Jumanne Mwita
JF-Expert Member
- Nov 18, 2014
- 424
- 1,044
Habarini za majukumu? Pamoja na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.
Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.
KWENU.
Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta napata mawazo ya hapa na pale, nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.
1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.
2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.
Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.
Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.
Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili