Nahitaji ushauri: Namna ya kupiga plasta katika nyumba

Nahitaji ushauri: Namna ya kupiga plasta katika nyumba

Sio ukuta wote unaochafuka, ni kule chini tu na kisababishi hasa ni pale maji ya mvua yanapobounce na kwenda ukutani. Paka rangi nyeusi au weka tiles za ukuta sentimenta (60cm sio mbaya) chache kutokea chino

Sent using Jamii Forums mobile app
Tilez za cutting kuta za nje zile zipi ni nzuri na je zinafaa and are they not expensive

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu zangu, Salaam!!

Nipo ktk hatua ya kupiga plasta nyumba yangu. Na kwa kuwa nina fedha kiasi kidogo nimeamua kuanza kupiga plasta kuta za ndani, na baadae nitamalizia upande wa nje.

Ninachoomba kutoka kwenu ni msaada wa kitaalamu, maana mafundi ninaowategemea (fundi wa plasta na wa rangi) wana maoni tofauti.

Fundi wa plasta anasema, plasta nzuri ni ile inayopigwa baada ya kuchanganya cement, mchanga na chokaa. Wakati fundi atakayepaka rangi anashauri kuwa ili aje apake rangi vizuri na kuepuka rangi kubanduka baada ya muda mfupi ni vema plasta iwe inatokana ya mchanganyiko wa mchanga na cement tu.


Ushauri wenu (mafundi na wataalamu wa masuala ya plasta na rangi) ni muhimu sana.

Plasta ipi ni bora??
Akupigie plasta ya kawaida bila chokaa,tena iwe plasta ya mkono bao na sio steel galamara(plasta ya mkono bao inaacha voids ambazo hushikilia skimming na rangi),plasta ukiimwagilia baada ya siku 7 ikikauka fundi rangi afanye skiming ya gypsum powder na rangi kwa kuta za ndani ambazo haziathiriwi na unyevu,na askimu PVA na cement kuta za nje(zinazoathiriwa au kuguswa na maji ya mvua) na zile za bafuni,hii itakusaidia rangi kukaa mda mrefu bila kuvimba,
Plasta ya mchanganyo na chokaa ni mbaya maana inafanya kuta iwe smooth kama imepigwa polish hvyo ukipaka rangi inakuwa iko juu juu haiingii kwa ndan,baada ya mda hyo rangi n lazma ibanduke,kwa ufanisi na uzur wa jengo hakikisha fundi plasta anyooshe plasta asitengeneze ikawa na mawimbi,fundi rangi nae akupigie skimming iliyonyooka na kupiga msasa vzuri bila kuchubua hyo skiming,hapo rangi ikipakwa utafurah,maana ikiwa tofauti utapachukia kama taa ikiwashwa utaona matuta kibao
ukutani
NIMEKUSHAURI MAANA MM NI EXPERT WA UJENZI,ASANTE
 
Zinaweza kusababisha ukungu au rangi kubabuka,rangi inakuwa kama imevimba then inabanduka.Japo ukungu na rangi kubabuka inaweza kusababishwa na vitu vingine pia.
Nijuavyo mm n kwamba gypsum powder n nzuri kwa kuskimu kuta ambazo haziguswi na maji yaan za ndani(gypsum n nzur),ila kwa kuta ambazo huguswa na maji mfano bafuni au choon ingawaje utaweka wall tiles,na kuta za nje n vyema ukatumia PVA(ant bacteria) ambayo huichanganya na cement then unaskimu,hapo rangi haitovimba
 
Kingereza chake sijui vzr ila hii puchi mara nying inapigwa nje ya nyumba ila kwasasa hapa kwetu arusha kama ni mfanyabiashara hasa wa nyumba za kupanga wanafanya hii kitu sana angalia hii picha japo ni chafu kidog

Picture1.jpg
Mkuu lweli hiyo picha ni chafu maana hata haifunguki
 
Ujenzi wa kisasa ni ule wa mchanga na cement tu,kama fundi rangi alivyokushauri,baada ya hapo una skeem kwa gypsum powder kwa ndani,nje unatumia whitr cement.
Kwa ndani baada ya skeeming,unapiga msasa ili kuweka ukuta laini zaidi,halafu unapaka PRIMER kabla ya rangi ili kulifanya vumbi la msasa na gypsum powder kushikana vizuri na kuimarisha rangi inayokuja.UMEMALIZA.
kizamani watu baada ya plaster waliweka "NIL" hiyo ya chokaa,lakini ukija kupinga rangi za kisasa kama WASH N WEAR huwa zinabanduka,inabidi utumie EMULSION pekee.LONG TIME.
 
Back
Top Bottom