Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

nilikuwa nawaza wakaka wa maana tunaopishana nao wakati tunatoka kazini au miangaiko huwa wakogo wap? wanishi wapi? maana tunakutana nao wakiwa busy hata bila salamu, nikawaza huwa wakitoka kazini wanaendaga wapi?

nikawaza kuna siku nilikuwa na mi stress yangu natoka supermarket mlangoni nilikutana mkaka alivyokuwa smart, nilisema ee mungu wewe wajua.

kumbe mkitokaga kazini mnaendaga club ambapo wakina sie hatuend?

lakini mleta mada una matatizo gani? wewe unaenda club mwanamke ulimuokota club sasa unategemea nini mdogo wangu

lakini uzi huu umenifanya nijiulize hivi kumbe kuna wanaume wanapenda wapendwe na waheshimiwe? hii si kweli

lakini mbona mkipata wanaowapenda mnachukulia poa? mnaona hawana thamani.

nahisi wewe kinachokusumbua ni umri, na bahati mbaya wewe ni kavulana, ila ungekuwa mwanaume na una malengo usingekuwa unazoazoa club afu unategemea atabadilika never.

si semi kuwa waenda club wote wadangaji ila asilimia kubwa wadangaji, wachache wanaenda kupunguza stress

take this frome me ukiona umekosana na mwanamke hata kabla ya mwezi akawa tiyari kwenye mahusiano jua hakukupenda.

hivi una moyo gani mtu anakuchanganya na vizee wewe bado upo?

unataka ukimwi au?

lastly,ndege wafananao uruka pamoja hilo ndo chaguo lako, ukiendelea kudanga club basi kubali matokeo. umri unakusumbua u need to grow up dogo
Anachokitafuta atakipata
 
Mkuu hivi hapo unasbiri nini? Mapenzi ya hvyo ni ujinga
 
Nashukuru mungu niliamza haya mambo utotoni,mapema sana,changamoto nyingi nilishamalizana nazo mapema.
 
nilikuwa nawaza wakaka wa maana tunaopishana nao wakati tunatoka kazini au miangaiko huwa wakogo wap? wanishi wapi? maana tunakutana nao wakiwa busy hata bila salamu, nikawaza huwa wakitoka kazini wanaendaga wapi?

nikawaza kuna siku nilikuwa na mi stress yangu natoka supermarket mlangoni nilikutana mkaka alivyokuwa smart, nilisema ee mungu wewe wajua.

kumbe mkitokaga kazini mnaendaga club ambapo wakina sie hatuend?

lakini mleta mada una matatizo gani? wewe unaenda club mwanamke ulimuokota club sasa unategemea nini mdogo wangu

lakini uzi huu umenifanya nijiulize hivi kumbe kuna wanaume wanapenda wapendwe na waheshimiwe? hii si kweli

lakini mbona mkipata wanaowapenda mnachukulia poa? mnaona hawana thamani.

nahisi wewe kinachokusumbua ni umri, na bahati mbaya wewe ni kavulana, ila ungekuwa mwanaume na una malengo usingekuwa unazoazoa club afu unategemea atabadilika never.

si semi kuwa waenda club wote wadangaji ila asilimia kubwa wadangaji, wachache wanaenda kupunguza stress

take this frome me ukiona umekosana na mwanamke hata kabla ya mwezi akawa tiyari kwenye mahusiano jua hakukupenda.

hivi una moyo gani mtu anakuchanganya na vizee wewe bado upo?

unataka ukimwi au?

lastly,ndege wafananao uruka pamoja hilo ndo chaguo lako, ukiendelea kudanga club basi kubali matokeo. umri unakusumbua u need to grow up dogo
umemaliliza kila kitu
 
Dawa chungu ndio inatibu mkuu achana nae kubali maumivu ya leo ili ufurahi maisha yajayo
 
Jombaaa bila shaka huyo mwanamke utakuwa ulimuokota Villar Park (nipo Mwanza right now) na hakuna penzi la club lililowahi kudumu...wanawake wengi wa viwanja huwa ni Machangudoa,nimeshatembelea sana maeneo kama Villar Park (Mwanza),Malindi club,Club Alberto,Diamond club (Moshi-Kilimanjaro),Giraffe hotel/club,Conner bar,Mrina etc (DSM),Shivazi (Arusha) maeneo hayo hakuna mwanamke seriously wa kutengeneza nae maisha wengi ni Malaya wa kutupwa hata ukiwa unamiliki B.O.T huwezi kumridhisha!
 
uliposema tu neno club sijaendelea kusoma
 
Habari zenu ndugu zangu, matumaini yangu ya wazi kuwa hamjambo na mnaendelea na harakati za kulisukuma gurudumu la Maisha.

Kwa upande wangu weekend ya leo haijakaa sawa, nahisi kuchanganyika, Presha sio presha, kuumwa sio kuumwa, yaani kwa ujumla hali ni mbaya.

Nikianza na mkasa wangu huu wa mapenzi ambao umenitokea kati yangu mimi na mpenzi wangu ambaye kiukweli nilitokea kumpenda sana na kushindwa kujizuia.

Awali nilikuwa naishi Dsm sema nikaamishwa kikazi kwenda Mwanza, kazi yangu ni nzuri na kama kijana nimeweza kumudu kupanga nyumba nzuri na kausafiri ka kutembelea.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa 9 mwaka Jana ndio nilikutana na huyu mwanamke kwenye klabu moja hivi jijini Mwanza. Hakika nilitokea kumpenda. Safari ya mahusiano ikaanzia hapo.

