Nahitaji ushauri: Namna ya kupiga plasta katika nyumba

Bado sijaelewa puchi ni nini hasa?

Muulize Fundi atakuambia H=Inapigwa njee ya Nyumba mkuu ningekuwa najua kingereza ningekuambia ...Ila mkuu inamaana wew sio mbongo??Kweli hujui puchi au unafanya makusudi mkuu
 
Ndugu zangu, Salaam!!

Nipo ktk hatua ya kupiga plasta nyumba yangu. Na kwa kuwa nina fedha kiasi kidogo nimeamua kuanza kupiga plasta kuta za ndani, na baadae nitamalizia upande wa nje.

Ninachoomba kutoka kwenu ni msaada wa kitaalamu, maana mafundi ninaowategemea (fundi wa plasta na wa rangi) wana maoni tofauti.

Fundi wa plasta anasema, plasta nzuri ni ile inayopigwa baada ya kuchanganya cement, mchanga na chokaa. Wakati fundi atakayepaka rangi anashauri kuwa ili aje apake rangi vizuri na kuepuka rangi kubanduka baada ya muda mfupi ni vema plasta iwe inatokana ya mchanganyiko wa mchanga na cement tu.

Ushauri wenu (mafundi na wataalamu wa masuala ya plasta na rangi) ni muhimu sana.

Plasta ipi ni bora??
Niaje mkuu,kabla ya kupiga hakikisha umeweka bomba za umeme ukutani,mie ni fundi kama utanihitaji tuwasiliane 0718 30 21 32
 
Mkuu kuhusu kuchanganya chokaa cement na mchanga hapo sina uhakika napo kwa kweli japo hapa sound vizuri.

Watu wengi naona wamekushauri upige unga wa gypsum na kweli hivyo ndivyo watu wengi wanavyofanya ila kwa uhakika kabisa kwamba gypsum powder ukutani ni sumu,itakuharibia kuta zako.

Wanatumia kulainisha ukuta,na kweli inapendeza ila kuna product maalum kwa ajili ya hiyo kazi na sio gypsum powder.

Hata sijui nani alianzisha hii yakupaka huu unga ukutani.

Ungetutajia hiyo product ya kulainisha Ukuta badala ya Gypsum Powder ungetusaidia wengi.

Pia ututajie na madhara ya Gypsum Powder kwenye Ukuta,kwani ndio material inayotumiwa kwa sasa.
 
KWA MIKOANI MCHANGA HAUNA CHUNVI NA MAJI YA KUJENGEA HAYANA CHUNVI
KWAHIYO PLASTA UNACHANGANYA MCHANGA NA CEMENT TU!

KWA DAR ES SALAM NA PWANI MAJI YA KUJENGEA YANACHUNVI MCHANGA UNACHUNVI UNASHAURIWA KUCHANGANYA NA CHOKAA ILI KUUA ILE CHUNVI inamaanisha ukiweka CHOKAA+CEMENT+MCHANGA plasta itakuwa imara, huyo FUNDI UJENZI YUPO SAHIHI KUTOKANA NA KIASI CHA CHUNVI KILICHOPO ENEO UNALOJENGA, DSM NA PWANI WAJANJA HUFANYA HIVYO

Mmmhhhh.... hii ndo naisikia kwako kwa mara ya kwanza.

Watu kibao wanapiga plasta ya cement na mchanga peke yake na plasta zinakuwa imara sana tu.

Mimi mwenyewe ni shuhuda wa hili.
 
Muulize Fundi atakuambia H=Inapigwa njee ya Nyumba mkuu ningekuwa najua kingereza ningekuambia ...Ila mkuu inamaana wew sio mbongo??Kweli hujui puchi au unafanya makusudi mkuu
Au una maanisha ripu?
 
Mkuu kuhusu kuchanganya chokaa cement na mchanga hapo sina uhakika napo kwa kweli japo hapa sound vizuri.

Watu wengi naona wamekushauri upige unga wa gypsum na kweli hivyo ndivyo watu wengi wanavyofanya ila kwa uhakika kabisa kwamba gypsum powder ukutani ni sumu,itakuharibia kuta zako.

Wanatumia kulainisha ukuta,na kweli inapendeza ila kuna product maalum kwa ajili ya hiyo kazi na sio gypsum powder.

Hata sijui nani alianzisha hii yakupaka huu unga ukutani.
Hujambo, nimeguswa na hii message ndio chanzo cha kujiunga na Jamiiforums badala yakupaka gypsum powder ukutani kabla ya rangi tupake nini?
 
Mwambie fundi wako ya kwamba hutaki a skimm kwa kutumia gypsum powder na atakuelewa.Pia ukipenda mwambie pia atumie primer hasa kwenye kuta za nje.
 
Ndio nimekuelewa ila mimi nnajenga bujumbura burundi maji sio ya chumvi, je unawezanisaidia kunijulisha nini madhara ya gypsum kwa kuta za ndani
 
Zinaweza kusababisha ukungu au rangi kubabuka,rangi inakuwa kama imevimba then inabanduka.Japo ukungu na rangi kubabuka inaweza kusababishwa na vitu vingine pia.
 
Sawa sawa nimekuelewa nashkuru kwa ushauri wako sababu ndio hatua nimedkia kwa sasa
 
Ndugu zangu, Salaam!!

Nipo ktk hatua ya kupiga plasta nyumba yangu. Na kwa kuwa nina fedha kiasi kidogo nimeamua kuanza kupiga plasta kuta za ndani, na baadae nitamalizia upande wa nje.

Ninachoomba kutoka kwenu ni msaada wa kitaalamu, maana mafundi ninaowategemea (fundi wa plasta na wa rangi) wana maoni tofauti.

Fundi wa plasta anasema, plasta nzuri ni ile inayopigwa baada ya kuchanganya cement, mchanga na chokaa. Wakati fundi atakayepaka rangi anashauri kuwa ili aje apake rangi vizuri na kuepuka rangi kubanduka baada ya muda mfupi ni vema plasta iwe inatokana ya mchanganyiko wa mchanga na cement tu.

Ushauri wenu (mafundi na wataalamu wa masuala ya plasta na rangi) ni muhimu sana.

Plasta ipi ni bora??
Mchanga na cement. Huyu wa chokaa mwambie siku nyingine umemaliza
 
Jamani naomba tuendeleze kuujuzana, Mimi nataka kupiga plasta baada ya hapo niende hadi kwenye rangi ila nimekosa pa kushika maana kila MTU anakomenti lake please naomba mwenye kujua zaidi hatua nzuri za kufuata atusaidie zaid ili tuzidi kujifunza
 
Muulize Fundi atakuambia H=Inapigwa njee ya Nyumba mkuu ningekuwa najua kingereza ningekuambia ...Ila mkuu inamaana wew sio mbongo??Kweli hujui puchi au unafanya makusudi mkuu
Nadhani unamaanisha "chipping". Ule upeleupele unaowekwa kwenye ukuta wa nje.
 
Back
Top Bottom