Habari za muda huu wakubwa.
Mimi ni kijana wa kiume ambae nimebahatika kupata sehemu yangu ya urithi toka kwa wazee wangu ambapo nimepata milioni 30.
Nilikua naomba wazoefu, watu mnaoifanya hii biashara tusaidiane kwenye mambo kadhaa juu ya hii biashara kama eneo, mbinu za kuongeza mauzo, nk.
Kwanini nimeomba ushauri juu ya kufungua pharmacy tu jibu ni sababu ni taaluma yangu(Pharmaceutical Technician), naipenda, nina uzoefu na ujuzi wa kuuza dawa japo sijawahi kufanya biashara yoyote ile ya kwangu ndo nataka kuanza.
Kwasasa nimeajiriwa kwenye community pharmacy flani Tanga Mjini. Nimefanya utafiti wangu kwa huu mji naona kama sitafikia malengo ya mauzo mazuri ukizingatia kuna wingi wa pharmacy za jumla, aina ya wakazi wake wamekariri baadhi ya maduka kua ndio yenye dawa za bei nafuu tu, wingi wa pharmacy mpya katikati ya mji(hapa ikumbukwe Tanga sio kubwa kwa mjini ambapo unaweza ukazunguka kwa masaa kadhaa ukaumaliza).
Kinachoniumiza ni location maana hapa najua hua ni kila kitu katika hii biashara ni wapi niende? Eneo/mkoa gani? Hali ya kiuchumi ya huo mkoa/eneo? Je miundombinu za usafirishaji kwenye hilo eneo/mkoa ukoje kama nikifanya order ya dawa zitachukua mda gani hadi zinifikie? Unafuu wa dawa nk.
Muuzaji nitakua mimi mwenyewe japo nilikua nafikiria kuajiri mtu wa jinsia ya kike mwenye dispensing certificate kubalance gender ili kutokosa baadhi wa wateja ambao hua hawako huru kuelezea tatizo lake hasa la baadhi ya magonjwa kwa mhudumu ambae sio wa jinsia yake.(hili nimelishuhudia mtu anaondoka kabisa kwakuona aibu)
Hivyo gharama kubwa itabaki kwa mfamasia ambae nitatumia cheti chake, mashelf, milango na karabati nyinginezo, kodi pamoja na kuagiza mzigo.
Nawaza hadi kichwa kinapata moto wakuu, nipeni mawili matatu wenye uzoefu na hii biashara hapahapa au hata ikiwa PM pia sawa nitashukuru sana.
Asanteni.