Hapa kejeli hazisaidii kitu.
Mleta mada ya uhitaji alikuwa na nia nzuri saana tu,ila naona malumbano yamefikia sipo kabisaa kwenye Lengo.
Zaidi ya kuoneshana mie nani na wewe nani.Na sasa mie tajiri na mie Tajiri.
Halafu Asprin wewe ni mzoefu sana wa jukwaa hili,sijafikiria kama mnawez kufika hatua hii katika post hii.
Mwenzio akipandisha Jazba,sio lazima wote mpandishe Jazba mwisho wa siku woote mnakuwa hamna faida.Na mbaya zaidi mnawapoteza hata wasiohusika na ugomvi wenu na wengine wanaingilia malumbano bila hata kujua.So,end of the day hata muuzaji na mteja kunakuwa hakuna link nzuri tena.
Kununua kitu used sidhani kama ni umaskini au utajiri.Hata Hammer kwenye zoom zipo zinauzwa used.Je mwenye kununua hammer ni maskini.
Mie naamini mtu ananunua kulingana na hali yake,na hata kama mtu kuitwa maskini sidhani kama ni tusi,maana hakuna anaejua hali ya mwenzie.Tajiri ni Mungu peke peke yake mwenye kutupa Pumzi na uzima na wote kuamka Salama.
Ukiamka mzima tu basi wewe jua ni Tajiri,hayo mengine ni majaaliwa tu ya kipato.
Dhamira ya maisha kwa kila binaadam anaijua ni Mungu peke yake,na sio kila hatari ni hatari kwa wote.Unaweza kulala na kuamka mgonjwa au maiti.
Kwahiyo kama ananunua ili afanye Biashara ya Bodaboda cha msingi ni kumpa moyo kwamba awe makini tu kama kijana mwenzio.Maana mchango wa mawazo utakaompa,na kumuombea kwa mungu kwamba mungu amlinde katika biashara hiyo.Basi Mungu anakulipa zaidi bila wewe kujua.
Yangu ni hayo,turejee kwenye track