Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Nahitaji ushauri wa haraka, moyo unauma

Hakuna aliyesema kuwa itakuwa rahis? An brother you are a codependet. Ww uko radhi umuombeasamaha wkt kosa alifany yeye.

Jikaze, futa namba zake, picha zake, ikilazimika hama mtaa. Usipite maeneo ambayo yatakukumbusha kuhusu yeye.
Now invest maisha yako kwenye kutafuta pesa, tafuta maisha jombaaa.

Nakupa miezi mitatu. Ukiweza vumilia baasi utakuwa umemsahau.
Asante sana, japo jana ametuma wadogo zake kwangu. Hawakunikuta
 
Daaaaah kuna watu Wamepitia njia hatari sana, achana naye Fanya maamuzi ya kiume, MUNGU hawez kuwa upande wako kila siku
 
Hapana, mahusiano nimeanza tangu nikiwa na miaka16, kwa sasa nina 27yrs , yy ana 24.

Sema katika kipindi chote cha historia ya mahusiano yangu, haijawahi kuvuka miezi 6 na mwanamke.

Wa kwanza tulipendana sana tukaa miezi 4, mwanamke wa pili niliyekaa nae kwny mahusiano ilikuwa miezi5 na uyu ni miezi 6 sasa.

Ukiacha yale mahusiano mengi ya muda mfupi.
Nimekuelewa mkuu..ushauri wangu nikwamba achana na huyo binti haraka iwezekavyo , soon atakuweka kwenye shimo ambalo hutaweza kutoka kabisa
 
Asante sana, japo jana ametuma wadogo zake kwangu. Hawakunikuta
Hata akimtuma shangazi yake... kaka huyu ukioa atakusumbua ..utapata presha mbeleni. Ni either ufanye maamuzi sasa au uteseke ww na kizazi chako... chaguo ni lako
 
Jela ama kifo vinapiga hodi mlangoni kwako... achana nae kabisa, ila kabla inabidi uondoe hicho ulifanyiwa 'dawa' either kwa maombi au njia nyingine otherwise ni kazi bure, hata ukioa utamfuata tu. hayo maoni yangu.
 
Batoto ba siku hizi bakho na bichwa ngumu sana dada mkuu
Yani bado nashindwa kumuelewa huyu kijana au ndo wale walisomaga seminary wanawake wamewajua wakiwa kazini,,usikute hata hyo mimba haikuepo anakwambia tu akuumize moyo wanawake akili zetu tunazijuaga wenyew bhana
 
Habari zenu ndugu zangu, matumaini yangu ya wazi kuwa hamjambo na mnaendelea na harakati za kulisukuma gurudumu la Maisha.

Kwa upande wangu weekend ya leo haijakaa sawa, nahisi kuchanganyika, Presha sio presha, kuumwa sio kuumwa, yaani kwa ujumla hali ni mbaya.

Nikianza na mkasa wangu huu wa mapenzi ambao umenitokea kati yangu mimi na mpenzi wangu ambaye kiukweli nilitokea kumpenda sana na kushindwa kujizuia.

Awali nilikuwa naishi Dsm sema nikaamishwa kikazi kwenda Mwanza, kazi yangu ni nzuri na kama kijana nimeweza kumudu kupanga nyumba nzuri na kausafiri ka kutembelea.

Nakumbuka ilikuwa mwezi wa 9 mwaka Jana ndio nilikutana na huyu mwanamke kwenye klabu moja hivi jijini Mwanza. Hakika nilitokea kumpenda. Safari ya mahusiano ikaanzia hapo.

Kumbe historia ya huyu Crush wangu haikuwa nzuri hasa kutokana na background yake ya watu aliotoka nao kipindi cha nyuma, watoto wa mjini wanasema MDANGAJI.

Ama kweli mapenzi upofu ndio naamini, licha ya kufikishiwa habari zake lakini binafsi sikuzitilia maanani sana, nilijisemea moyoni kwamba nitamrekebisha aje kuwa Mama watoto wangu.

Kwa ufupi kwenye mahusiano yetu ya kipindi cha miezi 6 tumepitia katika changamoto nyingi sana, tumewahi kuachana na kurudiana zaidi ya mara tano. Chanzo kikubwa cha kugombana kwetu ni huyu mwanamke kuendekeza sana starehe. Ikifika weekend kama ya leo ni lazima mtoke.

Hata Kama nikimshauri tusitoke basi atatumia mbinu yeyote atoke kisha arudi asubuhi anigongee au arudi Kulala nyumbani kwake, mbaya zaidi kichwa cha pombe hana.

Tatizo lingine ni kuendeleza mawasiliano na ex's zake, nimefumania text za whatsapp na kawaida akichart na ma-ex wake. Nilikuwa nikijaribu kumwambia abadilike anaacha kwa muda kisha anaendelea. Mbaya zaidi kwny simu niliyomnunulia.

Nakumbuka siku moja tulitoka club ukazuka ugomvi baina yetu ambao ulipelekea nimtembezee kipigo cha mbwa koko. Kipindi hicho alikuwa hajapata kazi. Kila kitu nilikuwa najitaidi kumuhudumia ukiacha kodi ya nyumba aliyokuwa akilipa mwenyewe.

Baada ya ugomvi huu uliopelekea akae ndani wiki nzima kutokana na majeraha ulimpelekea aka-abort mimba yangu ya mwezi mmoja. Penzi likavunjika na kila mtu akachukua time zake.

Ukapita mwezi m1 bila mawasiliano, nilichofanya kosa nikaanza kutembea na rafiki zake ambao kwa idadi wanafika wanne. Drama zote hizi alikuwa akizishuhudia na nyingine kupelekewa taarifa.

