Nahitaji msichana wa kuoa

lovefamily

Member
Mar 20, 2017
18
3
Habari zenu wapendwa. Naamini JF ni sehemu nzuri sana ya kufahamiana. Nimeshuhudia watu waliooana kipitia jf.Hivyo nami naamini nawezapata mke kupitia humu. Mimi nina 43yrs. nimejiajiri, mrefu (5.6), maji ya kunde, mbena, nimeokoka. Nina mtoto mmoja wa miaka 9. Nilitalikiana na mke miaka 6 iliyopita. Naishi Dar.

Nimtakaye: Awe ameokoka kwelikweli, urefu 4.10 hadi 5.0, mweupe wa asili si wa mchina, umbo la kati, awe tayari kumpokea binti yangu bila ubaguzi, asiwe na mtoto wala kutoa mimba, afahamu vizuri maana ya ndoa. awe tayari kupima UKIMWI. Umri kati ya miaka 20 hadi 28. elimu ya chini form four. Asiwe na kazi ya kuajiriwa. Wazazi au familia yake isiwe na imani za kienyeji yaani matambiko, masangoma, uchawi n.k.

Mwenye sifa hizo ani PM.
 
Wow! Age yako iko poa.. Wish i could be hata rafk ako coz ushafanya meng now umesettle
 
Mkuu Mungu wetu habagui wewe umeanzaje???? Ukikupa mwenye vigezo tofauti na hivyo utamkataa????

Ushauri wangu ingia kwenye maombi akufunulie kama yupo aliyekuwekea.
Mungu atabaguaje wakati watu wote ni wake? Lakini mwanadamu yeyote lazima awe na vigezo vya yule amtakaye ili angalau kwa sehemu nafsi yake iridhike. Na Mungu anasema ukiomba lolote sawa sawa na mapenzi yake utapewa. Na hakuna sehemu specific ya kupata mke, Mungu anaweza kukukutanisha na mwenzio hata kupitia mtandaoni.

Kama Mungu atanipa mtu ambaye hana vigezo vyangu itakuwa ni kwa sababu maalum na atanipa moyo wa kumkubali nami nikithibitisha hivyo nitampokea bila shaka, maana Mungu hafanyi makosa. He is always perfect and right.
 
Kwa vigezo hivyo ulistahiki kabisa kumpa talaka mkeo
Kwani kuna kigezo gani kigumu hapo? Maana wenye sifa hizo wapo. Na kwa taarifa yako huyo wa kwanza alijitariki mwenyewe kwa ujinga wa kupotoshwa na watu na sasa anajuta. Mimi nasonga mbele na mwanangu.
 
Aisee wewe mbinafsi,una mtoto halafu unabagua mwanamke aliye na mtoto mmh utakua na matatizo kibao ndio maana ndoa ya kwanza ikakushinda.
Hakuna ubinafsi hapo! Mtoto huwa ni wa baba, hivyo sihitaji kuingia mashaka kisa eti baba wa mtoto ana mazungumzo na mke wangu. Na kwa walio wengi utakuta kigezo cha mtoto kinawarudisha kwenye mahusiano. Upande wangu toka huyo mwanamke aondoke nilikata mahusiano kabisa, na haitakuwa tena, sasa miaka sita imepita. Labda mtoto awe amefiwa na baba.
Kwani kuna kigezo gani kigumu hapo? Maana wenye sifa hizo wapo. Na kwa taarifa yako huyo wa kwanza alijitariki mwenyewe kwa ujinga wa kupotoshwa na watu na sasa anajuta. Mimi nasonga mbele na mwanangu.
 
Una mawazo ya kizamani sana,hapo unamaanisha hata huyu mpya atakae jitokeza mkishindwana(huku mmeshapata mtoto mwingine)utamnyang'anya mtoto kwa kigezo mtoto ni wa baba.
Hakuna ubinafsi hapo! Mtoto huwa ni wa baba, hivyo sihitaji kuingia mashaka kisa eti baba wa mtoto ana mazungumzo na mke wangu. Na kwa walio wengi utakuta kigezo cha mtoto kinawarudisha kwenye mahusiano. Upande wangu toka huyo mwanamke aondoke nilikata mahusiano kabisa, na haitakuwa tena, sasa miaka sita imepita. Labda mtoto awe amefiwa na baba.
 
Una mawazo ya kizamani sana,hapo unamaanisha hata huyu mpya atakae jitokeza mkishindwana(huku mmeshapata mtoto mwingine)utamnyang'anya mtoto kwa kigezo mtoto ni wa baba.
Huo ni mtazamo wako. Kisheria anayepaswa kutoa huduma za mtoto ni baba. Na mimi sitimui mke labda ajitimue mwenyewe. Na kama nikifanya hivyo si qualify kuoa tena, maana nitakuwa na hatia. Biblia inasema yeye asiye amini akitaka kuondoka na aondoke, ndipo huyo ndg mme au mke yu huru. Huyu alijitimua nwenyewe kwa kudhani amepata sasa anajuta, mtoto alimwacha mwenyewe akiwa na 2 yrs. Sikubabaika, nimemlea mwenyewe kwa hadi sasa she is 8yrs karibia 9yrs.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom