Zimeshindwa Kuzaa Matunda!! Magari Mabovu Dar ndio Kitovu Chake!! Unakuta gari imebeba Container inakwenda Zambia Halafu Imepata Breakdown Kabla Hata ya Kufika Kimara!! Hii Ni aibu Kubwa Kiasi Gani?? Magari Mabovu yanatoka Bandarini na Makontena na Mengine Yanatoka Wazo na cement ambayo hayana hata Hadhi ya kutembea Barabarani Halafu Polisi wanakenua Meno Tu!! Ni nini kimetufikisha Hapa? Vuai Kumbuka Umeishi Hotelini kwa muda mrefu na Gharama Kubwa tufanyie Hata Kitu Kidogo cha Kutufanya tukukumbuke!! Hata Just Kusimamia Sheria!!
   
 20. m

  matawi JF-Expert Member

  #20
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  mimi siko magamba lakini kwa wazo hili nawapongeza. Ila shida ya magamba ni tofauti kati ya kutoa wazo na kulitekeleza
   
Loading...