Kumbe historia ya huyu Crush wangu haikuwa nzuri hasa kutokana na background yake ya watu aliotoka nao kipindi cha nyuma, watoto wa mjini wanasema MDANGAJI.

Ama kweli mapenzi upofu ndio naamini, licha ya kufikishiwa habari zake lakini binafsi sikuzitilia maanani sana, nilijisemea moyoni kwamba nitamrekebisha aje kuwa Mama watoto wangu.

Kwa ufupi kwenye mahusiano yetu ya kipindi cha miezi 6 tumepitia katika changamoto nyingi sana, tumewahi kuachana na kurudiana zaidi ya mara tano. Chanzo kikubwa cha kugombana kwetu ni huyu mwanamke kuendekeza sana starehe. Ikifika weekend kama ya leo ni lazima mtoke.

Hata Kama nikimshauri tusitoke basi atatumia mbinu yeyote atoke kisha arudi asubuhi anigongee au arudi Kulala nyumbani kwake, mbaya zaidi kichwa cha pombe hana.

Tatizo lingine ni kuendeleza mawasiliano na ex's zake, nimefumania text za whatsapp na kawaida akichart na ma-ex wake. Nilikuwa nikijaribu kumwambia abadilike anaacha kwa muda kisha anaendelea. Mbaya zaidi kwny simu niliyomnunulia.

Nakumbuka siku moja tulitoka club ukazuka ugomvi baina yetu ambao ulipelekea nimtembezee kipigo cha mbwa koko. Kipindi hicho alikuwa hajapata kazi. Kila kitu nilikuwa najitaidi kumuhudumia ukiacha kodi ya nyumba aliyokuwa akilipa mwenyewe.

Baada ya ugomvi huu uliopelekea akae ndani wiki nzima kutokana na majeraha ulimpelekea aka-abort mimba yangu ya mwezi mmoja. Penzi likavunjika na kila mtu akachukua time zake.

Ukapita mwezi m1 bila mawasiliano, nilichofanya kosa nikaanza kutembea na rafiki zake ambao kwa idadi wanafika wanne. Drama zote hizi alikuwa akizishuhudia na nyingine kupelekewa taarifa.

Baada ya kufanya upumbavu wote huu, nilirudi nyuma na kujitafakari upya na kuamua kumtafuta na mapenzi yakarudi upya. Kipindi hiki alikuwa kwny mahusiano na Mzee mmoja mume wa mtu ambaye alikuwa akimsaidia katika mahitaji yake.

Tukashauriana tukapime afya zetu, bahati nzuri hatukukutwa na maambukizi, lakini kumbe huyu mwenzangu alipanga afanye revenge pasipo mimi kujua.

Kwanza aliweka utaratibu ambao naweza kusema sio sahihi, yaani yeye atakuwa na yule babu kimaslahi na hata nilipokuwa nawakuta sehemu nilijifanya kama siwajui mpk yule Mzee atakapokuwa ameendoka.

Hali hii ilinisumbua sana hasa ukizingatia wivu ulikuwa juu zaidi, kama hiyo haitoshi hivi majuzi katoa kali, alikuwa anakunywa na Mzee wake, baada ya Mzee kusepa akaja ex wake wa zamani ambaye yupo vzr kifedha.

Baada ya kuona picha ile kiukweli nilizidiwa na wivu na kusababisha ugomvi Mkubwa ambao Kama sio mkono wa Mungu huyu mwanamke angekuwa Marehemu.

Nimekaa nikaona hapana kwa hili lilotokea ngoja nije niombe ushauri kwa wakubwa zangu ambao huenda Wakawa wamepitia kwenye changamoto kama hizi waweze kunishauri haya.

Nimtafute nimuombe radhi maana moyo wangu bado unampenda? Au ni-move on na Maisha yangu? Labda huenda haikuwa ridhki aliyoniandikia Mwenyezi Mungu.

Nipo kwenye hali mbaya. Nakaribisha ushauri na wale ndugu zangu wa matusi na kejeli nawakaribisha pia.

Nawasilisha.
Nikweli au simulizi
Km nikweli skiliza moyo wako unasema nini
 
Mh! Ameshagundua huna uwezo kumuacha na atakusumbua sana ipo siku ataleta mwanaume kwenye kitanda chako na ujiandae namajambazi atakuletea
 
Ametoa mimba yako. !?? Mtu wa club..!?? Wew ukamsaliti na rafiki zake wanne alafu leo mrudiane utegemee anakuja kwa nia nzuri!??? labda umrudie umlee usepeee tuu
Wastage of time, sepa mazima
 
Yaani mi mwanamke nikijua tu kanisaliti, basi ndio nakua simtaki tena,hata kama nilikua nampenda mpaka naumwa. maana tayari kawa nuksi.
 
Nilipoona tu umekutana nae club niliweka mashaka kidogo, simaanishi wote wanaoenda huko ni vicheche lkn... kwa jinsi ulivyojihangaisha na huyo shangingi napata ukakasi hata kukushauri maana kwa ninavyokuona bado hujajifunza kitu kwake... Any way Achana nae na anza kuhudhuria misa za kanisani ukapate mke huko
 
Back
Top Bottom