Nahitaji msaada wa mawazo na ushauri nini nifanye juu ya hii Tsh Milioni 8

kama upo katoro geita na uhakika hyo hela unaweza jenga nyumba hata 3 za kupangisha,, na fremu za maduka
Hata mimi nimemwambia mwenzake kwa milioni 5 tu nilijenga nyumba kubwa sana Kilosa, Morogoro na mzee wangu anakaa pale wanasema ni shule ama hahah, hela nyigni sana hiyo kwa nyumba za nje ya miji mikubwa
 
Nunua bodaboda 4 halfu funga mkataba wa miezi 13 kila pikipik iwe inaingiza 10000 kila siku.hakikisha mkataba wako unahusisha mamlaka ya kiserikal baada ya mwaka utakuwa bodaboda zaidi ya hizo pesa ya ziada
 
Inabidi ujenge kwa utulivu sana hiyo nyumba ya vyumba vitatu kwa milioni 6! Maana nyumba ina maajabu yake. Unatenga hiyo milioni 6, mwisho wa siku inakupeleka mpaka milioni 20!

Mbaya zaidi ukishaanza tu ujenzi, ndiyo basi tena! Huwezi kuishia katikati. Na hutafurahia kuona imeishia kwenye renta na inanyeshewa na mvua. Biashara awamu hii nayo siyo ya kufanyia majaribio.

Mzunguko wa hela mtaani siyo wa kuvutia sana kama zamani. Ni wabishi tu ndiyo wanatusua. Wenye mioyo myepesi wanafunga.
Uzuri nyumba ni kitu unachoweza kukaa chini, kabla ya kujenga, na kufanya makisio yote ya ujenzi. Ujenzi unaoshinda wengi ni ule mtu anakurupuka na kuanza kujenga bila kufanya plan yoyote. Akae chini afanye makisio ya kila kitu aone.
 
Sipajua Katoro na sijui wingi wa watu huko ila ningeshauri fanyia uchunguzi hiz biashara

1. Vifaa vya pikipiki na baiskeli
2. Kuna zile biashara machinga wanauza kama sosi, mikanda, saa n.l
3. Mahitaji ya vitu vya ndan - Mangi shop
No 1 kule sawa kbs
 
Km upo mkoani jenga nyumba hautajutia! Km upo mjini hasa Dar fungua tu biashara ya uwakala wa pesa au Mangi shop
 
Umeipataje pataje? kama unapata hela afu hujui uifanyie nini hii itakua umeipata ima umebet,umepewa,umeokota au umeipata kwenye urithi au madini... kama ni mkulima bora uirudishe kwenye kilimo,lakini kama mfanyakazi usianze biashara kwa hela ya "zali la mentali",jenga nyumba
 
Kama mtu hana experience ya biashara yoyote,basi kuweka pesa ktk biashara ni sawa na kununua gari bovu...
JENGA Nyumba simple angalau ujitahid upige hadi bati na madirisha, mengineyo utamalizia ukiwa ndani ya nyumba...
Kwa hali ya biashara kwasasa ni ngumu SANAAAAA usijaribu
 
Nunua gari mkuu
Najaribu kuwaza kama wewe ndo umeleta hili wazo hapa jukwaani alafu unapokea jibu kama hili ki ukweli tu sio jibu zuri kama uwezi kuchangia n bora kukaa kimya watu watachangia tu
 
Milioni tatu nunua gari GX100 engine beams 2000 6 cylinders.
Milioni tatu oa mke awe mzuri watu wageuze shingo wakipishana nae.
Hela iliyobaki SPORTPESA inahusu maana kwa hela hiyo una uhakika wa kupata nyingi zaidi na kusahau kazi kabisa hapa duniani. Kubeti kumewatoa wengi sana.
 
Habarini za majukumu? Pamona na hayo natumaini wote ni wazima pia! Mimi sijambo na naendelea na majukumu yangu ya kila siku kwa ajili ya maisha yangu ya sasa na ya baadae.

Katika kitu kinachonichanganya nikaona naweza kupata wapi mawazo mazuri na ya kujenga zaidi ya #JamiiForum. Nikasema hapana ngoja nifikishe ujumbe na wazo hili nililonalo ili niweze kuchanganua nawezaje kulifanya hili na nisije kujutia baadae.

KWENU.

Nimepata kiasi cha Tsh million 8 taslimu, hizi hela nimejikuta nianze na nini kati ya mambo makuu mawili ambayo ni.

1. Wazo la kwanza
Nimepanga nijenge nyumba ya vyumba 3 maana kiwanja ninacho kabla ya kupata hii pesa na kama ikibaki hata million 2 kwenye hiyo hela niangalie ntakachoiwekezea ili nisipate shida hapo baadae.

2. Wazo la pili
Hili ndio linaniumiza kichwa mpaka basi, kwanza nilitaka niifanyie biashara kwanza kabla haijaisha ili niikuze baadae ndio nijenge sasa maana kiwanja tayari ninacho.

Sasa najikuta nawaza nitaifanyia niashara gani wakati sina experience yeyote na biashara na sijui biashara gani ambayo nitawekeza hiyo hela ili nisije kujuta mbeleni huko.

Pia najikuta niko njia panda kati ya mawazo hayo mawili nimeshindwa nianze na lipi ambalo lingeniwezeshea hela hiyo ikatumika vyema na baadae nikaitwa mtu katika watu.

Nitangulize shukrani zangu kama mchango wako kwangu na mawazo yako ili niweze kulishinda hili

Kwenye ujenzi hiyo mil 8 utalala na viatu aiseeee ,nyumba ya vyumba vi3 ni kubwa sana au labda kama unataka kujenga polisi post ,ukifungua mlango upo nje,hakuna sebule,jiko,dining,store,wala public toilet.

Kama unataka kujenga polisi post unaweza kujenga ya kawaida na pia ukabakiza mil 2 ya biashara.
 
Mkuu, nakushauri usiingie kwenye biashara maana inaonekana hujui hata ABCs za biashara.

Fumba macho jenga nyumba uistiri familia yako. Hatujui kesho zetu, imagine linatokea la kutokea. Mungu akunusuru unapata ulemavu, utakimbilia kwa nani na dunia ya sasa?? Shemeji?? Watoto hata pa kukaa hawajapata!!!!

Jenga nyumba ndugu yangu hizi biashara baadae.

Ila pia swali la msingi ambalo inabidi utujibu ni pesa umezipataje?? Hili linaweza badilisha maono yetu katika kukushauri.

Am just saying.....
 
Jenga Kwanzaa akiba ya nyumba ndio hazina Isiyo halibika kilahisi.
Hizi biashara kunakufel au kutapeliwa

Maneno yangu siyo sheria kwamba lazima uyafuate
 
Ingiza kwenye mzunguko wa biashara, utakuja kunishukuru baadaye :)
La hajui ni biashara gani afanye utampoteza , biashara inataka kwanza taarifa za kutosha nini ufanye , sio juu kea juu na hela yako unafanya biashara , utachoma pesa yote
 
Biashara ndio sina experience nayo na sijawahi fanya biashara!
Jenga kwanza uwe kwako , hiyo mbili ndo uchezee kamari kwenye biashara , ukiweza Boda Boda unatusua fasta , epuka tu wake zetu na uwe na nidhamu barabarani
 
Milion8 kwa nyumba ya vyumba vitatu kisha ibaki milioni mbili? Inamaana nyumba vyumba vitatu utakuwa umejenga kwa mil.6? Kweli mkuu?
Ngumu ila anaweza akawa na plan ya kunyanyua chumba kimoja labda
Yote yanawezekana.
 
Back
Top Bottom