Nahitaji msaada wa mawazo na ushauri nini nifanye juu ya hii Tsh Milioni 8

Najenga ya kawaida sana tena vyumba vya madarasa itakapoishia ila hata isipokuwa na lipu ntakomaa baadae nipige lipu!
Inabidi ujenge kwa utulivu sana hiyo nyumba ya vyumba vitatu kwa milioni 6! Maana nyumba ina maajabu yake. Unatenga hiyo milioni 6, mwisho wa siku inakupeleka mpaka milioni 20!

Mbaya zaidi ukishaanza tu ujenzi, ndiyo basi tena! Huwezi kuishia katikati. Na hutafurahia kuona imeishia kwenye renta na inanyeshewa na mvua. Biashara awamu hii nayo siyo ya kufanyia majaribio.

Mzunguko wa hela mtaani siyo wa kuvutia sana kama zamani. Ni wabishi tu ndiyo wanatusua. Wenye mioyo myepesi wanafunga.
 
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza.

Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili.

Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili
Kiwanja unacho!!??
 
Huna uzoefu wa biashara tena katika awamu ambayo biashara ni ngumu!!! Kama una sehemu ya kuhifadhi, nunua bati 50, weka ndani. Nunua sementi mifuko 50, weka ndani. Tafuta ushauri kwa mifuko hiyo ya sementi na bati, utahitaji nondo na mbao kiasi gani, ukishapata jibu, nunua hivyo vitu, weka ndani! Pesa utakayobaki nayo ndiyo anza kujifunzia nayo kufanya biashara huku ukipiga tofali mdogo mdogo hata wewe mwenyewe
 
Aisee wazo zuri sana shukrani
 
Inabidi ujenge kwa utulivu sana hiyo nyumba ya vyumba vitatu kwa milioni 6! Maana nyumba ina maajabu yake. Unatenga hiyo milioni 6, mwisho wa siku inakupeleka mpaka milioni 20!

Mbaya zaidi ukishaanza tu ujenzi, ndiyo basi tena! Huwezi kuishia katikati. Na hutafurahia kuona imeishia kwenye renta na inanyeshewa na mvua. Biashara awamu hii nayo siyo ya kufanyia majaribio.

Mzunguko wa hela mtaani siyo wa kuvutia sana kama zamani. Ni wabishi tu ndiyo wanatusua. Wenye mioyo myepesi wanafunga.
Ni kweli kabisa sasa hapa niko njia panda ngoja nione
 
Katoro / Buselesele kuna mzunguko mkubwa mno wa pesa kwa sababu maeneo hayo yamezungukwa na wachimbaji wadogowadogo wengi wa gold. Sasa kama huwezi kuona ufanye nini Katoro au Buselesele ujue hutokaa uone cha kufanya sehemu yeyote Tanzania
Nikweli ndio maana nikahitaji utulivu kwanza ili nichanganue nafenye nini
 
Back
Top Bottom