Baada ya kufanya upumbavu wote huu, nilirudi nyuma na kujitafakari upya na kuamua kumtafuta na mapenzi yakarudi upya. Kipindi hiki alikuwa kwny mahusiano na Mzee mmoja mume wa mtu ambaye alikuwa akimsaidia katika mahitaji yake.

Tukashauriana tukapime afya zetu, bahati nzuri hatukukutwa na maambukizi, lakini kumbe huyu mwenzangu alipanga afanye revenge pasipo mimi kujua.

Kwanza aliweka utaratibu ambao naweza kusema sio sahihi, yaani yeye atakuwa na yule babu kimaslahi na hata nilipokuwa nawakuta sehemu nilijifanya kama siwajui mpk yule Mzee atakapokuwa ameendoka.

Hali hii ilinisumbua sana hasa ukizingatia wivu ulikuwa juu zaidi, kama hiyo haitoshi hivi majuzi katoa kali, alikuwa anakunywa na Mzee wake, baada ya Mzee kusepa akaja ex wake wa zamani ambaye yupo vzr kifedha.

Baada ya kuona picha ile kiukweli nilizidiwa na wivu na kusababisha ugomvi Mkubwa ambao Kama sio mkono wa Mungu huyu mwanamke angekuwa Marehemu.

Nimekaa nikaona hapana kwa hili lilotokea ngoja nije niombe ushauri kwa wakubwa zangu ambao huenda Wakawa wamepitia kwenye changamoto kama hizi waweze kunishauri haya.

Nimtafute nimuombe radhi maana moyo wangu bado unampenda? Au ni-move on na Maisha yangu? Labda huenda haikuwa ridhki aliyoniandikia Mwenyezi Mungu.

Nipo kwenye hali mbaya. Nakaribisha ushauri na wale ndugu zangu wa matusi na kejeli nawakaribisha pia.

Nawasilisha.
Mwanmke wa Club unataka awe wa kwako mwenyewe...
 
Wewe kweli kaka mgeni,inaonekana ni mgeni wa hayo mambo,.......hv unajua kulinganisha kwelii,mdada wa club umweke ndani,
 
Mlikutania club alafu unashangaa yeye kupenda sana starehe!! Vumilia tu mkuu.
 
Jela ama kifo vinapiga hodi mlangoni kwako... achana nae kabisa, ila kabla inabidi uondoe hicho ulifanyiwa 'dawa' either kwa maombi au njia nyingine otherwise ni kazi bure, hata ukioa utamfuata tu. hayo maoni yangu.
Nahisi dawa sio bure huyu Mwanamke, nimemfata kwake tumeombana msamaha, amenieleza sababu za kufanya yote. Ameniahidi atabadilika. Navyoandika sasa tupo wote. Moyo wangu nahisi una amani. Hakika hii sio bure
 
Yani bado nashindwa kumuelewa huyu kijana au ndo wale walisomaga seminary wanawake wamewajua wakiwa kazini,,usikute hata hyo mimba haikuepo anakwambia tu akuumize moyo wanawake akili zetu tunazijuaga wenyew bhana
Nahisi dawa sio bure huyu Mwanamke, nimemfata kwake tumeombana msamaha, amenieleza sababu za kufanya yote. Ameniahidi atabadilika. Navyoandika sasa tupo wote. Moyo wangu nahisi una amani. Hakika hii sio bure
 
Yani bado nashindwa kumuelewa huyu kijana au ndo wale walisomaga seminary wanawake wamewajua wakiwa kazini,,usikute hata hyo mimba haikuepo anakwambia tu akuumize moyo wanawake akili zetu tunazijuaga wenyew bhana
Hapana nina historia nzuri tuu ya mahusiano na huyu sio Mwanamke wangu wa kwanza, cha ajabu ni kwamba najiuliza kwann nashindwa kumuacha?
 
Nahisi dawa sio bure huyu Mwanamke, nimemfata kwake tumeombana msamaha, amenieleza sababu za kufanya yote. Ameniahidi atabadilika. Navyoandika sasa tupo wote. Moyo wangu nahisi una amani. Hakika hii sio bure
We kaka rudi kwenu jamani jaribu kumueleza mtu mzima atakushauri na ufanyiwe sawa au maombi hapo utakufa mapema shaurilako
 
Kati ya wewe au mapenzi kuna bwege either ww au mapenzi, aliekupatia hio kaxi ndie kakuonea zaidi
 
We kaka rudi kwenu jamani jaribu kumueleza mtu mzima atakushauri na ufanyiwe sawa au maombi hapo utakufa mapema shaurilako
Asante kwa ushauri, tatizo nikiwa mbali nae moyo unaweweseka na kukosa amani kbs. Nitajitaidi kulifikisha kwa wazazi na viongozi Wangu wa kiroho
 
Kati ya wewe au mapenzi kuna bwege either ww au mapenzi, aliekupatia hio kaxi ndie kakuonea zaidi
Nahisi kuna vitu kanifanyia huyu Mwanamke, Mimi ni mwanaume mwenye misimamo, smart na muelewa. Hata mahusiano yangu yaliyopita niliweza ku-move on, ajabu uyu Mwanamke nanishangaa nashindwa kbs
 
Nahisi kuna vitu kanifanyia huyu Mwanamke, Mimi ni mwanaume mwenye misimamo, smart na muelewa. Hata mahusiano yangu yaliyopita niliweza ku-move on, ajabu uyu Mwanamke nanishangaa nashindwa kbs
Msimamo upi ulionao?? Huo wa kumuacha demu amegwe kisa pesa huku unaona au
 
Back
Top Bottom