Nahitaji ushauri: Namna ya kupiga plasta katika nyumba

Nahitaji ushauri: Namna ya kupiga plasta katika nyumba

kikaniki

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2014
Posts
508
Reaction score
979
Ndugu zangu, Salaam!!

Nipo ktk hatua ya kupiga plasta nyumba yangu. Na kwa kuwa nina fedha kiasi kidogo nimeamua kuanza kupiga plasta kuta za ndani, na baadae nitamalizia upande wa nje.

Ninachoomba kutoka kwenu ni msaada wa kitaalamu, maana mafundi ninaowategemea (fundi wa plasta na wa rangi) wana maoni tofauti.

Fundi wa plasta anasema, plasta nzuri ni ile inayopigwa baada ya kuchanganya cement, mchanga na chokaa. Wakati fundi atakayepaka rangi anashauri kuwa ili aje apake rangi vizuri na kuepuka rangi kubanduka baada ya muda mfupi ni vema plasta iwe inatokana ya mchanganyiko wa mchanga na cement tu.

Ushauri wenu (mafundi na wataalamu wa masuala ya plasta na rangi) ni muhimu sana.

Plasta ipi ni bora??
 
mkuu wataalam watafika..ila ni vema unapiga plasta ya cement na Mchanga bila kusahau kufanya skimming hii itakurahisishia kutumia Nguvu ndogo sana kwenye rangi
 
mkuu wataalam watafika..ila ni vema unapiga plasta ya cement na Mchanga bila kusahau kufanya skimming hii itakurahisishia kutumia Nguvu ndogo sana kwenye rangi
Asante sana@mchepuko. Hivi chokaa huwa ina function gani katika plasta?
 
Mkuu chokaa usiweke kabsa, kuna fundi alinishauri hivyo ila baada ya kupiga plasta , nilipopaka rangi ikawa inabanduka, ilibidi nitoe plasta yote tena. Plasta changanya cement na mchanga tuu, hakikisha unapata mchanga mzuri pia
 
je ukatumia hiyo plasta ya kuchanganya na chokaa na badala ya kupiga rangi uka tumia wallpaper hizi wanazo promote inakuaje hapo wakuu
 
ukishapiga plasta nyumba yako utapaka gypsum powder tayar kwa Rangi....kama utafanya skiming mzuri bac utapiga Rangi moja kwa moja baada ya plasta hii itakupunguzia SNA garama...mwambie fund wako afanye plasta na skimng apo apo..
 
Mkuu chokaa usiweke kabsa, kuna fundi alinishauri hivyo ila baada ya kupiga plasta , nilipopaka rangi ikawa inabanduka, ilibidi nitoe plasta yote tena. Plasta changanya cement na mchanga tuu, hakikisha unapata mchanga mzuri pia

Asante sana Nsuri. Haya mambo ni vema ukishirikisha wadau
 
plasta.. ni cement na mchanga tuuuu... huyo anaetaka kukuchanganyia na chokaa ataharibu.
 
KWA MIKOANI MCHANGA HAUNA CHUNVI NA MAJI YA KUJENGEA HAYANA CHUNVI
KWAHIYO PLASTA UNACHANGANYA MCHANGA NA CEMENT TU!

KWA DAR ES SALAM NA PWANI MAJI YA KUJENGEA YANACHUNVI MCHANGA UNACHUNVI UNASHAURIWA KUCHANGANYA NA CHOKAA ILI KUUA ILE CHUNVI inamaanisha ukiweka CHOKAA+CEMENT+MCHANGA plasta itakuwa imara, huyo FUNDI UJENZI YUPO SAHIHI KUTOKANA NA KIASI CHA CHUNVI KILICHOPO ENEO UNALOJENGA, DSM NA PWANI WAJANJA HUFANYA HIVYO
 
CEMENT ENEO LENYE CHUNVI HUPUNGUA UWEZO WAKE MAPEMA KULIKO ENEO LISILO NA CHUNVI ili kuondoa chunvi unashauriwa kuchanganya na CHOKAA, au ujenge kwa kutumia maji yasiyo nachunvi MAENEO MENGI YA PWANI YANA CHUNVI NDO MAANA FUNDI AKAKUSHAURI UTUMIE CHOKAA KUPUNGUZA CONCENTRATION YA SALT KWENYE MCHANGA NA MAJI
 
Siku hivi watu wanafanya hivi, plasta ni mchanga na cement, usiweke cement kama marun, baada ya hapo unapiga plasta ya,gypsum nyembamba sana nyumba nzima kama marun, baadae ukitia rangi kama kiyoo shine
 
Mi ni fundi wa vyote ushauri wangu sasa ni hiv, kama una2mia maji yenye chumvi kwa ujenzi ni vema ukachanganya huo mchanga na cement na chokaa wakat wa plaster ili utakapopaka rangi idumu. Na km maji hayana chumvi changanya mchanga na cement piga plaster yako ikikauka vizur km una uwezo skim kwa gypsum powder kisha paka rangi yako huo ukuta wa ndan lakn ukuta wa nje baada ya plaster skim kwa white cement kisha paka rangi yako.UTAIPENDA.
 
Mim ningekuwa wew nisingepiga plasta ila ntapiga Puchi ndani na Nje kisha ndani wakati napiga ndani kwa ajili ya decoration lazima ichanganywena gypsum powder itakayofanya kuta iwe soft sana alaf napiga nari ninayotaka nyumba inakuwa fresh kbs
 
Mkuu unamaanisha nini unaposema "Puchi" naomba hio elimu kaka.
 
Mkuu unamaanisha nini unaposema "Puchi" naomba hio elimu kaka.

Kingereza chake sijui vzr ila hii puchi mara nying inapigwa nje ya nyumba ila kwasasa hapa kwetu arusha kama ni mfanyabiashara hasa wa nyumba za kupanga wanafanya hii kitu sana angalia hii picha japo ni chafu kidog
Picture1.jpg
 
Mkuu kuhusu kuchanganya chokaa cement na mchanga hapo sina uhakika napo kwa kweli japo hapa sound vizuri.

Watu wengi naona wamekushauri upige unga wa gypsum na kweli hivyo ndivyo watu wengi wanavyofanya ila kwa uhakika kabisa kwamba gypsum powder ukutani ni sumu,itakuharibia kuta zako.

Wanatumia kulainisha ukuta,na kweli inapendeza ila kuna product maalum kwa ajili ya hiyo kazi na sio gypsum powder.

Hata sijui nani alianzisha hii yakupaka huu unga ukutani.
 
Mi ni fundi wa vyote ushauri wangu sasa ni hiv, kama una2mia maji yenye chumvi kwa ujenzi ni vema ukachanganya huo mchanga na cement na chokaa wakat wa plaster ili utakapopaka rangi idumu. Na km maji hayana chumvi changanya mchanga na cement piga plaster yako ikikauka vizur km una uwezo skim kwa gypsum powder kisha paka rangi yako huo ukuta wa ndan lakn ukuta wa nje baada ya plaster skim kwa white cement kisha paka rangi yako.UTAIPENDA.
Darasa zuri sana. Asante sana kwa somo
 
Kingereza chake sijui vzr ila hii puchi mara nying inapigwa nje ya nyumba ila kwasasa hapa kwetu arusha kama ni mfanyabiashara hasa wa nyumba za kupanga wanafanya hii kitu sana angalia hii picha japo ni chafu kidog
Picture1.jpg

Bado sijaelewa puchi ni nini hasa?
 
Back
Top Bottom